Taarifa kuhusu namna ya kujiunga na Ualimu baada ya kumaliza kidato cha 4

tata mvoni

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
534
81
NAOMBA MWENYE TAARIFA KUHUSU NAFASI ZA KUSOMEA UALIMU KWA WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE TUJUZANE. natanguliza shukrani
 
jamani nisaidieni chuo ambacho kinaweza kumchukua aliyepata division 4 ya 28 ni msichana hata binafsi naomba msaada wenu
 
Vyuo vingi vinachukua hadi div 4 ya 26 pts (nadhani hii ndio criteria ya NECTA), nadhani anaweza kuchukuliwa kwenye chuo ambako wana nafasi ya re-seat exams.
 
Mdogo wang alipata three ya 23 lakini hakupata chuo cha ualimu,shenz zao
 
[h=2]Tangazo kuhusu nafasi za mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti na stashahada kwa mwaka wamasomo 2012/2013[/h]
2. STASHAHADA YA UALIMU ELIMU MAALUM: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi au Sayansi ya Jamii na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili ;
(b) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari;
(c) Mwalimu anayefundisha watoto wenye mahitaji maalumu (wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili nk) ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).

3. STASHAHADA YA UALIMU SAYANSI KIMU: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:

(a) Mwalimu mwenye Cheti cha Ualimu Daraja A;
(b) Mwalimu mwenye Cheti cha ualimu Sayansi Kimu; na
(c) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua 'Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo ya ‘Biology, Chemistry and Nutrition'.

VIAMBATISHO/ MAELEZO MUHIMU
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu waambatishe vielelezo vifuatavyo:
(i) Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV na cha VI;
(ii) Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stahshahada (kwa Walimu kazini);
(iii) Barua za Walimu kazini zilizopitishwa na Waajiri;
(iv) Sifa zilizoelekezwa kwa kila kozi ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya ualimu katika vyuo vya ualimu vya Serikali na Vyuo Visivyo vya Serikali;
(v) Wahitimu wa Kidato cha 4 mwaka 2011 na Kidato cha 6 mwaka 2012 walioomba kupitia „Sel forms‟ wanatakiwa kutuma maombi upya kwa barua;
(vi) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu yatatolewa kwenye Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
(vii) Barua za kujiunga na mafunzo zitatolewa na chuo atakakopangwa mwombaji kwa kutumia anuani ya yake; na
(viii) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: WELCOME TO MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING OFFICIAL WEBSITE:::::::::, Ofisi za Makatibu Tawala (M) na Vyuo vya Ualimu.

MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 30/04/2012.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)



source: WELCOME TO MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING OFFICIAL WEBSITE:::::::::
 
Back
Top Bottom