Wakati wa Utawala wa Mwl. ilikuwa shida kweli kuonana na Rais Unaweza kufuatilia mazungumzo ya Edwin Mtei anavyosema hakuwa na muda wa kukutana na wawekezaji; aende wizara husika na kumalizana... Nyerere alikuwa anatoa miongozo na ifuatwa wakati waziri na wawekezaji wakijadili ...
Sidhani sasa ni Hivi... Picha na Rais - Kila kitu shwari
Usanii unaendelea....JK umaarufu wake ulivyoporomoka kila kamwanya kakujipandisha chat anataka akatumie bila kujali ataonekana vipi mbele ya walalahoi.Anataka aonekane mkombozi wa taifa letu kutoka katika giza (Ukosefu wa umeme)Ambapo chanzo ni yeye mwenyewe CCM na serikali yake.Ni changa jingine la macho kunakitu nyuma ya kampuni hii( Richmond,Dowans,symbion power n.k)Mitambo hii imekua KINYONGA kinachojibadilisha rangi kuchota pesa zetu za walalahoi wakati viongonzi MAFISADI wa chama TATIZO LA UMEME WAMELIGEUZA MRADI WA KUJINEEMESHA wanaendelea kutanua Richmond,dowans and then symbions power.Mitambo ile ile.Kama mitambo ni ile ile nini ilikua tatizo la Richmond?Nini tatizo la Dowans?Au kwanini serekali isinunue mitambao yake kwani mbali na kubadili majina ya wamiliki huduma inabaki kua ile ile na wizi ule ule.Kwa sababu mbali na mpango huo wa kubadili majina ya makampuni ya kua ni mpango wa mafisadi kuturubuni na kuendele kutuibia pia serikali inaingia gharama kibao kutoka mkataba hadi mkataba kulipia wanasheria na gharama nyingine kibao.JK inatosha!Kikwete anajirahisisha sana.Hii inanipa picha kwamba kuna hidden agenda.Why should Hinks go to see the President.Mambo haya yangeishia kwenye wizara husika na TANESCO.Kwanza mtambo wenyewe umegubikwa na kashfa chungu nzima.
Kama hauna magamba uweze kumeza hiyo, lakini kama umejaa magamba that is an order of the day. Chama kwanza mtu baadaye.