Swali la Ugomvi: Kwani Lowassa Kawa Mganga wa Kienyeji?

mtu hufananishwa na kile anachofanana nacho. Hakuna sababu yoyote ya msingi ya watu kumshabikia Lowassa zaidi ya ile nguvu ya pete anayovaa mkono wa kulia.

Try to be a bit scientific. Akili ya kudhania kama yako isiipotoshe nchi!
 
umekuwa kama mjinga siku hizi....kila thread yako lazima useme..''swali la ugomvi''....na pia umekuwa na kasumba ya kumponda lowassa...tuachie lowassa wetu...huyo magufuli ni malaika? kwanza aliokota embe dodo chini ya mwarobaini..hakufaa kuwa hapo...kinachokuwasha nini?
 
Yaaap mzeee umenena lowasa namfanisha na Mzee was loliondo Mzee masapila kwa mda mfupi watu walimwamini watu walimiminika wagojwa kitu kikombe cha babu kikapta umaharufu watu wakatoa wagojwa mahospital babu wA watu Leo anandinga kibao katajirika watu wakapoteza maisha ndugu wanajuta kuwatoa mma zao hospital bila kufikiria hasara watakayo ipata ile nyota ya Mzee yule iko kwa lowasa mnamjua vizuri eti lowasa msafi anafaa kuwa raising eti mabadiriko yeye alikuwa huko kwa nini asifanye mabadiko yeye na rafiki ake
 
huyu jamaa kawa kama mjinga flani hivi lakini kwa kifupi ni kwamba huyu ni mmoja wao wa wale wanaotaka watz waendelee kuwa na maisha duni ili wao waoendee kula kwa kisingizio cha kuwasemea watz...ni mtu wa ajabu sana huyu na mnafiki mkubwa...yeye ndo kamfikisha hapo alipofika dr mihogo na sasa anaendelea kuleta vi makala vyaka vya kpuuzi humu....
 
Since then I have locked these two persons in one cell; Mzee Mwanakijiji and Humphrey Polepole.
Since then, I have thrown the keys until on 28th October 2015 whereby, i will release them from the cell.

I hope, during that time, they both, will come into their senses!!!!
 
mganga.jpg

KWANI LOWASSA KAWA MGANGA WA KIENYEJI?
Na. M. M. Mwanakijiji

Jamii nyingi za Kiafrika (na inawezekana sehemu nyingine duniani) zina hofu kubwa ya watu ambao wanaaminiwa kuwa wana uwezo fulani hivi ama wa kudhuru watu au kuponya watu. Watu hawa wamepewa majina mbalimbali kutegemeana na kabila au mila na desturi za mahali; wanajulikana kwa majina mengi lakini kwa ujumla wao tunawatambua kama “waganga wa kienyeji”.

Waganga hawa wanatofautishwa vile vile; wapo wale ambao kazi yao kubwa ni kutibu kwa kutumia miti shamba na hawa hujulikana kama waganga wa tiba za “asili” na hawa hutumia zaidi madawa yatokanayo na miti na mimea (na hata wanyama) kujaribu kutibu wagonjwa wao. Kundi jingine ni la wale ambao hutumia siyo tu madawa mbalimbali bali pia hutumia “kunuia”; yaani wanaaminiwa wana uwezo wa kutoa maneno (sala, dua, maapizo n.k) ambayo yanachangia katika kuleta tiba kwa mtu au kumuondolea mtu matatizo yake. Hawa hujulikana zaidi kama waaguzi (seers); na katika kundi hili wapo wasoma nyota, viganja, alama za sayari, wenye kutumia vitabu vya kidini n.k
Katika hilo hilo kundi la pili wapo ambao pia huaminiwa kuwa siyo tu wana uwezo wa kutibu au kumuondolea mtu matatizo yake bali pia wanaweza (wakiamua kunuia) kumdhuru mtu na kumfanya mtu limfikie jambo baya. Kundi hili ni kundi la waganga wanaoogopwa sana kwani hawa ndio hujulikana katika lugha za wenzetu kuwa wanafanya “black magic” yaani wana uwezo wa kudhuru watu na wanapofanya hivyo basi tunawaita ni “wachawi”. Wachawi hasa ni kundi la mbali zaidi ambalo wao hawajishughulishi na tiba bali katika kudhuru watu (wawe na sababu au bila sababu). Wapo waganga ambao wanaanzia upande mmoja na mwisho wanaweza kujikuta upande mwingine kabisa.

Hata hivyo, watu wengi katika bara letu, nchini mwetu na hata sehemu nyingine duniani huwaendea zaidi wale waganga wenye kuonekana wana uwezo wa kutibu hasa wenye kuchanganya miti ya asili (mitishamba) na namna fulani ya kunuia. Waganga hawa wengine wakitumia mbinu za kimazingaombwe (viinimacho) wanaweza kabisa kuwaaminisha watu kuwa vitu fulani vipi au havipo na wanaweza kufanya vitokee au visitokee na hivyo kujijengea imani hasa. Na watu wa namna hii huogopwa sana hasa kwa vile inaaminika wana “uwezo fulani”. Karibu jamii zote duniani zimewahi kuwa na watu wa namna hii.

Katika nchi yetu hata hivyo, imani hii kwa waganga wa kienyeji inatokana na imani za kishirikina zaidi (superstitious beliefs). Tunaogopa vitu fulani fulani, tunaamini vitu fulani fulani, na wakati mwingine hata kuwafuata watu kwa sababu ya imani hizi hizi. Mtu akitaka kumtishia mtu mwingine basi anamwekea “hirizi” kwenye mlango wa ofisi yake na mtu huyo akiikuta anaweza kutahamaki kuwa wanataka kumroga (na anaweza kuwa ni msomi na PhD juu yake) lakini mara moja ataahirisha kwenda kazini siku hiyo na yeye aende “Bagamoyo” kwenda kutafuta Kinga. Na kama “Bagamoyo” alikokwenda hakuji na majibu ya kutosha basi anaweza kuamua kwenda “Sumbawanga”. “Sumbawanga” hiyo ikikataa basi anaweza akaamini waganga wakali zaidi wako “Tanga” na hivyo atatafuta safari ya kwenda Tanga! Maisha ya mtu huyo utaona mara moja yanazidi kuzama katika imani hizi kiasi kwamba hata dini kama alikuwa nayo inapotelea mbali au anachanganyia “mumo kwa mumo”.

Katika matatizo yote ya wananchi wenye kunufaika ni hawa waganga wa kienyeji hasa wale wenye majina ya kutisha zaidi na ambao sifa zao zimetangaa nchi nzima. Wapo – kwa mujibu wa vyanzo vingi – waganga ambao wanafanya “house calls”; yaani, hawa ni waganga ambao huweza kualikwa na kwenda kufanya huduma kwenye nyumba za watu hasa kama mtu mwenyewe hawezi kwenda kwa mganga huyo akaonekana. Wapo watu mashuhuri ambao hutembelewa na wengine wanao waganga wao ambao wako kwenye malipo yao!

Ukiangalia sana siasa zetu za mwaka huu ni lazima mtu ujiulize kama watu wanaomshabikia Lowassa wanafanya hivyo kwa vile wanamuamini au wanaamini katika uwezo wake? Nimeshangaa sana kuwa hata baadhi ya watu ambao wanakubali kabisa kiakili kuwa Lowassa hafai kuwa Rais lakini na wao wamejipanga mstari kusema “tutampa tu” ilimradi asionekane kumpinga! Wengine ambao kwa hakika unaweza kuamini walikuwa ni watu wa misimamo lakini na wao wamegeuka na kuwa “watu” wa Lowassa. Unajiuliza imewezekana vipi?
Ukiangalia hata watu wengine wanavyomshabikia ni kana kwamba wameamua kuegesha akili zao mahali wenyewe wakaamua kutembea kwa miguu!

Imenifanya nijiulize kama watu wanamuangalia Lowassa kama mganga wa kienyeji hivi? Unajua kabisa kuwa unachoamini hakiingii akilini lakini bado mtu anaenda kuvaa hirizi kubwa imeandikwa “ulipo tupo!”! Unajiuliza vipi watu waamini mtu ambaye hajawahi kuwa na imani ya upinzani wala kuonekana kuwa anaelewa unachosimamia leo yeye ndiyo awe “mabadiliko” na kuwa “mabadiliko” ni yeye na unakosa jibu zaidi ya “Hamtuambii chochote Lowassa nitampa kura yangu”; kama watu walioamua kupeleka kuku, mbuzi na hela zao kwa masangoma wakiamini kabisa kuwa majibu yatakuwa wanavyofikiria! Unajiuliza inakuwaje watu wanaruka ruka na kushangilia kabisa kwa imani hupati majibu zaidi ya “nyie mko nje ya nchi, tuachienie mganga wetu!”

Mwisho wa siku unagundua kuwa imani za kishirikina ni imani zenye nguvu sana kwa wenye kuziamini. Mtu anaweza asile, anaweza kufanya mambo ambayo angekuwa na akili nyingine asingefanya! Mtu mzima kavaa suti kumbe begani kuna hirizi kama simu ya iphone6 inaning’inia! Binti mzuri kabisa na kapendeza kabisa na amesoma na anajiita msomi (anafanya Masters yake mwenyewe tena ya Fizikia) lakini kiunoni kwenye makutano ya shanga kuna pande la hirizi limezunguka na chale zilizofichika!

Ubaya wa imani hizi ni kuwa hazimruhusu mtu kutumia akili yake kufikiri kwa sababu akiamua kufikiri anaweza asiendelee kuamini. Kwa mfano, kama mganga wa kienyeji anauwezo wa kumfanya mtu awe tajiri kwanini yeye mwenyewe maskini? Mtu mwenye imani hizi haruhusu maswali katika kichwa chake na mtu yeyote atakayejaribu kumfanya ajiulize maswali au kumuonesha upotofu wa hiyo imani ataonekana mara moja ni adui yake nambari moja na hachelewi kumtukana, kumfukuza au kumsemelea kwa huyo mganga! Huu ndio ubaya wa imani za kishirikina na kinachosikitisha ni kuwa Tanzania tunatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kwa imani hizi (kwa mujibu wa Pew Research). Ati asilimia 93 ya Watanzania wanaamini katika uchawi! (hizi 'nyomi hizi!)

Uzuri ni kuwa imani hizi huwa zinaisha! Wakati mwingine kwa njia ya kawaida lakini wakati mwingine kwa kulazimishwa. Zinakwisha kwa sababu hatimaye watu wanafunguka na kuachana na imani hizi na kuona makosa ya njia zao (errors of their ways) na kuamua kurudi kwenye njia sahihi. Mashabiki wengi wa Lowassa hasa wale WanaCHADEMA walioingizwa mkenge huu wa kihistoria nab ado wanajitambua wataanza kuamka na kufunguka. Siku hizi chache zilizobakia tutawaona watu wale wale ambao walimshangilia Lowassa wakianza kumtupa mikono na kumuachia chama kilichokuwa compromised. Lowassa na kundi lake itabidi watumie mbinu nyingine za kujaribu kujijengea ujiko mwingine ili kutishia watu waweze kuamini katika uwezo wao.

Ndivyo ilivyo kwa waganga wote; ili upate wateja ni lazima uje na mbinu za kutishia zaidi au kufanya mambo ambayo watu itabidi waamini kuwa ndiyvyo ilivyo. Wapo watakaoamini na wapo amba wataendelea kuhoji na kukataa hata kama kwa kufanya hivyo watakuwa wamejipotezea marafiki; hasa marafiki ambao wameamua kuamini katika geresha hii ya kihistoria.

Hata hivyo, kwa vile hawa ni ndugu zetu hatutawateta au kuwasema vibaya; tunajua kuwa Oktoba 25 wakati Lowassa na agenda yake ya kuutaka Urais (ndiyo ajenda pekee aliyonayo) itakapokataliwa na WAtanzania ndugu zetu watarudi na kutambua walivyopotea – wengine watasema “walipotoshwa” na kuona kile ambacho wengine tumekiona mapema na kwa miaka sasa – Lowassa siyo tu hafai lakini ni miongoni mwa viongozi wabovu kabisa kupata kutokea katika nchi yetu.

Ni kama mganga wa kienyeji fulani hivi ambaye watu wamemuamini sana lakini mwisho wa siku wakatambua tu. Uganga ni dili tu; haihusiani kabisa na kutaka kutibu maisha ya watu.

MMM
we mburura kweli aise
 
Mganga wa kienyeji anaweza kukuambia lolote nawewe ukaamini! Utaanzia wapikumuuliza kitu?
Una wivu wa kike. Kaa na ccm yako. Tuachie chadema yetu. Tushibde tusishinde haikuhusu. Na wewe umekuwa Mganga wa kienyeji au yahya husein mpaka ututabirie kwamba Lowasa hawezi kubadilika? Wewe ni nani mpaka ujifanye unaweza kusoma mioyo ya watu? Wewe ulikuwa unamfaidi Dr Slaa akiwa chadema sasa ameondoka huna pa kupatia tena mkate wako wa kila siku. Fanya kazi acha kuishi kwa kutegemea siasa. Kaa huko ccm wala hatukuhitaji huku upinzani. Kulialia tu. Au ile bil 150 Dr slaa kakuunganishia?
 
ni kweli kabisa mkuu BEHOLD,huyu MMM sana ni bonge la Great Sinker.
Inawezekana pia wakina Bulembo,Nape na Lusinde huyu ndio mshauri wao mkuu wa mikakati.Iweje mtu mzima utumie maneno ya hovyo kama swali la ugomvi halafu uwe na nia njema?Kwa nini leo na ni Lowasa pekee?

Hahahhaah From Great Thinker to Great Stinker!!!!! Stinky mouth:A S wink:
 
Yaaap mzeee umenena lowasa namfanisha na Mzee was loliondo Mzee masapila kwa mda mfupi watu walimwamini watu walimiminika wagojwa kitu kikombe cha babu kikapta umaharufu watu wakatoa wagojwa mahospital babu wA watu Leo anandinga kibao katajirika watu wakapoteza maisha ndugu wanajuta kuwatoa mma zao hospital bila kufikiria hasara watakayo ipata ile nyota ya Mzee yule iko kwa lowasa mnamjua vizuri eti lowasa msafi anafaa kuwa raising eti mabadiriko yeye alikuwa huko kwa nini asifanye mabadiko yeye na rafiki ake

heheheh umaarufu ameupata kipindi sahihi kabisa maana 25 october ni keshokutwa tu
 
Kwa nini awadanganye? Muda muafaka kila kitu kitawekwa kweupe. good evening!

Ndo uganga wa kienyeji unaoongelewa huo, mtu akihoji anaambiwa majibu kama 'subili muda muafaka kila kitu kitawekwa kweupe'. Ni ninyi tu ndo mtakubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia, wenye mantiki ya kuhoji hatulikubali hilo.
 
mganga.jpg

KWANI LOWASSA KAWA MGANGA WA KIENYEJI?
Na. M. M. Mwanakijiji

Jamii nyingi za Kiafrika (na inawezekana sehemu nyingine duniani) zina hofu kubwa ya watu ambao wanaaminiwa kuwa wana uwezo fulani hivi ama wa kudhuru watu au kuponya watu. Watu hawa wamepewa majina mbalimbali kutegemeana na kabila au mila na desturi za mahali; wanajulikana kwa majina mengi lakini kwa ujumla wao tunawatambua kama “waganga wa kienyeji”.

Waganga hawa wanatofautishwa vile vile; wapo wale ambao kazi yao kubwa ni kutibu kwa kutumia miti shamba na hawa hujulikana kama waganga wa tiba za “asili” na hawa hutumia zaidi madawa yatokanayo na miti na mimea (na hata wanyama) kujaribu kutibu wagonjwa wao. Kundi jingine ni la wale ambao hutumia siyo tu madawa mbalimbali bali pia hutumia “kunuia”; yaani wanaaminiwa wana uwezo wa kutoa maneno (sala, dua, maapizo n.k) ambayo yanachangia katika kuleta tiba kwa mtu au kumuondolea mtu matatizo yake. Hawa hujulikana zaidi kama waaguzi (seers); na katika kundi hili wapo wasoma nyota, viganja, alama za sayari, wenye kutumia vitabu vya kidini n.k
Katika hilo hilo kundi la pili wapo ambao pia huaminiwa kuwa siyo tu wana uwezo wa kutibu au kumuondolea mtu matatizo yake bali pia wanaweza (wakiamua kunuia) kumdhuru mtu na kumfanya mtu limfikie jambo baya. Kundi hili ni kundi la waganga wanaoogopwa sana kwani hawa ndio hujulikana katika lugha za wenzetu kuwa wanafanya “black magic” yaani wana uwezo wa kudhuru watu na wanapofanya hivyo basi tunawaita ni “wachawi”. Wachawi hasa ni kundi la mbali zaidi ambalo wao hawajishughulishi na tiba bali katika kudhuru watu (wawe na sababu au bila sababu). Wapo waganga ambao wanaanzia upande mmoja na mwisho wanaweza kujikuta upande mwingine kabisa.

Hata hivyo, watu wengi katika bara letu, nchini mwetu na hata sehemu nyingine duniani huwaendea zaidi wale waganga wenye kuonekana wana uwezo wa kutibu hasa wenye kuchanganya miti ya asili (mitishamba) na namna fulani ya kunuia. Waganga hawa wengine wakitumia mbinu za kimazingaombwe (viinimacho) wanaweza kabisa kuwaaminisha watu kuwa vitu fulani vipi au havipo na wanaweza kufanya vitokee au visitokee na hivyo kujijengea imani hasa. Na watu wa namna hii huogopwa sana hasa kwa vile inaaminika wana “uwezo fulani”. Karibu jamii zote duniani zimewahi kuwa na watu wa namna hii.

Katika nchi yetu hata hivyo, imani hii kwa waganga wa kienyeji inatokana na imani za kishirikina zaidi (superstitious beliefs). Tunaogopa vitu fulani fulani, tunaamini vitu fulani fulani, na wakati mwingine hata kuwafuata watu kwa sababu ya imani hizi hizi. Mtu akitaka kumtishia mtu mwingine basi anamwekea “hirizi” kwenye mlango wa ofisi yake na mtu huyo akiikuta anaweza kutahamaki kuwa wanataka kumroga (na anaweza kuwa ni msomi na PhD juu yake) lakini mara moja ataahirisha kwenda kazini siku hiyo na yeye aende “Bagamoyo” kwenda kutafuta Kinga. Na kama “Bagamoyo” alikokwenda hakuji na majibu ya kutosha basi anaweza kuamua kwenda “Sumbawanga”. “Sumbawanga” hiyo ikikataa basi anaweza akaamini waganga wakali zaidi wako “Tanga” na hivyo atatafuta safari ya kwenda Tanga! Maisha ya mtu huyo utaona mara moja yanazidi kuzama katika imani hizi kiasi kwamba hata dini kama alikuwa nayo inapotelea mbali au anachanganyia “mumo kwa mumo”.

Katika matatizo yote ya wananchi wenye kunufaika ni hawa waganga wa kienyeji hasa wale wenye majina ya kutisha zaidi na ambao sifa zao zimetangaa nchi nzima. Wapo – kwa mujibu wa vyanzo vingi – waganga ambao wanafanya “house calls”; yaani, hawa ni waganga ambao huweza kualikwa na kwenda kufanya huduma kwenye nyumba za watu hasa kama mtu mwenyewe hawezi kwenda kwa mganga huyo akaonekana. Wapo watu mashuhuri ambao hutembelewa na wengine wanao waganga wao ambao wako kwenye malipo yao!

Ukiangalia sana siasa zetu za mwaka huu ni lazima mtu ujiulize kama watu wanaomshabikia Lowassa wanafanya hivyo kwa vile wanamuamini au wanaamini katika uwezo wake? Nimeshangaa sana kuwa hata baadhi ya watu ambao wanakubali kabisa kiakili kuwa Lowassa hafai kuwa Rais lakini na wao wamejipanga mstari kusema “tutampa tu” ilimradi asionekane kumpinga! Wengine ambao kwa hakika unaweza kuamini walikuwa ni watu wa misimamo lakini na wao wamegeuka na kuwa “watu” wa Lowassa. Unajiuliza imewezekana vipi?
Ukiangalia hata watu wengine wanavyomshabikia ni kana kwamba wameamua kuegesha akili zao mahali wenyewe wakaamua kutembea kwa miguu!

Imenifanya nijiulize kama watu wanamuangalia Lowassa kama mganga wa kienyeji hivi? Unajua kabisa kuwa unachoamini hakiingii akilini lakini bado mtu anaenda kuvaa hirizi kubwa imeandikwa “ulipo tupo!”! Unajiuliza vipi watu waamini mtu ambaye hajawahi kuwa na imani ya upinzani wala kuonekana kuwa anaelewa unachosimamia leo yeye ndiyo awe “mabadiliko” na kuwa “mabadiliko” ni yeye na unakosa jibu zaidi ya “Hamtuambii chochote Lowassa nitampa kura yangu”; kama watu walioamua kupeleka kuku, mbuzi na hela zao kwa masangoma wakiamini kabisa kuwa majibu yatakuwa wanavyofikiria! Unajiuliza inakuwaje watu wanaruka ruka na kushangilia kabisa kwa imani hupati majibu zaidi ya “nyie mko nje ya nchi, tuachienie mganga wetu!”

Mwisho wa siku unagundua kuwa imani za kishirikina ni imani zenye nguvu sana kwa wenye kuziamini. Mtu anaweza asile, anaweza kufanya mambo ambayo angekuwa na akili nyingine asingefanya! Mtu mzima kavaa suti kumbe begani kuna hirizi kama simu ya iphone6 inaning’inia! Binti mzuri kabisa na kapendeza kabisa na amesoma na anajiita msomi (anafanya Masters yake mwenyewe tena ya Fizikia) lakini kiunoni kwenye makutano ya shanga kuna pande la hirizi limezunguka na chale zilizofichika!

Ubaya wa imani hizi ni kuwa hazimruhusu mtu kutumia akili yake kufikiri kwa sababu akiamua kufikiri anaweza asiendelee kuamini. Kwa mfano, kama mganga wa kienyeji anauwezo wa kumfanya mtu awe tajiri kwanini yeye mwenyewe maskini? Mtu mwenye imani hizi haruhusu maswali katika kichwa chake na mtu yeyote atakayejaribu kumfanya ajiulize maswali au kumuonesha upotofu wa hiyo imani ataonekana mara moja ni adui yake nambari moja na hachelewi kumtukana, kumfukuza au kumsemelea kwa huyo mganga! Huu ndio ubaya wa imani za kishirikina na kinachosikitisha ni kuwa Tanzania tunatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kwa imani hizi (kwa mujibu wa Pew Research). Ati asilimia 93 ya Watanzania wanaamini katika uchawi! (hizi 'nyomi hizi!)

Uzuri ni kuwa imani hizi huwa zinaisha! Wakati mwingine kwa njia ya kawaida lakini wakati mwingine kwa kulazimishwa. Zinakwisha kwa sababu hatimaye watu wanafunguka na kuachana na imani hizi na kuona makosa ya njia zao (errors of their ways) na kuamua kurudi kwenye njia sahihi. Mashabiki wengi wa Lowassa hasa wale WanaCHADEMA walioingizwa mkenge huu wa kihistoria nab ado wanajitambua wataanza kuamka na kufunguka. Siku hizi chache zilizobakia tutawaona watu wale wale ambao walimshangilia Lowassa wakianza kumtupa mikono na kumuachia chama kilichokuwa compromised. Lowassa na kundi lake itabidi watumie mbinu nyingine za kujaribu kujijengea ujiko mwingine ili kutishia watu waweze kuamini katika uwezo wao.

Ndivyo ilivyo kwa waganga wote; ili upate wateja ni lazima uje na mbinu za kutishia zaidi au kufanya mambo ambayo watu itabidi waamini kuwa ndiyvyo ilivyo. Wapo watakaoamini na wapo amba wataendelea kuhoji na kukataa hata kama kwa kufanya hivyo watakuwa wamejipotezea marafiki; hasa marafiki ambao wameamua kuamini katika geresha hii ya kihistoria.

Hata hivyo, kwa vile hawa ni ndugu zetu hatutawateta au kuwasema vibaya; tunajua kuwa Oktoba 25 wakati Lowassa na agenda yake ya kuutaka Urais (ndiyo ajenda pekee aliyonayo) itakapokataliwa na WAtanzania ndugu zetu watarudi na kutambua walivyopotea – wengine watasema “walipotoshwa” na kuona kile ambacho wengine tumekiona mapema na kwa miaka sasa – Lowassa siyo tu hafai lakini ni miongoni mwa viongozi wabovu kabisa kupata kutokea katika nchi yetu.

Ni kama mganga wa kienyeji fulani hivi ambaye watu wamemuamini sana lakini mwisho wa siku wakatambua tu. Uganga ni dili tu; haihusiani kabisa na kutaka kutibu maisha ya watu.

MMM

Hii tafakuri yako inapaswa iingie kwenye akili ya kila mpiga kura (sio mpiga matusi ambae inawezekana hata kujiandikisha hajajiandikisha lakini ndio wa kwanza kusema Edo ndie rais wake).

Kwa kweli ifike mahali ukweli uwekwe hadharani. Mzee Mwanakijiji umejitahaidi kufanya hivyo kwa lugha nyepesi mno. Hatukatai kwamba kila mtanzania anayo haki ya kuchaguliwa kuwa rais wa JMT iwapo atakidhi vigezo vya katiba. Lakini kwa kweli EL hachaguliki kwa kigezo cha namna yeyote.

Inahitaji uwe hujitambui, umelogwa, umekataa tamaa ya maisha kupindukia na kujiaminisha kwamba Mwenyezi Mungu hayupo hivyo mtu huyo ameyaweka matumaini ya kuishi mikononi kwa EL !! Mbaya zaidi miongoni mwa watu hao ni watu tunaowaita wasomi!!!!
 
Rostam Aziz,Nazir Karamag,Philemon Ndessamburo,Freeman Mbowe,Edwin Mtei,Edward Lowassa na Reginard Mengi WANAKUDANGANYA eti CCM imekufanya maskini mbona wao WAMETAJIRIKA chini ya utawala wa CCM, mbona haikuwafanya wao MASKINI????!Huo mfumo wa Mbowe na Mtei ndo waamuzi wa kila kitu TUKIWAUZIA NCHI TUMEKWISHA.
Swadakta
 
Unakaa kusoma kitu chenye kujenga. Mtu atapotezaje kusoma porojo kama hii. Hizo nchi za wenzetu watu hawakai kupoteza muda kusoma porojo wakati kuna vitu vya muhimu anataka kuvifanya. Pia si jambo la kujisifia kukaa chini kupoteza muda kisa unaandika porojo ambayo unajua matokeo yake watu hawatasoma na wataangalia na kuishia kukukandia.
Watu Mwanakikijiji hawakuelewi kwa porojo zako wameshaamua cha kufanya. Waulizie wenzio akina Polepole wamekalia Channel Ten kutoa porojo, na watu wakiona ni yeye wanabadili channel kuendelea na vipindi vingine yeye akidhani anasikilizwa kumbe yupo peke yake. Waulize wale waliokuwa wanapiga kampaini za ohoo mgonjwa sasa wanaona anazidi kudunda tu, ohooo Richmond, wanasahau wamebeba Escrow na twiga uko Ngorongoro zinadi kupanda ndege uku mafuriko ya Lowasa yakizidi kuwa Tsunami. Uliza Tanga kunani? We kalia ughaibuni kupiga porojo tu
Siyo jambo la kujisifia; mnafikiri nchi za wenzenu zimejengwa na watu wenye kusoma mstari mmoja? Labda ndio maana mgombea fulani hazungumzi sana kwa sababu akizungumza sana anaweza akawapoteza watu bure...
 
Na kuna watu na akili zao wanaamini akipita Lowassa Tanzania itakua ile ya sayari nyingine.

Wapo wanaoamini akipita Lowassa utajiri nje nje, huduma za kijamii bure, ufanye usifanye kazi wewe utakua na maisha mazuri tu.

Wengi wanategemea Tanzania ya miujiza toka kwa Lowassa,eti gesi ipo, bandari ipo, vivutio vya utalii vipo kwa hiyo haina haja ya kuhangaika na kazi.

Watu wanasubiri Tanzania ya Lowasa itawafanyia nini, sio wao wataifanyia nini Tanzania.

Lowassa anawaaminisha watu vitu ambavyo yeye mwenyewe haamini ilimradi awe Rais.

Sioni Lowassa akiwa Raisi utawala wake ukikosolewa, hizi kauli mbona ccm nao wameiba sana zitaendelea Hadi kwenye utawala wake,

Yaani kila ovu la utawala wa Lowassa litatetewa kwa ovu la utawala wa ccm, hapo ndipo wenye uchu na nchi hii watavyoitafuna Bila shida.

Kwa nini unawasemea watu wanaomtaka Lowassa . . ? Wewe upo ndani ya vichwa vya watanzania wengi hivyoo..?
Na bado upo ccm pia. . . ?! Nadhani Mwanakijiji anakuzungumzia wewe hapa . . " Mganga wa Kienyeji " . .
 
Mwanakijiji ni msukule wa dokta ndio maana hizi makala za kichokozi zimezidi toka dokta alipoenda kupunguza stress Marekani
 
mganga.jpg

KWANI LOWASSA KAWA MGANGA WA KIENYEJI?
Na. M. M. Mwanakijiji

Jamii nyingi za Kiafrika (na inawezekana sehemu nyingine duniani) zina hofu kubwa ya watu ambao wanaaminiwa kuwa wana uwezo fulani hivi ama wa kudhuru watu au kuponya watu. Watu hawa wamepewa majina mbalimbali kutegemeana na kabila au mila na desturi za mahali; wanajulikana kwa majina mengi lakini kwa ujumla wao tunawatambua kama “waganga wa kienyeji”.

Waganga hawa wanatofautishwa vile vile; wapo wale ambao kazi yao kubwa ni kutibu kwa kutumia miti shamba na hawa hujulikana kama waganga wa tiba za “asili” na hawa hutumia zaidi madawa yatokanayo na miti na mimea (na hata wanyama) kujaribu kutibu wagonjwa wao. Kundi jingine ni la wale ambao hutumia siyo tu madawa mbalimbali bali pia hutumia “kunuia”; yaani wanaaminiwa wana uwezo wa kutoa maneno (sala, dua, maapizo n.k) ambayo yanachangia katika kuleta tiba kwa mtu au kumuondolea mtu matatizo yake. Hawa hujulikana zaidi kama waaguzi (seers); na katika kundi hili wapo wasoma nyota, viganja, alama za sayari, wenye kutumia vitabu vya kidini n.k
Katika hilo hilo kundi la pili wapo ambao pia huaminiwa kuwa siyo tu wana uwezo wa kutibu au kumuondolea mtu matatizo yake bali pia wanaweza (wakiamua kunuia) kumdhuru mtu na kumfanya mtu limfikie jambo baya. Kundi hili ni kundi la waganga wanaoogopwa sana kwani hawa ndio hujulikana katika lugha za wenzetu kuwa wanafanya “black magic” yaani wana uwezo wa kudhuru watu na wanapofanya hivyo basi tunawaita ni “wachawi”. Wachawi hasa ni kundi la mbali zaidi ambalo wao hawajishughulishi na tiba bali katika kudhuru watu (wawe na sababu au bila sababu). Wapo waganga ambao wanaanzia upande mmoja na mwisho wanaweza kujikuta upande mwingine kabisa.

Hata hivyo, watu wengi katika bara letu, nchini mwetu na hata sehemu nyingine duniani huwaendea zaidi wale waganga wenye kuonekana wana uwezo wa kutibu hasa wenye kuchanganya miti ya asili (mitishamba) na namna fulani ya kunuia. Waganga hawa wengine wakitumia mbinu za kimazingaombwe (viinimacho) wanaweza kabisa kuwaaminisha watu kuwa vitu fulani vipi au havipo na wanaweza kufanya vitokee au visitokee na hivyo kujijengea imani hasa. Na watu wa namna hii huogopwa sana hasa kwa vile inaaminika wana “uwezo fulani”. Karibu jamii zote duniani zimewahi kuwa na watu wa namna hii.

Katika nchi yetu hata hivyo, imani hii kwa waganga wa kienyeji inatokana na imani za kishirikina zaidi (superstitious beliefs). Tunaogopa vitu fulani fulani, tunaamini vitu fulani fulani, na wakati mwingine hata kuwafuata watu kwa sababu ya imani hizi hizi. Mtu akitaka kumtishia mtu mwingine basi anamwekea “hirizi” kwenye mlango wa ofisi yake na mtu huyo akiikuta anaweza kutahamaki kuwa wanataka kumroga (na anaweza kuwa ni msomi na PhD juu yake) lakini mara moja ataahirisha kwenda kazini siku hiyo na yeye aende “Bagamoyo” kwenda kutafuta Kinga. Na kama “Bagamoyo” alikokwenda hakuji na majibu ya kutosha basi anaweza kuamua kwenda “Sumbawanga”. “Sumbawanga” hiyo ikikataa basi anaweza akaamini waganga wakali zaidi wako “Tanga” na hivyo atatafuta safari ya kwenda Tanga! Maisha ya mtu huyo utaona mara moja yanazidi kuzama katika imani hizi kiasi kwamba hata dini kama alikuwa nayo inapotelea mbali au anachanganyia “mumo kwa mumo”.

Katika matatizo yote ya wananchi wenye kunufaika ni hawa waganga wa kienyeji hasa wale wenye majina ya kutisha zaidi na ambao sifa zao zimetangaa nchi nzima. Wapo – kwa mujibu wa vyanzo vingi – waganga ambao wanafanya “house calls”; yaani, hawa ni waganga ambao huweza kualikwa na kwenda kufanya huduma kwenye nyumba za watu hasa kama mtu mwenyewe hawezi kwenda kwa mganga huyo akaonekana. Wapo watu mashuhuri ambao hutembelewa na wengine wanao waganga wao ambao wako kwenye malipo yao!

Ukiangalia sana siasa zetu za mwaka huu ni lazima mtu ujiulize kama watu wanaomshabikia Lowassa wanafanya hivyo kwa vile wanamuamini au wanaamini katika uwezo wake? Nimeshangaa sana kuwa hata baadhi ya watu ambao wanakubali kabisa kiakili kuwa Lowassa hafai kuwa Rais lakini na wao wamejipanga mstari kusema “tutampa tu” ilimradi asionekane kumpinga! Wengine ambao kwa hakika unaweza kuamini walikuwa ni watu wa misimamo lakini na wao wamegeuka na kuwa “watu” wa Lowassa. Unajiuliza imewezekana vipi?
Ukiangalia hata watu wengine wanavyomshabikia ni kana kwamba wameamua kuegesha akili zao mahali wenyewe wakaamua kutembea kwa miguu!

Imenifanya nijiulize kama watu wanamuangalia Lowassa kama mganga wa kienyeji hivi? Unajua kabisa kuwa unachoamini hakiingii akilini lakini bado mtu anaenda kuvaa hirizi kubwa imeandikwa “ulipo tupo!”! Unajiuliza vipi watu waamini mtu ambaye hajawahi kuwa na imani ya upinzani wala kuonekana kuwa anaelewa unachosimamia leo yeye ndiyo awe “mabadiliko” na kuwa “mabadiliko” ni yeye na unakosa jibu zaidi ya “Hamtuambii chochote Lowassa nitampa kura yangu”; kama watu walioamua kupeleka kuku, mbuzi na hela zao kwa masangoma wakiamini kabisa kuwa majibu yatakuwa wanavyofikiria! Unajiuliza inakuwaje watu wanaruka ruka na kushangilia kabisa kwa imani hupati majibu zaidi ya “nyie mko nje ya nchi, tuachienie mganga wetu!”

Mwisho wa siku unagundua kuwa imani za kishirikina ni imani zenye nguvu sana kwa wenye kuziamini. Mtu anaweza asile, anaweza kufanya mambo ambayo angekuwa na akili nyingine asingefanya! Mtu mzima kavaa suti kumbe begani kuna hirizi kama simu ya iphone6 inaning’inia! Binti mzuri kabisa na kapendeza kabisa na amesoma na anajiita msomi (anafanya Masters yake mwenyewe tena ya Fizikia) lakini kiunoni kwenye makutano ya shanga kuna pande la hirizi limezunguka na chale zilizofichika!

Ubaya wa imani hizi ni kuwa hazimruhusu mtu kutumia akili yake kufikiri kwa sababu akiamua kufikiri anaweza asiendelee kuamini. Kwa mfano, kama mganga wa kienyeji anauwezo wa kumfanya mtu awe tajiri kwanini yeye mwenyewe maskini? Mtu mwenye imani hizi haruhusu maswali katika kichwa chake na mtu yeyote atakayejaribu kumfanya ajiulize maswali au kumuonesha upotofu wa hiyo imani ataonekana mara moja ni adui yake nambari moja na hachelewi kumtukana, kumfukuza au kumsemelea kwa huyo mganga! Huu ndio ubaya wa imani za kishirikina na kinachosikitisha ni kuwa Tanzania tunatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kwa imani hizi (kwa mujibu wa Pew Research). Ati asilimia 93 ya Watanzania wanaamini katika uchawi! (hizi 'nyomi hizi!)

Uzuri ni kuwa imani hizi huwa zinaisha! Wakati mwingine kwa njia ya kawaida lakini wakati mwingine kwa kulazimishwa. Zinakwisha kwa sababu hatimaye watu wanafunguka na kuachana na imani hizi na kuona makosa ya njia zao (errors of their ways) na kuamua kurudi kwenye njia sahihi. Mashabiki wengi wa Lowassa hasa wale WanaCHADEMA walioingizwa mkenge huu wa kihistoria nab ado wanajitambua wataanza kuamka na kufunguka. Siku hizi chache zilizobakia tutawaona watu wale wale ambao walimshangilia Lowassa wakianza kumtupa mikono na kumuachia chama kilichokuwa compromised. Lowassa na kundi lake itabidi watumie mbinu nyingine za kujaribu kujijengea ujiko mwingine ili kutishia watu waweze kuamini katika uwezo wao.

Ndivyo ilivyo kwa waganga wote; ili upate wateja ni lazima uje na mbinu za kutishia zaidi au kufanya mambo ambayo watu itabidi waamini kuwa ndiyvyo ilivyo. Wapo watakaoamini na wapo amba wataendelea kuhoji na kukataa hata kama kwa kufanya hivyo watakuwa wamejipotezea marafiki; hasa marafiki ambao wameamua kuamini katika geresha hii ya kihistoria.

Hata hivyo, kwa vile hawa ni ndugu zetu hatutawateta au kuwasema vibaya; tunajua kuwa Oktoba 25 wakati Lowassa na agenda yake ya kuutaka Urais (ndiyo ajenda pekee aliyonayo) itakapokataliwa na WAtanzania ndugu zetu watarudi na kutambua walivyopotea – wengine watasema “walipotoshwa” na kuona kile ambacho wengine tumekiona mapema na kwa miaka sasa – Lowassa siyo tu hafai lakini ni miongoni mwa viongozi wabovu kabisa kupata kutokea katika nchi yetu.

Ni kama mganga wa kienyeji fulani hivi ambaye watu wamemuamini sana lakini mwisho wa siku wakatambua tu. Uganga ni dili tu; haihusiani kabisa na kutaka kutibu maisha ya watu.

MMM

Kum we mzee nawe ni zuzu? looh!
 
Mkuu Pasco, kwa manufaa ya nifah na wengine naomba uilete tena ile comment ya Mzee Mwanakijiji aliyosema yeye ni CCM, na aliomba kadi (ila wakamnyima). Nadhani itasaidia sana unapokuwa unasoma posts zake utumie nguvu na muda kiasi gani.

Good morning Tanzania.

Ikiwezekana aweke kama signature.

Na a-declare the conflict of interest.
 
Back
Top Bottom