Swali la Ugomvi: Kwani Lowassa Kawa Mganga wa Kienyeji?

Jukumu la kuthibitisha bila shaka ni la mahakama. At least kama aliona haki haikutendeka angesema ataishawishi mahakama ili kesi isikilizwe upya. Kutoa watuhumiwa wa jinai gerezani ndo mamlaka yaliyopitiliza ya rais tunayoyalalamikia kila siku. Siku nyingine akimtoa Rostam gerezani (kama atafungwa) mtawezaje kulalamika?

Ngoja nikusaidie, Lowassa aliombwa na wananchi akipewa nchi amrudishe babu Seya, sasa wewe huoni hapo kuna tatizo? Alichokijibu Lowassa ni kwamba, atahitisha mafaili upya na kuona kama kuna haki ilikiukwa anarejeshewa hiyo haki. Kuna tatizo hapo.
 
Wewe unafikiri ktk nchi za kiafrika na duniani kwa ujumla Lowasa ndio wa kwanza kupendwa namna hii? Jambo la kawaida kabisa imani zako za ushirikina kaa nazo mwenyewe usitupoteze cc!
 
Matunda ya CCM.
Hoja yako ni nini?

Nisaidie kufafanua zaidi!

Kwa hiyo uwepo wa shetani hapa duniani lawama lazima azibebe Mungu pamoja na kwamba kuna watu wengi ambao hawataki kuungana na shetani katika matendo yake?

Hoja yangu ni kuwa, kuna wananchi wengi ambao siyo wapumbavu ndani ya nchi ambayo inaongozwa na CCM. Huwezi kuilaumu CCM kwa sababu ya upumbavu wa baadhi ya wananchi kama ambavyo huwezi kumlaumu Mungu kwa uwepo wa shetani duniani.
 
“Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira”. Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha “wateule” na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, “kulikoni?”. Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya “malofa” wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: “Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?”Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza “nyomi” katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni “vijisenti”, au “fedha ya mboga”, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa “Wapige mbizi” na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa “Ni heri wale nyasi”…Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni “wapumbavu,amlofa na mbumbumbu”. Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.“ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
 
Hoja yako ni nini?

Nisaidie kufafanua zaidi!

Kwa hiyo uwepo wa shetani hapa duniani lawama lazima azibebe Mungu pamoja na kwamba kuna watu wengi ambao hawataki kuungana na shetani katika matendo yake?

Hoja yangu ni kuwa, kuna wananchi wengi ambao siyo wapumbavu ndani ya nchi ambayo inaongozwa na CCM. Huwezi kuilaumu CCM kwa sababu ya upumbavu wa baadhi ya wananchi kama ambavyo huwezi kumlaumu Mungu kwa uwepo wa shetani duniani.

Kwani Shetani alikuwa wapi mwanzoni na ilikuwaje akaja duniani?.
Kuna maombi yaliyopelekwa kwa Mungu ili amshushe shetani? au yeye aliamua tu kumleta huku duniani!.
 
  1. Ni makala nzuri ambayo imejaribu kuwadhalilisha waTanzania wanaoamini katika tiba asili. Maana wapo hata viongozi ambao wamewahi na wanaenda kupata tiba na "kunywa vikombe" kwa waganga hawa. Wakati sayansi ya kimagharibi inakataza dawa zinazotokana na miti shamba (dawa za waganga wa kienyeji) ili kuimarisha soko la dawa zao (rejea historia ya darasa la tano la zamani) wewe unapinga asili yako.
  2. Kutofautiana katika kuamini wagombea haimaanishi wale walio upande wa pili wanaamini mganga wa kienyeji. Ni jambo jema kuvumiliana na kuelimishana bila kutumia lugha ya kejeli na dharau. Kwa nini tusijikite kujadili sera na ilani za vyama hivi ambazo ndizo vyama vinaziuza?
  3. Si vema kudharau taaluma ya watu wengine. Wapo waganga wa kienyeji ambao serikali imewasajili na wala si matapeli.
  4. Baadhi ya kauli unazotoa zinaweza kumhusisha hata Mheshimiwa Rais. Rais anaemteua "kiongozi mbovu ambae hajawahi kutokea Tanzania" kuwa Waziri Mkuu tutamuonaje sisi wananchi. Tunaomba sana usituchonganishe sisi wananchi na Rais wetu ambae demokrasia ya kutoa na kupata taarifa ameikuza mno. Au tuwaonaje marais wastaafu waliomteua katika nafasi za uwaziri na unaibu waziri. Nikimrejea Mwanasiasa mmoja maarufu, tujue kuweka akiba ya maneno.
  5. Kuna njia nyingi za kuonesha mapungufu ya mgombea bila kumvunjia staha au kutumia maneno makali dhidi yake na wanaomshabikia. Umepata wapi ushujaa wa kuwaambia wenzio wameweka akili pembeni halafu wanatembea?
 
Na kuna watu na akili zao wanaamini akipita Lowassa Tanzania itakua ile ya sayari nyingine.

Wapo wanaoamini akipita Lowassa utajiri nje nje, huduma za kijamii bure, ufanye usifanye kazi wewe utakua na maisha mazuri tu.

Wengi wanategemea Tanzania ya miujiza toka kwa Lowassa,eti gesi ipo, bandari ipo, vivutio vya utalii vipo kwa hiyo haina haja ya kuhangaika na kazi.

Watu wanasubiri Tanzania ya Lowasa itawafanyia nini, sio wao wataifanyia nini Tanzania.

Lowassa anawaaminisha watu vitu ambavyo yeye mwenyewe haamini ilimradi awe Rais.

Sioni Lowassa akiwa Raisi utawala wake ukikosolewa, hizi kauli mbona ccm nao wameiba sana zitaendelea Hadi kwenye utawala wake,

Yaani kila ovu la utawala wa Lowassa litatetewa kwa ovu la utawala wa ccm, hapo ndipo wenye uchu na nchi hii watavyoitafuna Bila shida.

Nimejitahidi sana kujizuia lakini wewe una ukelbu mkubwa sana!!!
Una akili za ajabu sana wewe. Aliekuambia kwamba Lowasa anatuambia hakutakuwa na haja ya kufanya kazi tutaishije? Unadhani wana UKAWA na mandondocha kama mafisiemu yanayoiba vya wavujajasho? Tutafanya kazi ila mazingira ya kazi yatakuwa mazuri zaidi kwa sababu tutakuwa na kiongozi anaetujali na kututengenezea mazingira mazuri ya kujipatia chochote.

fisiemu ni chama ambacho nakifananisha na mzazi wa hovyo. Anazaa watoto halafu hajui awafanye nini. Kidogo kilichopo anakula peke yake na kuwafukuzia wanae barabarani wakatafute "nini wataifanyia Tanzania". JFK aliesema "usijiulize Amerika itakufanyia nini bali nini utaifanyia Amerika?" aliweza kuuliza hayo maana misingi ya "nini cha kuifanyia Amerika" ilikuwa imewekwa vizuri. Walikuwa na barabara, maji safi, working governmental systems, no kipindupindu!, umeme wa uhakika, afya bora, elimu, n.k.

Leo kijana anafungua saluni ya nywele kwa mkopo ili apate chochote. Umeme wa manati, unategemea atajikwamuaje? Akakope tena apate hela ya generator? Akakope pia na hela ya mafuta ya kuweka kwenye hilo generator?

Ninakuomba usirudie tena kuongea kama taahira lisilokuwa na macho wala akili ya kuona jinsi mafisiemu yanavyotumaliza.

kelbu haram
 
Mzee Mwanakijiji, msome Abel Ndundulu kwa makini, nina hakika majibu yote kayatoa katika hiki kipande chake kuhusu jamii unayoiita inaamini katika waganga wa kienyeji.

  • Ni jamii iliyochoka na kuchakaa;
  • ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani,
  • Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji;
  • ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira”.
wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,

Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala;
Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia:

Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha “wateule” na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao.

Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, “kulikoni?”.

Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya “malofa” wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: “Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?”



  • Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,
  • vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza “nyomi” katika mikutano,
  • wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,
  • wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia...Dah!
  • wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.
Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni “vijisenti”, au “fedha ya mboga”, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku.

Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa “Wapige mbizi” na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa “Ni heri wale nyasi”…

Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni “wapumbavu, malofa na mbumbumbu”.

Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,

Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.

“ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!


 


Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,

Unataka CCM ipumzishwe na taasisi ya Lowassa na genge lake? Hivi ulijifunzia wapi hii fani ya vichekesho?

Lowassa mabadiliko, Mabadiliko Lowassa. My left foot.

"ALUTA Continua, Victoria Ascerta".... "The Struggle Continues, Victory is Certain"; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!

Yes, struggle zilianza siku uliyozaliwa na utaziacha siku ya kufa!

Hakuna jipya katika hitimisho lako!
 
Back
Top Bottom