Swali kwenu wanandoa

Hakuna anayefundishwa kuishi na mke au mume kwa siku moja (kitchen party). Tabia ya mtu inatengenezwa na life experience.

Ndio maana unakuta wa mkoa fulani wako hivi na wa mkoa fulani wako vile...wanaiga matendo ya baba na mama zao...walimu wa dunia

mamie sijamaanisha kitchen party ama beg party. ninachouliza hapa ni wakati mdada/mkaka anajiandaa kuolewa/kuoa. je wazazi / walezi huwa wanafundisha ni jinsi gani wanatakiwa kuishi na wake / waume zao????
 
BADILI TABIA Simaanishi mafunzo ya siku moja kwenye kitchen party / begparty bali nazungumzia je kuna mafunzo ambayo mwanaume/mwanamke hupewa wakati anajiandaa kuoa / kuolewa? ukiachilia mbali hizo kitchen party na bag party. . .
 
Last edited by a moderator:
Kwa wakristo, mafundisho ya ndoa hutolewa kwa wote wawili.
Mafundisho huwa yanatolewa wote wawili wakiwa pamoja, taani mwamamme na mwanamke wanafundishwa pamoja.
 
99% ya ndoa zinazovunjika usababishwa na utovu wa nidhamu ndani ya ndoa.

ni kweli, watu wengi hasa vijana hawaziheshimu ndoa zao. na asilimia kubwa ya kuvunjika kwa ndoa nyingi chanzo ni usaliti. je nini kifanyike kuzinusuru ndoa hasa za vijana wa leo?
 
hakuna kufundishwa wala kufundishwa mambo mengine yanakuja otomatekale tu!
nani amewahi kufundishwa na mzazi wake kuwa kutia wanatia hivi,au mkeo akisema hiki mpige au mumeo akisema hiki lia!
mi nafikiri kila mtu anaishi ndoa yake kulingana na tabia yake binfsi
mambo yote yanayokuwa applied kwenye ndoa ni personal oriented ingekuwa tunafundishwa basi woooooooote tungekuwa na ndoa za aina moja!
lakini kutokana na ukweli kwamba ndoa ni maisha na sio rehasal ndo mana kila mtu ana ndoa ya pekee kulinganisha na mwingine!
wenzio waogeshana kila siku wewe shurti kuingia kitandani na suruali na bado mumeo au mkeo anafurahia ndoa yenu kwa hiyo its all aboout knowing u and ur better half!
 
Kwa wakristo, mafundisho ya ndoa hutolewa kwa wote wawili.
Mafundisho huwa yanatolewa wote wawili wakiwa pamoja, taani mwamamme na mwanamke wanafundishwa pamoja.

mkuu mbali na mafundisho ya dini wakati washakuwa wachumba. je wakati kijana anajiandaa kuanza mchakato wa kutafuta mwenza kabla hata hajajua atamuoa nani ndio hapo kwenye swali langu.
 
Idea yako au niseme swali lako halina tofauti na kuulizia umuhimu wa kitchen party....'n'gombe hanenepi siku ya mnada' (Kongosho 2012 quoting wahenga 1890)

Tabia ya mtu uanza kujijenga siku anapozaliwa na kuendelea...si akikaribia kuoa au kuolewa;

hata kama una watoto wengi unaweza ku tell huyu atakuwa mkorofi kwa mkewe...huyu atakuwa husband material kwa jinsi wanavyo behave....nina mpwa wangu kila mtu anampenda kwa kuwa japo ni wa kiume haoni shida kusema wote tupumzike yeye leo mpishi...sasa imagine what a husband akikuoa mtu kama huyo...tena anapenda na kuwaheshimu sana wanawake na wasichana.

mamie sijamaanisha kitchen party ama beg party. ninachouliza hapa ni wakati mdada/mkaka anajiandaa kuolewa/kuoa. je wazazi / walezi huwa wanafundisha ni jinsi gani wanatakiwa kuishi na wake / waume zao????
 
Mwanamke ndo anafundwa, mara 100 uishi na mwanaume mpumbavu kuliko mwanamke mpumbavu, Charminglady nyie ndo wajenzi wa familia, so ukiwa mwerevu utamwelimisha mumeo, God forbid mwanamke akiwa mpumbavu yaani sipatii picha.
 
mkuu mbali na mafundisho ya dini wakati washakuwa wachumba. je wakati kijana anajiandaa kuanza mchakato wa kutafuta mwenza kabla hata hajajua atamuoa nani ndio hapo kwenye swali langu.

Kwa hapo mimi sijaona mafunzo yoyote yakitolewa.
Nadhani ndio maana mafunzo hutolewa kanisani kabla tu ya kufunga ndoa.
Mafunzo hayo huwa ni comprehensive sana, na utakuta kwa baadhi ya madhehebu ya kikristo mafunzo hayo huwa marefu sana hata kufikia mwezi mzima !!
 
Mimi nimepitia hayo mafunzo ya kanisani...lakini to be honest sikumbuki hata moja...kwanza akili yangu yote ilikuwa kwenye harusi. Lol..

I am what I am si kwa sababu ya mafunzo fulani bali my learning through the whole life experience...

Mimi nakumbuka sana mafundisho ya kanisani.
Mojawapo ni kuhusu uhuru wa wanandoa baada ya ndoa.
Kuhusu uhuru wa wanandoa, ni kwamba baada ya ndoa uhuru wote waliokuwa nao unapotea kabisa.
Hapo unakuja uhuru wenge masharti ya mwenzako. Huwezi tena kutoka nyumbani weekend bila ruhusa ya mwenzako.
huwezi tena kulala nje ya nyumbani bila ruhusa ya mwenzako.
Huwezi tena kwenda kwenye starehe bila ruhusa ya mwenzako.
Huwezi kwenda safari ya mbali (kusalimia wazazi, wakwe, ndugu, n.k) bila ruhusa ya mwenzako.
Huwezi tena kuanzisha mradi bila kushauriana na mwenzako, etc, etc.......

Hapo kwenye uhuru ndio pagumu sana kwa watu wengi.
Watu wengi wanafukiri wanaweza kuendelea na uhuru wao waliokuwa nao kabla ya ndoa.
Ndio ugomvi unapoanzia hapo.....
 
hapo kwenye bold mkuu.........hizo akili zenyewe sasa..........mhhuuuu........i beg oooo (though sio wote)

mwanaume hufundishwi kuishi na mwanamke kwakua hawatabiriki na inafika mahala unaweza usijue anataka nini,nguzo kuu ya mwanaume ktk ndoa ni kuishi namwanamke kwa kutumia akili,mwanamke anafundishwa kwakua wanaume wengi kuna vitu basic na common ambavyo tulio wengi tunapenda kufanyiwa na wake zetu so anafundwa ili aje na hizo abc na kuongeza na yake
 
Mu-Israel umesema kweli kabisa, hata katika uchumba watu wengi huwa wanapishana hata kugombana sababu ya uhuru. unakuta mwingine keshazoea kwenda bar kila siku, club kila weekend, kutembelea marafiki kila anapojisikia na kurudi muda anaotaka,sasa ifikapo wakati huo ndio huwa mgumu maswali mengi hujitokeza mara upo wapi,unarudi saa ngapi, upo na nani. hebu mkuu nieleze wewe binafsi huwa unalitatuaje suala kama hilo la uhuru ikiwa ni mojawapo ya mafunzo uliyoyapata kanisani!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom