Swali kwa wapenzi wa kinywaji

Pomole

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
257
7
Kutokana na hali halisi ya usafi wa glasi kuwa kizungumkuti katika sehemu nyingi za vinywaji yaani hazioshwi,au hazioshwi vema au zinalowekwa tu kumekuwa na wimbi kubwa la watu kupiga tarumbeta(kunywea kupitia chupa bila glasi)
Chupa za siku hizi hasa ndovu zina karatasi laini ambayo inafunika hadi kifuniko!!ukichunguza kwa makini hii karatasi inawekwa na gundi fulani ambayo ina ka harufu ka kali tu ikiwa mbichi,swali langu ni kuwa hii gundi na hii karatasi ya dhahabu havina madhala kwa wanywaji,Naomba wataalamu mtusaidie ili tunywe kwa amani
nv.jpg
nd.JPG
n.jpg
 
Bora mi sinywi ndovu nakunywa castle lager bariiiiiiiiiiiidi inayovuja jasho.
 
haina madhara,mbona mimi nakunywa toka ziingie sokon lakn mpaka sasa niko poa.......ww piga ondoa shaka kwenye starehe(starehe gharama)
 
duuuuuuuuuuuuuuuuuu bora mimi nakunywa safari baridiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!
 
Kwa hali yoyote ile zile karatasi zitakuwa na madhara kwani kuna kemikali ambazo huwa zinatumika kutengeneza aina ile ya karatasi,na kwa kuwa zimewekwa kuifanya chupa iwe katika muonekano mzuri sidhani kama kuna viwango vya usalama wa mtumiaji wa kunywa kwa chupa vimezingatiwa,kama kuna mdau hapa wa TBL atujuze kuhusu hili.
 
Mimi nakunywaga Mbege,Gongo na Wanzuri!hayo mambo yenu mimi siyafahamu hata kidogo!!
 
Joseph -Nimekupata mdau-tusubiri wadau wa tbl watujuze vizuri
 
IGWE-Nimeipata comment yako-kuna wakati huwa tunafuta na tishu lakini vitengo vingine uswazi havina tishu!!Inawezekana madhala ya papo kwa papo hayapo!!ni vipi kwa yale ya muda mrefu??
 
MALLABA-Asante kwa ushauri wako japo huwa nasikia wajumbe wanasema ukinywa kama moja au mbili inaongeza damu!!sijajua kipi ni kipi ila ushauri wa kuacha utafikiriwa!
 
Ukinywa kama 'unanyonya' ndio tatizo lakini ukinywa kama 'unakiss' hutaigusa ile gundi.
Kuhusu harufu huwa inaisha unapofikia chupa ya 4 au ya 5 hivi.

"drink beer save water"
 
KIPINDUPINDU-Comment yko sijaelewa kunywa kwa kunyonya na kwa ku kiss ndio kunakuwaje?Hapo umeniacha ila kuhusu harufu nimekupata sana!!!nadhani ukishafika huko kwenye 4,5,au 6 hata gundi utaiona kama supu!!!ila sitaki kufika huko wengine vichwa vya panzi mbili ,tatu hoi..!!!
 
Ukifungua chupa ile sehemu ambayo mwanzo ilikuwa na kizibo inakuwa haina tena karatasi. Mpaka ulambe gundi ina maana wewe unadumbukiza chupa mdomoni kama unanyonya ninihii.... vinginevyo hakuna cha harufu wala cha gundi.
 
Back
Top Bottom