Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 9,527
- 14,403
Habari zenu wote?
Mimi nina swali hapa linanitatiza kidogo, kuna rafiki yangu wa karibu, ana mpenzi wake na mahusiano yao yamedumu kwa takribani miezi minne sasa, na kwa kipindi hiki wamekua katika mvutano wa hapa na pale na mshikaji anaonekana kazimika ile mbaya na kusema kweli wakati wanaanza mahusiano yao demu alikuwa yuko serious na jamaa kila baada ya dk 10 jamaa alikuwa anapokea simu au ujumbe, sijui ni nini kinaendelea kwa kipindi hiki mawasiliano ni adimu na mshikaji wangu anateseka sana juu ya hili.
Nimeanzisha hii thread mara baada ya siku ya jana mshikaji kunionesha ujumbe aliotumiwa na demu wake ulikuwa unasema; SIJAWAHI KUONA MWANAMME WA AJABU KAMA WEWE HUISHI KULALAMIKA, NA NIKIKUAMBIA TULICHOKUA TUNAFANYA NA X BOYFRIEND WANGU HAUTANITAMANI TENA NA NATAMANI KURUDIANA NAE.
Huo ndio ujumbe nimeuwasilisha kama ulivyo hivi ni kweli unaweza kurudiana na jamaa wako wa zamani ambae zaidi ya mara 4 umemfumania na wasichana tofauti? Kutokana na maelezo ya jamaa yangu anasema demu aliachana na mshikaji kwa ajili ya tabia za mshikaji, na baada ya muda mshikaji akaanza kumfuatilia demu na kuomba msamaha lakini demu alikuwa ameshamtapika mshikaji, maana watu wengi walijaribu kusuruhisha akiwemo mama mzazi na shangazi, dada zake jamaa lakini juhudi zote ziligonga mwamba na demu baadae akabadilisha namba za simu, ilifikia kuna kipindi demu alitumiwa kama shilingi laki tano kwenye akaunti na X BF wake lakini akazirudisha nyumbani kwa mama yake jamaa. Na huyu mshikaji wangu wa sasa anamhudumia sana mtoto lakini ndio hivyo. Kuna migogoro ambayo hata haieleweki nimejaribu kuongea na demu wa jamaa lakini hayuko wazi na anasema hakuna tatizo lakini jana usiku mshikaji wangu katumiwa ujumbe huo niliyouandika kwa herufi kubwa. HIVI NI KWELI WEWE DADA UNAWEZA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI MWENYE TABIA KAMA ZA HUYU JAMAA? NA UNAWEZA KUMWAMBIA MPENZI WAKO MPYA KUWA UNATAMANI KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI?
Nawasilisha!