Swali korofi: Hii ni sensa au siasa?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kama watanzania tulijiandaa kuhesabiwa jana tarehe 23 Agosti, 2022, mambo yamekuwa si mambo. Nilikuwa nyumbani kwangu Sombetini, Arusha tangu asubuhi hadi usiku nikawasubiri makarani wa sensa bila mafanikio, sikuhesabiwa.

Sitaki kusema mengi, sitaki kuonekana nachonga kwa mambo ya kitaifa kama haya ya sensa. Mambo ya sensa ni mambo ya kisasa, ni mambo muhimu kuliko ndimu kwenye maendeleo ya taifa letu. Lakini, kama kawaida yetu, siasa imeiingilia sensa yetu na kuitishia kuiharibu bila aibu.

Sensa yetu imegeuka uwanja wa kisasa wa siasa. Kwanza, siasa ilianza kwenye kuwapata makarani, CCM yetu ikateka mchakato na 'kuteua' makarani tuliowataka. Pili, matangazo yote ya sensa yalituma ujumbe mmoja wa wazi; sensa ingefanyika tarehe 23 Agosti, 2022.

Hawafiki watanzania mia waliojua kuwa sensa ingefanyika kwa siku saba. Nani alipaswa kutuambia mapema na kutuelewesha? Bila kutulewesha kuhusu hili hakutimiza wajibu wake, tumfanyaje? Pia, utitiri wa maswali ya sensa unasemwa kupunguza kasi ya zoezi la sensa.

Halafu, ni kama jana wamehesabiwa viongozi tu na 'wenye majina' huko mitaani. Asilimia kubwa ya wananchi wa kawaida hawakufikiwa na kuhesabiwa. Viongozi wanarindima mitandaoni kuonesha walivyohesabiwa. Ni sensa au siasa? La mwisho, malipo ya makarani yawe wazi; wanalipwa ngapi, lini na kwa namna gani? Kificho ni kitisho!

Sensa kwa maendeleo, sensa si upendeleo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kwenda Dodoma)
 
Sitaki kusema mengi. Sitaki kuonekana nachonga kwa mambo ya kitaifa kama haya ya sensa. Mambo ya sensa ni mambo ya kisasa. Ni mambo muhimu kuliko ndimu kwenye maendeleo ya taifa letu. Lakini, kama kawaida yetu, siasa imeiingilia sensa yetu na kuitishia kuiharibu bila aibu
Ingakuwa ni Uchaguzi ndio ungejua serikali ya CCM huwa iko makini kwenye mambo gani🤣🤣
 
La mwisho, malipo ya makarani yawe wazi: wanalipwa ngapi, lini na kwa namna gani? Kificho ni kitisho
Kuna wananchi wamenipigia simu jana kama wawili wanataka kuhakikisha habari wanazosikia eti Makarani wanalipwa Milioni moja kwa siku?

Hii ni hatari kwa makarai.
Uwazi unaleta usalama kuliko usiri.

Huko mitaani watu wanaamini makarani wanalipwa mamilioni ya pesa kwa siku. Jambo ambalo sio kweli.
 
Ndugu yangu kwanza nakupongeza kwa uzalendo wako wa kuamua kuwasubiri makarani wa Sensa ili uhesabiwe, pili napenda kukuomba uendeleza uzalendo huo ili makarani wakifika wapate taarifa zote, naomba nikuhakikishie kuwa hakuna atakaye achwa bila kuhesabiwa,

Zoezi hili linatumia mfumo mpya wa teknolojia ukilinganisha na sensa zilizotangulia huko nyuma, hivyo changamoto za hapa na pale Ni kawaida kutokea, lakini zoezi huku mitaani linaendelea vizuri tu,

Mimi Kama kijana niliye huku mitaani na ninayeifuatilia zoezi hili na Kuendelea kuwahamasisha watu kutoa ushirikiano kwa makarani wanasema zoezi linaendelea vizuri tu na ushirikiano wanatoa kwa makarani

Kuhusu sijuwi viongozi kuonekana wakihesabiwa siku ya Jana na kupiga picha ilikuwa Ni njia ya Kuendelea kuwahamasisha watanzania waendelee kutoa ushirikiano na wote tuhesabiwe, ndio maana hukuona siasa zozote maana hili siyo zoezi la kuhesabu wanachama wa chama chochote maana hiyo Ni kazi ya chama husika kujuwa idadi ya wanachama wake, ndio maana uliona hata viongozi wa upinzani wakihamasisha watu wahesabiwe

Nakuomba uungane nami Lucas mwashambwa kumsaidia mh Rais wetu mpendwa kuwahamasisha watanzania waweze kuhesabiwa, ili iwe lahisi kwa mh Rais wetu kupanga mipango ya maendeleo na kibajeti itakayo gusa maisha ya kila mtanzania na makundi yote, kupanga maendeleo ambayo hayatamuacha mtu nyuma
 
Nakuomba uungane nami Lucas mwashambwa kumsaidia mh Rais wetu mpendwa kuwahamasisha watanzania waweze kuhesabiwa, ili iwe lahisi kwa mh Rais wetu kupanga mipango ya maendeleo na kibajeti itakayo gusa maisha ya kila mtanzania na makundi yote, kupanga maendeleo ambayo hayatamuacha mtu nyuma
Hii sentensi yako ukiitafakari sana unaweza cheka hadi kuzimia,ni bajeti za hela ngapi zinatengwa kwa wananchi na hazitufikii sisi raia wa uku chini
 
Hizi sensa zimeshakuwepo 2002, ikafanyika tena 2012, na sasa 2022, huku wakituambia muhimu uhesabiwe ili serikali ijue mahitaji yetu.

Lakini bado mpaka leo kuna maeneo huku mijini bado hayana maji safi na salama, huko vijijini shule nyingi hazina matundu ya vyoo ya kutosha, na nyingine hata madawati bado ni tatizo.

Sasa kama kweli solution ya matatizo yetu ni kuhesabiwa, mbona hizo sensa zilizopita hazikuleta majibu sahihi ya hayo matatizo?

Basi wacha niungane nawe unavyosema hili zoezi la sensa limegeuzwa la kisiasa, na kugeuzwa huko hakujaanza mwaka huu, kumeanza zaidi ya miaka ishirini iliyopita.
 
Hakika uzalendo wako umeonekana kwa vitendo kwanza kwa kushiriki zoezi na kwa kutoa hamasa kwa wananchi wote waendeleze uzalendo kwa kutoa ushirikiano katika kukamilisha zoezi muhimu la sensa

Kwa vile umedhihirisha uzalendo, napenda kukupa kazi ili kusaidia kufanikisha zoezi hili. Jana mimi na watu wa nyumba yangu tumehesabiwa mapema sana yapata saa nne asubuhi. Makarani na mwakilishi wa serikali ya mtaa walieleza changamoto kuwa jirani na kwangu wamefunga nyumba na hawapo pamoja na kupewa taarifa jana yake, yaani Jumatatu bado hawakutoa ushirikiano

Kwa ufahamu wangu jirani zangu wengi ambao wanaishi nyumba za squatter nyingi ziko mabondeni ni watu wanaotoka mkoa wa Kigoma na Katavi.

Huku ni Kigamboni ya Wilaya ya Temeke. Taarifa tuliopata juwa gawataki kuhesabiwa. Pia wanaabudu kanisa ambalo mchungaji wao ni wa kutoka huko kwao Kigoma mwenye kuwaimanisha kuwa kuhesabiwa ni kinyume na maandiko ya Biblia.

Hivyo nadhani wamegoma kutokana na imani yao au pia kuogopa maswali wakidhani yanahoji uraia. Makarani wamepata shida kuwapata.

Ndugu Lucas mzalendo, unaweza kusaidia kuondoa hii changamoto naamini.
 
Hii sentensi yako ukiitafakari sana unaweza cheka hadi kuzimia,ni bajeti za hela ngapi zinatengwa kwa wananchi na hazitufikii sisi raia wa uku chini
Kwani huko uliko Hakuna huduma za kijamii zilizojengwa na kuboreshwa, hakuna Miundombinu iliyojengwa huko uliko, huoni Elimu ikitolewa bure kutoka darasa la kwanza Hadi kidato Cha sita
 
Hakika uzalendo wako umeonekana kwa vitendo kwanza kwa kushiriki zoezi na kwa kutoa hamasa kwa wananchi wote waendeleze uzalendo kwa kutoa ushirikiano katika kukamilisha zoezi muhimu la sensa.

Kwa vile umedhihirisha uzalendo, napenda kukupa kazi ili kusaidia kufanikisha zoezi hili. Jana mimi na watu wa nyumba yangu tumehesabiwa mapema sana yapata saa nne asubuhi. Makarani na mwakilishi wa serikali ya mtaa walieleza changamoto kuwa jirani na kwangu wamefunga nyumba na hawapo pamoja na kupewa taarifa jana yake, yaani Jumatatu bado hawakutoa ushirikiano. Kwa ufahamu wangu jirani zangu wengi ambao wanaishi nyumba za squatter nyingi ziko mabondeni ni watu wanaotoka mkoa wa Kigoma na Katavi. Huku ni Kigamboni ya Wilaya ya Temeke. Taarifa tuliopata juwa gawataki kuhesabiwa. Pia wanaabudu kanisa ambalo mchungaji wao ni wa kutoka huko kwao Kigoma mwenye kuwaimanisha kuwa kuhesabiwa ni kinyume na maandiko ya Biblia. Hivyo nadhani wamegoma kutokana na imani yao au pia kuogopa maswali wakidhani yanahoji uraia. Makarani wamepata shida kuwapata.

Ndugu Lucas mzalendo, unaweza kusaidia kuondoa hii changamoto naamini.
Kwanza lazima ieleweke kuwa kuhusu kuishi nchini kwa mtu asiye mtanzania Ni lazima mtu awe na vibari vyote halali, hivyo Kama hao watu siyo watanzania na hawana vibali vya kuwaruhusu kuishi hapa nchini lazima hatua za kisheria zichukue mkondo wake, maana hamuwezi mkajuwa hao Ni akina Nani na wapo hapa nchini kwa lengo gani, na wanadhamila gani, na wamefikaje mpaka hapo walipo, walipitia wapi na kusaidiwa na Nani kuvushwa mpakani na hata kuelekezwa njia za kupita mpaka kufika hapo walipo fika

Ulinzi wa Tanzania Ni jukumu letu sote watanzania, hivyo imani yangu Ni kuwa viongozi wa eneo husika watafuatilia kwa karibu na kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi ili lifanye uchunguzi kwa kufika katika kaya hizo na kufanya mahojiano nao na upekuzi pia wa kinyaraka na vitu vyote vitakavyopatikana hapo

Lakini pia Kama Ni watanzania na mnauhakika huo Basi naomba uongozi ufike hapo mahali na kuwataka watoke nje na kuwapa Elimu ya dhumuni la Sensa ya watu na makazi na kwamba hii siyo sensa ya kwanza, na kwamba taarifa za sensa Ni Siri na hazitolewi kwa mtu yoyote yule
 
Back
Top Bottom