Sumu ya sera ya majimbo ya Dr. Slaa na Mbowe kuwaua wabunge wa CHADEMA

lazima watajwe sana hawa jamaa kwani wamelifikisha taifa pabaya. wamejenga mitandao mibaya ya kuhujumu uchumi halafu wanasingizia ccm
Kwa hiyo mmeambiwa kuwa waliosababisha nchi kuwa masikini ni wachaga, halafu na wewe kwa kuwa uwezo wako wa kupembua mambo ni finyu ukaamini, pole sana.
 
suala si ya kibaguzi. hoja ya msingi ni maeneo kuendelezwa na raslimali za maeneo husika. hizo ulizozitaja ni jiografia za kiutawala na hazina uhusiano na matumizi ya raslimali katika eneo husika

Utakua unakula bangi wee, kweli kabisa yanatoka moyoni haya....
 
Ni mjinga pekee anaeweza kuamini propaganda zako. Sera ya Majimbo Cdm ipo toka inaanzishwa.
walitangaza mpango wa Tanzania kuongozwa katika Mfumo wa
Majimbo. Katika nadharia yao hiyo, ni kwamba nchi ya Tanzania
itagawanywa katika Majimbo ili kuharakisha shughuli za maendeleo.

Wametolea mfano kuwa mataifa mengi ikiwa ni pamoja na Marekani
yameendelea kwa vile kuna majimbo ambayo yana mamlaka ya kupanga na
kutekeleza mipango ya maendeleo katika majimbo yao. Kwa mujibu wa
nadharia yao hiyo ni kuwa Tanzania itakuwa na mamlaka mbili za
kiutawala.

Kutakuwa na serikali kuu ambayo itakuwa na wajibu wa kushughulikia
masuala ya kitaifa ikiwa ni pamoja na ulinzi na usalama sambamba na
ushirikiano wa kimataifa. Aidha, kutakuwa na serikali za majimbo ambazo
zitakuwa na jukumu la kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika
maeneo yao.

Katika kutekeleza hilo, CHADEMA wameanzisha kampeni za kueneza hoja yao
hiyo kwa wananchi huku ikiwashawishi wakatae raslimali zao kutumika kwa
manufaa ya Taifa. Mathalan, baada ya OPERESHENI OKOA KUSINI kutokuwa na
mafanikio, viongozi wa CHADEMA waliwashawishi viongozi wa vyama vingine
vya upinzani katika mikoa ya Lindi na Mtwara ili waanzishe kampeni ya
kupinga mradi wa Taifa wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar
es Salaam chini ya kauli mbiu GESI KWANZA, VYAMA BAADAYE, HAPA HAKITOKI
KITU. Kudhihirisha hilo, bendera ya CDM ilipeperushwa wakati wa
maandamano yaliyofanyika Desemba 2012 na Januari 2013.


  • Inawezekana kabisa CDM hawana watu wa kutosha wenye sifa za kuunda
    serikali kwa maana ya Rais, Makamu wa Rais, waziri Mkuu, mawaziri,
    Makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya n.k na hivyo kuona kama
    sera hii ni mwarobaini wa kukidhi idadi ndogo kabisa ya watu wenye sifa
    hizo ukimwondoa Mwenyekiti wa chama ambaye hata elimu yake ya kidato cha
    nne haioneshi alisoma shule gani, huku uzoefu wake wa kazi ikiwa ni
    karani wa benki kuu wakati Baba mkwe wake akiwa Gavana
  • Kwa maoni yangu ni kuwa, kitendo cha viongozi wa CHADEMA cha kuigawa
    nchi ambayo hawana mamlaka nayo ni uvunjwaji wa katiba na sheria za
    nchi. Kwamba, nchi ya Tanzania kwa sasa inaongozwa kwa mujibu wa katiba
    ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ambapo ndani ya katiba ya sasa
    hakuna kipengele kinachoelezea sera ya majimbo. Kwa kitendo cha
    viongozi wa CHADEMA kuigawa nchi wanastahili kuchukuliwa hatua za
    kisheria na kama ingekuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kimabavu, Dr
    Slaa na Mbowe hivi sasa wangekuwa wapo ndani ya magereza yetu wanasubiri
    hukumu ya kifo kwa makosa yao ya uhaini
  • Hapana ubishi kuwa mikoa kama Dar es salaam, Tanga, Pwani, Lindi na
    visiwa vya Zanzibar waumini wake wengi ni waislamu, huku mikoa kama
    Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Manyara waumini wake walio wengi ni
    wakristo. CDM wameamua kwa makusudi mazima kuwagawa watanzania kwa
    misingi ya udini, hoja ambayo wanajaribu kuwa-preempt CCM kuwa ndiyo
    wanaeneza udini. Hili linafanyika kwa makusudi hasa ukizingatia kuwa
    wote wanaopiga kelele za kuwa CCM ni wadini wote wamelelewa na kanisa
    (SLAA, MBOWE, LEMA, MNYIKA n.k), kwa ushahidi tazameni CV zao kwenye
    tovuti ya bunge mkajionee, hata machapisho yao ni vitabu vya dini.
  • Kuonesha kwa vitendo kuwa ni wadini kwa kuyaenzi maneno yalioko
    kwenye vitabu vitakatifu kuwa “KILA MTU ATAUBEBA MSALABA WAKE MWENYEWE”
    kwani sasa ile mikoa ambayo haina maliasili kama mito, maziwa, milima na
    madini na iko nyuma kimaendeleo iendelee kuwa maskini na ile yenye
    maliasili na iko mbele kimaendeleo na iendelee tajiri.

Sera ya Majimbo imeanzishwa kama sehemu ya kuingilia tu mwelekeo halisi
ni kuigawa nchi kimkoa. Katika maandalizi ya hilo, CHADEMA wameanzisha
Tovuti za kimkoa kama vile Mbeya Yetu, Katavi Yetu, Iringa Yetu, Lindi
Yetu, Mtwara Yetu, Dar es Salaam Yetu, Arusha Yetu na Zanzibar Yetu.
Mitandao hiyo imeratibiwa na kuendeshwa na CHADEMA kwa lengo la
kuhamasisha vijana ambao ndio watumiaji wakubwa kuichukia serikali na
kujitambua kimkoa chini ya dhana ya WAGAWE UWATAWALE.

  • Katika kuonyesha kuwa dhana yao hiyo haitekelezeki, viongozi wa
    CHADEMA na hasa FREEMAN MBOWE na dr WILBROAD SLAA wamekuwa wakitumia
    mapato ya kitaifa ya CHADEMA kuendeleza majimbo yao ikiwa ni pamoja na
    kutoa huduma za kijamii kama vile maji na afya huku akina MNYIKA
    wakitegemea hoja binafsi bungeni na maandamano kuondoa matatizo
    yanayowakabili hususan tatizo la maji ubungo. Kutokana na hali hiyo,
    wabunge wengi wa CHADEMA watapoteza majimbo yao katika uchaguzi wa 2015
    kwa vile wananchi wanatambua kuwa wabunge hao hawana uwezo wa kuwaletea
    maendeleo
  • DR SLAA na MBOWE wamekuwa wakihamasisha maandamano katika maeneo
    mbalimbali nchini kama mkakati mmojawapo wa kutekeleza sera hiyo ya
    majimbo. Kwa kutambua athari za maandamano, viongozi hao hawajawahi
    kuitisha maandamano hata siku moja katika majimbo yao. Mathalan, siku
    chache zijazo, MBOWE ataitisha maandamano mkoani Mbeya kushinikiza
 
patriote, kihistoria huko kigoma kulikuwa source ya manamba wa kwenda kufanya kazi kwenye mashamba ya kahawa Kilimanjaro na karafuu Zanzibar. kutokana na hali hiyo, jitihada za maendeleo zinazofanyika hazilingani na mahitaji halisi ya sasa. labda kitu ambacho mngeshauri ni kuwa serikali itenge fedha za kutosha katika yale maeneo ambayo hayana kasi kubwa ya maendeleo kuliko kugawanya kwa msingi wa idadi ya watu
Historia hiyo hiyo inatueleza kuwa Africa ilikuwa source ya Manamba kwenda America. Mbona leo hii waafrica wenzetu wapo mbali na tulipo sisi?? au tuliochukuliwa enzi hizo tulikuwa sisi tu?? Mimi nadhan tuache blah blah! Lipo tatizo la msingi lililofanywa na serikali ya CCM katika hii miaka 52 toka uhuru. Tunatakiwa tulitafutie ufumbuzi badala ya kutoa visingizio.
 
Mleta Mada kajikita kuwajadili Mbowe na Slaa badala ya kujadili Sera ya majimbo. kama kwamba Mbowe na Slaa wataendelea kuwa viongozi CDM milele yote.
Kama kuigawa nchi kwa misingi ya UDINI, Hiyo ni sera ya CCM na matunda tumeshaanza kula.
 
No one can stop this move at all. Nchi nyingi zilizofikia maendeleo zinatumia hizi sera za majimbo. Hata majirani zetu Kenya Jumatatu ijayo wanafanya uchaguzi wa kwanza chini ya katiba mpya na mojawapo ya watakaochaguliwa ni magavana wa majimbo wao wakiziita "County". Hawa magavana watawajibika kwa wananchi waliowachagua sio sisi eti mkuu wa mkoa anawajibika kwa Rais aliyemteau badala ya wananchi anaowaongoza. Huu wehu inabidi ukomeshwe hapa kwetu.
Tiba

Mkuu, umeeleza vizuri kuwa Katiba Mpya ya kenya imeruhusu mfumo wa majimbo. na hiyo ni baada ya wadau kujadili kwa kina juu ya mfumo gani wanautaka na jinsi utakavyofanya kazi. hayo wameyafanya kupitia katiba mpya. si ilani ya PNU, NARC, ODM au KANU. kwa hapa Tanzania ni kinyume. mchakato haujapitia kwenye katiba na CHADEMA wanajaribu kushinikiza ili katiba ijayo ibebe mawazo yao. hawana tofauti na wale waliokuwa wanatuma sms kushinikiza mahakama ya kadhi iwe kwenye katiba. tusubiri katiba ijayo itasemaje na wananchi tuna fursa ya kuamua kwenye referendum. kwa sasa tukubali kuwa kuhamasisha majimbo ni uchochezi nha uvunjaji wa sheria na wahusika wanastahili kuchukuliwa hatua za kisheria ingawa wanao uhuru wa kutoa mawazo yao katika mamlaka husika, tume ya katiba
 
kwenye huu uzi CCM wamekuja kwa kujipanga na wametumwa ila nawasikitikia hakuna mjinga anayeingia hapa jamvini hata wale wa vijijini wameshawakataa cha msingi hapa CCM zikaneni wenyewe tu
 
We scramble si ndo yule jamaa(alaf Mwalimu) aliyesema mwalimu haitaji kujua mtaala.. Anachohitaji kujua ni syllabus....

Duh! watu mnajua kupekuana, hivi huwezi tu kusoma post na kuipotezea mpaka umkariri aliyeandika na kumuweka kiporo? Sasa mnakumbuka mangapi? inaelekea chip ya Ubongo wako ina nafasi kubwa sana ya kuhifadhi mambo!
 
sina chama na kazi yangu ninayofanya hainiruhusu kuwa mwanasiasa
lakini katu siwezi kuwa mnafiki kama nyie magamba bali nawaunga mkono M4C
sera zao ni za ukombozi wa ukweli
badala ya kukesha JF kuwakosoa chadema tekelezeni ahadi zenu
wananchi hatuna muda wa kusikia matusi au ngonjera, tuna shida ya maji,umeme,ellimu kushuka nk
shetani alivo mwema kawatuma mmpoteze muda na zile ahadi zenu zaidi ya 100 hata 7% hamjatelekeza.

Huna chama ila bora uaunge mkono M4C? ndo chama gani hicho?
 
Mleta Mada kajikita kuwajadili Mbowe na Slaa badala ya kujadili Sera ya majimbo. kama kwamba Mbowe na Slaa wataendelea kuwa viongozi CDM milele yote.
Kama kuigawa nchi kwa misingi ya UDINI, Hiyo ni sera ya CCM na matunda tumeshaanza kula.

MBOWE na SLAA lazima wajadiliwe kwa vile wanatumia vibaya mapato ya CDM kuendeleza majimbo yao huku akina ZITO na HALIMA MDEE wakiambiwa waendeleze majimbo yao kwa raslimali zilizopo kwao. Hata ofisi za chama za Majimbo tofauti na ya Slaa, Mbowe, Lisu hazipewi ruzuku kwa madai kuwa watafute vyanzo wenyewe huku mapato ya taifa yakitumika kujikopesha wakubwa hao
 
Kila anapoguswa SLAA na MBOWE unaambiwa lumumba hii tafsiri yake nini, mko mitandaoni kwa hisani ya watu fulani na siyo kutoa maoni yenye kulijenga taifa? Kama ndiyo hivyo basi tuna kazi kubwa ya kuwaelimisha watanzania wanavyolaghaiwa na wanasiasa. Hakuna utumwa mbaya kama huu wa kutumiwa kuvuruga mawazo ya watu.
Mtakunya mwaka huu masisiem na laana zenu,huo unaosema ni uvunjifu wa sheria na viongozi wakamatwe mimi nasema kamkamateni kwanza chenge na vijisenti,mamvi na richimond,ngeleja na ufisadi wa wizara,magembe,kinana na tembo wet na mafisadi wengine kibao wa masisiem ndo uje ulete hii shombo yako hapa....ptyuuuuuuuuu,tupa kule!!!
 
USITOE mifano ya USA ambayo hulingani nayo hata kwa chembe. Umetolewa mfano wa Nigeria ambayo tunafanana katika mambo mengi wewe unaulizia kuhusu USA. Pitia kwenye historia uone kwa nini USA wamekuwa na mfumo huo na kaone ikiwa majimbo yote yapo sawa kimaendeleo. Je hapa TZ unafikiri hali itakuwaje? nikiifikiria kigoma, rukwa na Lindi
Nigeria hawakugawa nchi ki majimbo kwa lengo la kuharakisha maendeleo, walilazimika kugawa kwa sababu za kidini, kuna watukufu waislamu wa Nigeria waliotaka kuongozwa na dini ndio maana ya kugawika kimajimbo, Kwa hiyo Nigeria sio mfano sahihi.
 
kwenye huu uzi CCM wamekuja kwa kujipanga na wametumwa ila nawasikitikia hakuna mjinga anayeingia hapa jamvini hata wale wa vijijini wameshawakataa cha msingi hapa CCM zikaneni wenyewe tu

Haya mawazo ya kwamba kila linalochangiwa humu likawagusa moja kwa moja SLAA na MBOWE ni umbumbumbu na kukosa hoja. Ni dhahiri kwamba mmekamatika vilivyo.
 
Historia hiyo hiyo inatueleza kuwa Africa ilikuwa source ya Manamba kwenda America. Mbona leo hii waafrica wenzetu wapo mbali na tulipo sisi?? au tuliochukuliwa enzi hizo tulikuwa sisi tu?? Mimi nadhan tuache blah blah! Lipo tatizo la msingi lililofanywa na serikali ya CCM katika hii miaka 52 toka uhuru. Tunatakiwa tulitafutie ufumbuzi badala ya kutoa visingizio.

kwa ujumla nchi zote za afrika ni maskini ila kiwango cha umaskini kinatofautiana. hata mataifa yaliyoendelea afrika kama Afrika ya Kusini, Angola na Nigeria, maendeleo hayako sawa na ndio maana kuna mapigano ya mara kwa mara na migomo ya wananchi na watumishi kutokana na ugumu wa maisha. suala la msingi ni kutafakari kama taifa na si kutafuta ufumbuzi kwa njia zisizofanyiwa upembuzi yakinifu
 
We scramble si ndo yule jamaa(alaf Mwalimu) aliyesema mwalimu haitaji kujua mtaala.. Anachohitaji kujua ni syllabus....

ndiyo mimi lkn mbona hii ni mada nyingine. japo siipendi ccm lkn siungi mkono sera ya majimbo. sera hiyo itatugawa na nchi itameguka! huo ndiyo msimamo wangu. una maoni gani kuhusu majimbo?
 
Back
Top Bottom