Sumry SKS bus vimeo.

Anyways, nafikiri umri wangu unachangia, n ina mawazo tofauti kidogo.
Tunajua kuwa chombo cha usafiri kupata hitilafu ni kawaida lakini wahudu wanatakiwa kuwa na njia mbadala ya kushughulika na tatizo hilo na kutoa taarifa ya maendeleo.
Ila inapooneka kuwa ni mara kwa mara au mmekaa muda mrefu unaweza kupeleka malalamiko yako katika ofisi za SUMATRA, nafikiri kwa mara ya kwanza najaribu kuamini utendaji wa SUMATRA kama shirika la umma, wanafanya kazi vizuri sana na kwa weledi, hata kama ni kupotelewa na mzigo.
 
Safi sana, naona makonda mnabishana kisawasawa! Napenda sana stori za mabasi, na kusafiria. Yutong gani inatoka dar kwenda pemba? Nataka kwenda mwezi wa tatu
 
Nakubaliana na mtoa mada hapo juu.
Sumry ni kampuni uliyojizolea umaarufu kwa miaka ya kati kutokana na usafiri wao wa uhakika na wa raha.
Sumry aliingia mkenge baada ya kuingiza hizi nissan dizel sks ambazo kimuonekano na comfortability ni nzuri sana.
Zile gari nyingi zilishindwa safari na kumuingizia hasara.
Ila kiujumla nissan ni bonge la gari na hakuna wa kuifuata ikitulia barabarani.

Nissan diesel haiwezi kufukuzana na scania iwe kwenye tambarare milima au miteremko, kuna scania engine yake ni F330 balaa tupu, Allys alikuwa na hizo engine ilikuwa ni balaa nakumbuka mwaka 2009-2010 Dar unaondoka 12 abh mwanza unaingia saa 1 jioni kipindi hicho malori barabarani yalikuwa kidogo siyo kama sasa hv ni kero
 
Back
Top Bottom