Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Nimeyashuhudia mara nyingi sana haya mabasi yakiharibika hovyo njiani.Sio siri,haya mabasi i.e sumry na mbeya express yasipoharibika njiani,basi mjue mbeya mtaingia saa 11 mapema.Haya mabasi yana mwendo mkali sana hata akina Happynation hawana ubavu kufukuzana nayo.Kasoro kuu ya haya mabasi ni kuharibika njiani mara kwa mara.SKS buses ni mabasi mazuri lakini hayataki shuruba kama wanavyoyaendesha madereva wa haya mabasi.Madereva wa sumry wana husudu mno kuweka ligi dhidi ya mabasi kama Scania ambayo ni imara.Unapokwenda mkoani mbeya sikushauri utumie mabasi haya kwani hayaaminiki.Ni bora upande happynation,nganga,ndenjela,al saedy,greenstar,hood,sai baba na ottawa.