Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 734
Yaani ni wizi wizi wizi wizi wizi wizi wizi wizi wizi wizi wizi wizi wizi wizi
JK angekuwa ni mtu wa kusoma alama za nyakati, angejiondoa tu kwenye kinyang'anyiro cha uraisi.
Hakuna haja ya kubaki madarakani kwa mtutu wa bunduki.
eYana ukweli lakini ni mazito sana. Mimi sijaamini sana kama serikali inahusika moja kwa moja na matukio yote haya. Wenye nchi wanapitia humu watatupa uhakika wa haya mambo.
Mwenzio kasema karibu tujadiri.... Sasa wewe hapo ndo umejadiri nini? Halafu what is the defn ya bushman kwako? Maana kwangu mimi bushman ni mtu yeyote anayetoka nje ya mada pale anapotakiwa kuchangia mada.Once yr a bushman, you will never change. point yako haina mshiko. Mchonganishi mkubwa wewe.
Yana ukweli lakini ni mazito sana. Mimi sijaamini sana kama serikali inahusika moja kwa moja na matukio yote haya. Wenye nchi wanapitia humu watatupa uhakika wa haya mambo.
Once yr a bushman, you will never change. point yako haina mshiko. Mchonganishi mkubwa wewe.
Wana jf habari;
nimejaribu kutafakari maneno ya waziri mkuu mstaafu mh.fredrick t.sumaye aliyosasema wakati wa kinyang'anyilo cha urais mwaka 2005 naona dalili zote za kutimia maneno yake alisema "anayefagia njia ya kwenda ikulu kwa kalamu na karatasi basi akifika huko atatumia risasi ili aweze kutawala"maneno haya aliyasema mzee sumaye baada ya kuchafuliwa na genge la wanamtandao ambalo lilikuwa linaongozwa na ;
- jakaya m.kikwete
- edward n.lowasa
- emmanuel nchimbi
- rostam azizi n.k
sumaye baada ya kuona anaandamwa sana na kashfa ambazo hazina kichwa wala miguu ilibidi aweke kumbukumbu kwa kutamka maneno hayo sasa toka wakati huo kumbukumbu zangu zinanionyesha yafuatayo yametokea;
""je unazungumziaje maneno ya mh.sumaye na wakati huu ambao kumeibuka mtindo wakuteka waandishi wa habari na kuwang'oa kucha na meno bila ganzi"" karibu tujadili
- mauji ya wafuasi wa cdm arusha.
- kumwagiwa tindikali saed kubenea
- kuwekewa sumu dr,mwakyembe
- mauji ya songea
- mauji ya morogoro
- mauji ya daud mwangosi
- kutekwa kwa dr.ulimboka
- kuuwawa kwa padre evarist mushi
- kutekwa kwa absalom kiband n.k (ongeza matukio mengine ambayo yamesaulika hapa)
Mkuu, kuna watu huwa hawaamini kwa common reasoning, eidha kwa makusudi au kwa kutoelewa mambo, yaani hadi na yeye awe muhanga wa tukio kama hilo ndo ataamini.Mkuu ni vyema ukafahamu serikali ya nchi yoyote ile ina mkono mrefu sana; kwa mfano nchini Tnzania kuna Usalama wa Taifa (UWT), Jeshi la wananchi (JWTZ), Polisi, Askari magereza, na mashushu kibao, amini usiamini hata hapo ulipo wapo.
Hivyo basi likitokea tukio linalo husiana na kutoa uhai wa binadamu, kisha wahusika wasifahamike na kuchukuliwa hatua stahiki, hamna haja ya kusumbua kichwa chako, kwani mhusika mkuu atakuwa ni serikali. Jiulize kwa nini wahusika waliochomoa uhai wa kamanda Barlow walitiwa mbaroni ndani ya siku mbili baada ya tukio? kwa nini isiwe vivyo hivyo kwa matukio mengine yanayo fanana na hayo? Je ulisoma makala ya Kubenea kuhusiana na sakata la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka? Je kwa nini Ramadhani Ighondu ambaye alitajwa na Dk. Ulimboka mwenyewe hakamatiki?
Mkuu in short maswali ni mengi sana kuliko majibu.
Kwenye bold, HIVI UKIHARIBU OFISI, ANAYETAKIWA KUKUPA ADHABU NI NANI KAMA SI BOSI WAKO AU HR? Sasa kama HR kimya, bosi wako kimya na wewe ndo unaendelea kuharibu, wengine tusemeje wakati uharibifu wako unatuumiza wengine ?? KWENYE KUMTETEA YES TUMTETEE... PINDA ALISHAWAHI KUSEMA, KAMA INGEKUWA NI UWEZO WAKE ANGEMFAYA MTU FULANI HIVI WAKATI RAIS AKIWA AFRIKA KUSINI LAKINI ALISHINDWA KWA SABABU MWENYE MADARAKA YALE ALIKUWA RAISI ... Usimtetee, hapo anaonyesha udhaifuJapo wengi tunamlaumu Mh Rais kwa kukaa kimya muda mrefu linapotoke jambo nikitofautisha na Ally Hassan Mwinyi (Rais Mstaafu), Mh Benjamin W Mkapa (Rais Mstaafu na yule Muasisi wetu Mh. Dr. Julius K. Nyerere,
Hoja yako ya kumshutumu moja kwa moja Rais Kikwete, nakaa pembeni siungi mkono. Inawezekana ni watendaji wake wanayakoroga mambo haya, tafakari, chukua hatua.
Ushauri wangu kwa Mh. Rais, japo si jambo jema wewe kama Mh. Rais kufanya kazi kwa kuombwa na vyombo vya mawasiliano, mimi nakushauri tu kwamba inapotokea jambo uwe unatoa TAMKO MAPEMA usisubiri mwisho wa mwezi, maana wakati mwingine tukio linatokea tarehe 2 ya mwezi kukaa na jambo hadi tarehe 31 inakuwa inatia wasi wasi.