Sumaye amgwaya Lowassa!

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Wakuu,

Nipo kwenye ukumbi tayari na nitawajuza kila kinachoendelea ikiwa ni pamoja na picha. Mods mtanisadia kuziweka sawa kwakuwa nitakuwa naandika kadiri matukio yanavyojiri.

Ni hapa Courtyard Hotel - Dar

attachment.php


• Akana kuwa na uhasama naye, adai hamwogopi mtu

na Edson Kamukara

WAZIRI Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, ametoa dukuduku lake la moyoni akisema hana uhasama na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa na kubainisha kuwa rushwa ya kimtandao iliyokighubika Chama cha Mapinduzi (CCM), ndiyo iliyomwangusha wilayani Hanang'.

Sumaye ambaye amepigwa mweleka kwenye uchaguzi wa ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa kupitia wilayani Hanang' na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji na Uwezeshaji), Mary Nagu, alikutana na wanahabari kuelezea mwendo mzima wa uchaguzi huo na hatima ya CCM.

Akizungumza kwa kujiamini huku akinukuu kauli zake za nyuma kuhusu mwenendo wa rushwa ndani ya chama chake, alisema uchaguzi wa Hanang' ulighubikwa na matumizi makubwa ya rushwa, vitisho vingi, uharamia wa kuhamisha wapiga kura usiku na maovu mengineyo mengi.

"La msingi ni kuwa mimi sijakata na wala sitakata rufaa ya kupinga matokeo wala kupeleka malalamiko katika chama changu kwa sababu yaliyokuwa yakitendeka yalikuwa yanafahamika," alisema.

Katika kile kinachoweza kutafsiriwa kama kuondoa uvumi uliokuwepo kuwa Sumaye na Lowassa wana ugomvi wa kisiasa hasa wakati huu wa kujipanga kuelekea mbio za urais 2015, kiongozi huyo alisema hajazungumza na mtu kuhusiana na mambo hayo.

Sumaye alisema taarifa hizo zimekuwa zikisambazwa na kunukuliwa kuwa zimetoka kwenye chanzo kilicho karibu naye, lakini akafafanua kuwa hawezi kupambana na Lowassa kwa sababu hana uhasama naye.

"Nikiamua kugombea urais sitagombea kwa sababu ya mtu fulani bali nitagombea kwa sababu ya nchi na wananchi wa Tanzania," alisema.

Akifafanua kuhusu vitendo vya rushwa ndani ya CCM, alisema kuwa nchi nyingi hasa zenye demokrasia changa kama Tanzania zimeingia katika vurugu na kuhatarisha amani na utulivu nyakati za uchaguzi.

Sumaye alisema madaraka yatakuja tu kama wananchi wapiga kura wanaona wewe ndiye utayewafaa na wala wasirubuniwe kwa fedha au jambo lolote kwa kutumia vibaya nafasi ya umaskini wao.

"Hivi leo tunavyoongea hali ya rushwa wakati wa uchaguzi imekuwa mbaya zaidi. Katika uchaguzi wa kidemokrasia wapiga kura humchagua mwakilishi wanayemtaka kwa sababu ya uwezo wake yaani humchagua mwakilishi wao kwa ajili yao.

"Katika demokrasia iliyopondeka kwa rushwa, fedha huwachagulia watu mwakilishi kwa ajili ya waliotoa fedha. Wapiga kura ni wapiga mihuri tu," alisema.

Sumaye bila kutaja majina ya wahusika, alisema hali imetoka kwenye kuhonga ili achaguliwe katika eneo lake na badala yake kuna rushwa za kimtandao ambapo mtu hutoa fedha katika maeneo mbalimbali nchini ili watakaochaguliwa wawe wafuasi wake mbele ya safari atakapowahitaji.

"Uchaguzi huu umeghubikwa sana na matumizi makubwa ya fedha za rushwa. Suala la rushwa katika nchi yetu na katika CCM siyo mgeni lakini sasa tatizo hilo limeota mizizi na linazidi kuwa kubwa," alisema.

Kuhusu kwenda CHADEMA
Sumaye alikanusha vikali akisema hajawahi kukutana na kiongozi yeyote wa CHADEMA wala chama chochote cha upinzani.
Lakini akabainisha kuwa hawapaswi kufikia kudai kuwa vyama vya upinzani au viongozi wake ni maadui wa CCM.

"Mimi ningekuwa nimekutana nao ningesema tu mbona hata hao wengine wanaoutafuta urais kwa udi na uvumba huwa wanakutana nao? Alihoji.

Alisema yeye ni mwanachama mwaminifu wa CCM na kwamba alishawahi kusema kuwa hayuko kwa ajili ya cheo na wala kukosa ujumbe wa NEC na hasa kwa njia iliyotumika hakumnyimi usingizi wala hahuzuniki kugombea urais kwa tiketi ya CCM endapo ataamua kufanya hivyo.

Sumaye alisema kama ni matatizo, vyama vyote vina kasoro zake, hivyo haoni kama kuhama chama ni suluhu na kutamba kuwa kushindwa kwake kumempa nguvu zaidi na hivyo akiamua kugombea urais lazima apitie CCM.

Kuhusu TAKUKURU
Alipoulizwa kuhusu utendaji wa Taaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kama imetimiza wajibu wake kushughulikia tuhuma za rushwa kwenye uchaguzi wilayani Hanang', Sumaye alitafakari kidogo kisha akajibu kwa kutumia mfano.

"Hivi kama nyie wanahabari mmekuja hapa mkanisikiliza haya ninayowaeleza, halafu kesho watu wanasoma kwenye magazeti yenu hawakuti kitu au kwenye televisheni hawaoni, wanaweza kusema mmetimiza jukumu lenu? Alihoji Sumaye.

Kada huyo aliwaachia wanahabari watafsiri wenyewe kama kweli TAKUKURU inatimiza wajibu wake katika kushughulikia madai ya rushwa kwenye chaguzi.

"Napenda nitambue kuwa haya ninayoyasema si matamu masikioni mwa baadhi yetu lakini ni vema tukayasikiliza kwa makini na kuchukua hatua chanya ili yasilete madhara zaidi katika jamii na wala tusidiriki kuwanyamazisha wanaoyazungumzia
 

Attachments

  • sumaye-leo.jpg
    sumaye-leo.jpg
    35.9 KB · Views: 6,037
  • sumaye-leo1.jpg
    sumaye-leo1.jpg
    45.3 KB · Views: 7,944
Muda wowote kuanzia sasa ataanza kuongea, kishawasili
 
Tuko pamoja mkuu, tupe anasemaje mheshiwa. Nategemea atoe maamuzi mazito kwamba anajitoa CCM ila hasije CDM
 
Ameanzia kanisani Azania Front, ndio maana kachelewa kuanza.
 
Sumaye:

Sijawahi kukutana na Chadema wala yeyote wa upinzani.... Lakini upinzani si uadui, ni Watznania... Kama ningekutana nao, ningesema tu kwamba mbona na wengine wanakutana nao na wanagombea Urais...

Kuna uvumi mzito kuwa kama nitaingia Chadema nitashughulikiwa.

Dawa si kushughulikia wanaokihama chama bali sababu ya wanachokihama... Kukosa NEC hakuninyimi usingizi wala hakunizuii kugombea Urais kama nitataka...

Mwalimu alisema Chama si mama yake
 
Sumaye: Tusiandame watu bali tuandame maovu
 
Sumaye:
Mambo ya Hanang, yalitokea nchi nzima... Na yalitokea kwa staili tofauti

Tatizo ni kubwa sana, maana nchi nzima mattumizi makubwa ya fedha... Tatizo ni kubwa na limeota mizizi

Nimewahi kuzungumzia mara kadhaa...

Nilisema nikiwa Same "Rushwa ni tatizo Barani na Tanzania pia... Kwetu sisi huwezi kushinda bila kutoa fedha"

Nilisema haya 2010:

"Kiongozi anayetoa rushwa anapata wapi kama si mwizi na mla rushwa... Hawezi kuwatendea haki maana wananchi ni kama bidhaa na hatawatumikia bali atatfuta za kihonga baadae"
 
Sumaye:
Mambo ya Hanang, yalitokea nchi nzima... Na yalitokea kwa staili tofauti

Tatizo ni kubwa sana, maana nchi nzima mattumizi makubwa ya fedha... Tatizo ni kubwa na limeota mizizi

Nimewahi kuzungumzia mara kadhaa...

Nilisema nikiwa Same "Rushwa ni tatizo Barani na Tanzania pia... Kwetu sisi huwezi kushinda bila kutoa fedha"

Nilisema haya 2010:

"Kiongozi anayetoa rushwa anapata wapi kama si mwizi na mla rushwa... Hawezi kuwatendea haki maana wananchi ni kama bidhaa na hatawatumikia bali atatfuta za kihonga baadae"

Aseme ni nani anatoa Rushwa. Kama ni mkweli ataje watu kwa majina na si kusema kuna watu bila kutaja majina. Kama anajeuri. CCM wote wameoza
 
Sumaye:

Baadhi ya taarifa katika magazeti na taarifa za habari.... Kuna gazeti limeandika "Sumaye kupasua jipu Dar es Salaam...." Sina jipu wala jipu wala bomu la kupasua.

Kuna lililonishangaza kwamba 'Sumaye amtangazia jipu Lowassa, ikiwa ataingia Lowassa basi atamkabili kwa namna yoyote....'

Hakuna aliyezungumza na mimi kwamba nitapambana na Lowassa, siamini kama kuna source ya karibu na mimi. Basi sikifahamu na kama chanzo kipo sikifahamu, sijaongea na mtu na wala nisingeweza kuyasema, sina uhasama na Lowassa, na niliamua kugombea sitogombea kwa sababu ya mtu, bali kwa sababu ya maslahi ya nchi na si ya mtu.
 
Sumaye: Tusiandame watu bali tuandame maovu

ma body guard wake wa TISS wapo naye hapo mkutanoni? maana ukiwa PM mstaafu si unalindwa kila kona na hao UWT, nahisi haohao ndio wanam-feed habari JK na EL kama vipi angekataa ulinzi!
 
Hadi hapo naona hamna jipya kabla hata hajamaliza,. Hawa ccm wanatuchezea akili
 
Sumaye:
Nilisema kiongozi anatumia rushwa hatajali umma bali atatafuta fedha kunnua tena... CCM lazima tupige vita rushwa... Nilisema haya Julai 7 mwaka jana...

Nasema haya isionekane nasema haya baada ya kushindwa Hanang
 
Katika uchaguzi wa demokrasia, mtu huchaguliwa kwa uwezo na kwa ajili yao kuwatumikia, katika demokrasia ya rushwa, fedha huwachagulia watu mwakilishi kwa ajili ya waliotoa fedha, kama nimetoa fedha kwa ajili yako, na wapiga kura wanakua wapiga mihuri.

Sasa imetoka mtu kuhonga achaguliwe, na sasa mtu anatoa rushwa kununua watu ili apate kujenga mtandao wake na sasa ni rushwa ya kimtandao ambayo ni hatari sana...
 
Nimeshastuka hakuna jipya hapa. Yale yale ya EL kusema sikukutana na JK barabarani. Aseme ameita mkutano kusema nini hasa
 
Back
Top Bottom