SUMATRA yasitisha mabasi 14 ya Dar Express

Sijui ni ajali gani wanaziongelea hapa...maana sijawahi sikia Dar Express imepinduka au kugongana na gari nyingine kusababisha vifo au majeruhi kadhaa! Kama unafungia Dar Express kwa mfano wa kugonga mpanda piki piki, sijui utafungia magari mangapi maana hawa jamaa wanagongwa kila siku na madereva wengi mnajua jinsi piki piki zinavyoendeshwa vibaya siku hizi na watu wasio hata na leseni wala kujua miongozo ya usalama barabarani! Kumekuwa na mlolongo wa jali mbaya za kutisha ambazo zimesababisha vifo vingi sana na vilema kibao, sijasikia Dar Express kuhusika hata kwenye ajali moja kati ya hizo...wala sijasikia hayo makampuni yaliyohusika kufungiwa!
 
YAMEBAKI MANGAPI yanayofanya kazi? au ndo wamefungia yote? high season hii ndo inaanza wachaga na kuhesabiwa sijui itakuwaje
AHaaaaaaaaaaaa, kumbe ni magamba+masaburi at work katika kile kinachoitwa "frustration approach"!
 
Nilifikiri SUMATRA wangewapa DAR EXPRESS tuzo ya kuendesha biashara ya usafirishaji wa nchi kavu kwa umahiri mkubwa. Hapa kuna mkono wa mtu hususani biashara ya High Way Restaurant
 
  • Thanks
Reactions: GP
Yawezekana mmiliki wa Dar Express ni CHADEMA damu ndo maana wameamua kumkomoa kama Lema vile.
 
Nilifikiri SUMATRA wangewapa DAR EXPRESS tuzo ya kuendesha biashara ya usafirishaji wa nchi kavu kwa umahiri mkubwa. Hapa kuna mkono wa mtu hususani biashara ya High Way Restaurant

Mwaga taarifa zaidi mkuu hapo kwenye blue.
 
Hapa nimeamini vyombo vyetu vinatumika kuharibiana biashara..siamini kama SUMATRA wamekubali kuonyesha ujinga wao kiasi hiki. Kwanza wamemfungia katika high season ambapo mabasi ya Dar express yamekuwa tegemeo la wasafiri wa Arusha. Wanachofanya ni kudistabilise ili na wengine wapate abiria. Hii inawezekana pale tu hata viongozi wa SUMATRA na Polisi wanapokuwa wamiliki na wadau wa vyombo vya usafiri. Jaribu kufuatilia utaambiwa jamaa wa SUMATRA ameingiza mabasi yake au anashare na kampuni fulani..lets be profesional jamani.
 
Mwaga taarifa zaidi mkuu hapo kwenye blue.

Nasikia kuna kampuni mpya ya yule kijana anapigiwa kelele na uvccm inaanzishwa. Pengine ndiyo mkakati sasa wa kuifungia Dar Express ili katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka watu watengeneze pesa! Dar Express imeleta mageuzi makubwa ktk makapuni ya usafirishaji abiria kanda ya kaskazini. Kwa kuiga mfano wa huduma nzuri na mabasi ya kisasa,kampuni nyingi zimebadilika sana na ajali za mabasi zimepungua sana ktk kanda ya kaskazini. Sasa kama imefungiwa,basi hakuna kampuni ya mabasi inafaa kusafirisha abiria ktk Tanzania.
 
Mohamed na Sumri ni magwiji wa hongo na rushwa ndio maana wao hawakumbwi na fagio la chuma.
...labda Mrema naye atahitajika kukata kitu kidogo...ajali sio Dar Express peke yao labda kuna kitu kingine...
 
hatuwezi jua ukute huyo mwendesha pikipiki aliegongwa na mabasi ya darexpress ni ndugu wa kibosile wa sumatra sasa machungu ya kupoteza ndugu yake anafanya uwamuzi wa kijinga!!!

lile basi liloteketea kwa moto juzi na kuwa watu mbona sijasikia limefungiwa!!???? mohamed trans kila kukicha linatoa roho za watu mbona kimya, simri nalenyewe hivyo hivyo kimya yanapeta tu barabarani..... hii nchi tunakoelekea sijui ni wapi??

madereva wa darexpress wanapewa mafunzo ya udereva salama chini ya DT Dobbie tanzania sasa sijui hizi hongo zitatufikisha wapi tunatowa vizuri tunapewa vibovu ama ndio mkakati wa kupunguza idadi ya watu unaanza taratibu.!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
dar express tunaipenda sababu wamiliki wake hawatutoi abiria KAFARA. Ajali zote hapo juu ni mpita kwa miguu alofariki.
Magari mengine, unasikia si chini ya abiria 16 walifariki.

Inashangaza sana maana hizo zilizotajwa ni ajali ndogo ndogo, nani mmiliki wa Dar express? kama ni mtanzania mweusi sitashangaa maana waarabu na wahindi wamejipa haki milki ya biashara za nchi hii
 
Ni kweli mkuu, hata mimi sijawahi kusikia ajali mbaya ya dar express. sumatra wana lao jambo
 
hizo sababu ni za kijinga hata mtoto mdogo humdanganyi atagundua, abood imeuwa watu sana mpaka wakaiita chinja chinja, sumri imeuwa watu sana halikadhalika mohamed trans kila siku ajali mbona hayasimamishwi? , pia kuna mabasi kibao yanabeba abiria hata ukiyatazama tu kwa macho bila kuwa mtalamu wa usalama barabarani utagundua ni mabovu na yanaendeshwa kwa mwendo kasi bila tahadhari lakini utashangaa yanapitaje barabarani bila kuzuiliwa
tanzania hii mtu anayefanya biashara kwa mafanikio makubwa bila kuwagawia ela viongozi wa ccm anakuwa adui mkubwa wa serikali, reginald mengi ameligundua hilo akaigiza yupo karibu na ccm ndio maana anaendelea vizuri
 
dar express tunaipenda sababu wamiliki wake hawatutoi abiria KAFARA. Ajali zote hapo juu ni mpita kwa miguu alofariki.
Magari mengine, unasikia si chini ya abiria 16 walifariki.
mh huo si uungwana hata kidogo, maana huyo mmoja aliyekufa anaweza kuwa na familia kubwa inayomtegemea. akifa tu maisha kwa famiia yanakuwa shagara bagara.
 
nauli zake haziendani na huduma wanazotoa. mfano kuna basi limepewa hadhi ya luxury na nauli ni shilingi 30,000 likiwa na maana ya full ac and tv. lakini ukilipanda neither tv nor ac. full vurugu. ticketi na namba ya basi ninayo kwa ushahidi hii ni fraud lakini watanzania huwa tunaona poa tu.
 
Back
Top Bottom