SUMATRA yasitisha mabasi 14 ya Dar Express

hivi huyu muzachai anaongea nini apo juu.........mi dar express ni usafiri wangu na wa wapenzi wengi wa safari zisizo na mashaka..masaa 9-10 barabarani!!mwendo mzuri/muda wa kuchuma dawa/lunch nzuri nz sina record yeyote seriuos ya mabasi haya achilia mbali siku hizi ajali za kaskazini zimepungua...........

kuna mkono wa sumatra hapa.si bure. yani hii nji hii nimeichoka.........kil akukicha ni visa dawa yenu ipo njiani anakuja nayo cameron
 
wakati mwengine unakuta hii ni mkakati wa kibiashara zaidi.
Yani lengo lao ni kuwachafulia jina lao (dar express) kibiashara kwa watu, ili watu wasiyaamini tena haya magari.
Mjini shule, SUMATRA kuhongwa na wamiliki wengine wa mabasi wafanye ivo hawashindwi.
Nalo neno.
 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imesitisha safari za mabasi 14 ya kampuni za Dar Express kutoa huduma kati ya Dar es Salaam- Arusha na Arusha-Tanga kuanzia kesho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sumatra jana, mamlaka hiyo kupitia kifungu namba 15 cha Sheria ya Sumatra namba 9 ya mwaka 2001, imeiagiza Kampuni ya Dar Express kusitisha utoaji huduma kwa magari yake yote yanayotoa huduma ya usafiri kati ya Dar - Arusha na Arusha- Tanga kuanzia kesho.

"Kutokana na kuwapo kwa matukio mengi ya ajali yaliyohusisha mabasi yanayomilikiwa na kampuni hiyo kwa kipindi kisichozidi miezi 10, mamlaka inatilia mashaka sifa za madereva wa mabasi ya Kampuni ya Dar Express," inaeleza taarifa hiyo. Pia, taarifa hiyo ilieleza kuwa imebainika Kampuni ya Dar Express imekiuka Kanuni namba 22 ya Kanuni za Ufundi na Usalama na Ubora wa Huduma kwa Magari ya Abiria za 2008.

"
Kuanzia Januari 2011 hadi sasa, mabasi ya Kampuni ya Dar Express yamehusika katika matukio ya ajali maeneo mbalimbali ambayo kampuni hiyo inatoa huduma za usafirishaji abiria. Matukio hayo ni kama lile la Januari 4, mwaka huu basi la Dar Express lilimgonga mpanda pikipiki na kusababisha kifo maeneo ya Kifaru- Mwanga, mkoani Kilimanjaro. Kwa mujibu wa taarifa za polisi chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi," ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza pia kuwa Septemba 22, mwaka huu, basi la Dar Express likitokea Arusha kwenda Tanga lilimgonga mtembea kwa miguu Ramadhani Hassan na kusababisha kifo eneo la Mkumbara - Mombo na Oktoba 24, basi jingine la kampuni hiyo liligonga gari jingine kwa nyuma kisha kuacha njia na kupinduka maeneo ya Kitumbi - Korogwe. Katika ajali hiyo watu tisa walijeruhiwa.

Mwananchi





Nikitafakari hapo kweye re nakumbuka MOHAMED TRANS, SUMRY, DELUX COACH, HOOD n.k
Naona kuna jambo LINAPIKWA ILA SIDHANI KAMA WANAJUA MOTO WANAOTAKA KUUWASHA WATAWEZA KUUZIMA......
SIJUI HAWA [h=3]JK ATOA SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA AJALI YA BASI LA ...[/h] WAMEFUNGIWA PIA????
 
hivi huyu muzachai anaongea nini apo juu.........mi dar express ni usafiri wangu na wa wapenzi wengi wa safari zisizo na mashaka..masaa 9-10 barabarani!!mwendo mzuri/muda wa kuchuma dawa/lunch nzuri nz sina record yeyote seriuos ya mabasi haya achilia mbali siku hizi ajali za kaskazini zimepungua...........

kuna mkono wa sumatra hapa.si bure. yani hii nji hii nimeichoka.........kil akukicha ni visa dawa yenu ipo njiani anakuja nayo cameron
tuache kutetea maovu. kugonga mtu kwa gari ni kosa. sema sheria au kisu hiki cha sumatra kipite kwenye mabasi yote. air msae tangu apigwe chini amejirekebisha sasa hivi ndio metro check huduma zake kwenye basi lake la luxury. kuna mabasi ya njia nyingi mbali mbali hayafai hata kidogo. kila mtu anayesafiri anayajua sipendi kuyataja. kila week yanapata ajali na hata magazetini na kwenye tv hayatajwi mpaka eti basi liue watu wengi. ni mara ngapi umepata habari basi limekanyaga mpita njia mmoja kwenye magazeti au vyombo vya habari vyote. ? ni mara chache sana ila basi likiua watu wengi ndo inakuwa stori ya kuuzia gazeti au vyombo vyote vya habari. Watanzania tubadilike akifa mtu mmoja kwa kugongwa na gari mtasema alikuwa mlevi, oh mara wengine watasema alikuwa chizi wala hakuna mtu atakae mnyooshea dereva kidole. wakifa wengi unakuwa msiba wa kitaifa na mtaji wa kisiasa kwa watu wengine

it is better to work hard during good time rather than in hard time."
 
Hii nchi tutakuja kumchinja afisa mmoja wa serkali hadharani we subiri, wanatuletea siasa kwenye utendaji, sasa hizo ndio ajali za kufungia mabasi hawa jamaa was........... nini?
 
Ndugu wasafiri wenzangu;

mara nyingi tunaposafiri safari ndefu tunashuhudia ajali nyingi sana barabarani za watu( wapita njia) kugongwa na mabasi ambapo baadhi hufa au kupewa vilema vya maisha. ajali hizi huwa hazipewi kipaumbele na polisi hata na media kwa ujumla huwa zinaishia hewani kwa matajiri na madereva kuonga mapolisi, ndugu wa mfiwa na watu wa media ili wasiandikwe vibaya. ila ikiwa ni ajali ya watu wengi unakuwa ndo mtaji wa media kuuza stori zao kwa kukosoa kila wanachoweza kusema tena huwekwa ukurasa wa mbele . vivyo sishangai watu kusifia baadhi ya mabasi wakati yanaongoza kwa kuuwa wapita kwa miguu bila sheria kali kuchukuliwa dhidi ya madereva na wamiliki wa magari. " KIFO CHA WENGI HARUSI" huu ndio msemo tunaoupenda watanzania maana hata viongozi wa ngazi za juu siku hiyo utawaona eneo la ajali inayoua watu wengi . akifa kwenye ajali mtu mmoja kazi hiyo ataachiwa mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wake. Tuache kasumba tupige vita ajali zote za barabarani iwe ya mtu mmoja au ya mamia ya watu.

"TANZANIA BILA AJALI INAWEZEKANA"
 
nauli zake haziendani na huduma wanazotoa. mfano kuna basi limepewa hadhi ya luxury na nauli ni shilingi 30,000 likiwa na maana ya full ac and tv. lakini ukilipanda neither tv nor ac. full vurugu. ticketi na namba ya basi ninayo kwa ushahidi hii ni fraud lakini watanzania huwa tunaona poa tu.

Hilo siyo linaloongelewa bwana, sababu ya kuwasimamisha wanasema ni ajali na siyo ubovu wa huduma au leo umelikoka zaidi??
 
Kuna kitu!!!!!!! mimi bora nipande Dar xpress kuliko hayo mengine.
 
Katika ajali tajwa hapo juu, vifo havifiki hata watu watatu kwa mabasi yote hayo.
But kila siku ni Mohammed Trans tu, likia wamepona sana zaidi ya 10,
Hapa kuna sababu zaidi ya hizo zilizotajwa.
Rushwa na Fitna za kibiashara zimetumika hapo kuyafungia hayo mabasi.
Naskia mwenye nayo ni mlokole, may be mgumu kukata kitu kidogo ndio wanamkomoa!!!
 
kumbe ajali zenyewe ni hizo...??kazi ipo kwa tz na kweli ipo kazi...Kisa kaleta Benzi za bei ghali na ndiyo maana wamenza fitina....inawezekana kwa tz ila sisi watz si vipofu tena...
 
Tunasubiri yafunguliwe mkombozi wa usafiri dasemba hapandishi nauli hata senti! Haunt anaemkaribia kwa ubora wa huduma. Hajali kama gari imepita nusu, anaheshimu abiria wachache aliopata na kuwahudumia ipasavyo kwa ufasaha na muda, pia kero zao nichache sana ukilinganisha na mabasi mengine
 
Nasikia kuna kampuni mpya ya yule kijana anapigiwa kelele na uvccm inaanzishwa. Pengine ndiyo mkakati sasa wa kuifungia Dar Express ili katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka watu watengeneze pesa! Dar Express imeleta mageuzi makubwa ktk makapuni ya usafirishaji abiria kanda ya kaskazini. Kwa kuiga mfano wa huduma nzuri na mabasi ya kisasa,kampuni nyingi zimebadilika sana na ajali za mabasi zimepungua sana ktk kanda ya kaskazini. Sasa kama imefungiwa,basi hakuna kampuni ya mabasi inafaa kusafirisha abiria ktk Tanzania.

Nakubaliana nawe mkuu. Yaani wakati mwingine wenye mamlaka huwa wanafanya ujinga ambao uko wazi kwa kila mtu. Na viongozi wetu hawana hata chembe ya aibu kwa huu uovu wao. Huu ni uonevu wa waziwazi kabisa uliofanywa kwa DAr Express na hapa ni wazi kuna mkono wa mtu. Kiila ninaposafiri kwenda Arusha huwa sipandi Bus lingine zaidi ya DAR Express baada ya Scandinavia kufilisika. Hapa inabidi wananchi tupige kelele kwa nguvu zote na tuseme hatuna imani tena na SUMATRA.
 
Sasa desemba tutaendake makwetu???washenzi hawa wamemlia timing wanaona krismasi inakaribia eti wamemfungia maana ndo wakati wa kutengeneza mshiko zaidi huo......

Hii si bure kuna kaufisadi kametendeka hapo.....wanamuonea tu mzee wa watu wivu kisa anamudu biashara yake vizuri au kwa sababu analeta mercedez benz ya mabasi inakuwa tabu???

Na huyo anayetaka kuanzisha route yake mpya hajipendi kabisa maana wananchi wa upande huo hawataki utani mambo ya siasa na huduma ni vitu viwili tofauti huezi mpindua dar express kwa rushwa za kijinga utegemee utachukua nafasi yake haitajakaa itokee wananchi hawatakubali na wachagga na waarusha walivyo wabishi bora aunge unge safari kuliko kupanda la huyo jamaa...............
 
inachekesha sana wanasema mti wenye matunda ndio hupigwa mawe,dar express wapo juusan alikuja scandnavia na mabasi yake lakini alichemsha mwenyewe kwa dar express ,hood,abood,sumry,delux,mohd trans kila kukich wanaua nguvu ya taifa kwa kafara zao,lakini yote `REHEMA ZA MUNGU ZIKO PALEPALE , KILA GOTI LITAPIGWA UKWELI UNAJULIKANA KWA KILA NAFSI` malipo ni hapa hapa duniani Mzee Mremi tupo pamoja nawe big up.
 
kama mtindo wa record za ajali ndiyo huo hakuna kampuni yeyote itakayokuwa njiani maana kwa wastani kila campuni ndani ya miezi mitatu kuna ajali zaidi ya moja.aibu kwenu sumatra kwa kuwaacha wauwaji na kuangaika na kampuni smart kama hiyo.
 
Lazima kutakuwa na kitu kimejificha sio bure. Nadhani hii kampuni ni miongoni mwa kampuni makini za mabasi TZ.
 
rushwa rushwa tu, utafungaje kampuni kubwa kama hii bila kupewa haki ya kusikilizwa?
wamewafanyia testing madereva wao na magari wakaona hayafai?
kumgonga mtu au pikipiiki hawajatueleza uzembe wa nani mwendo kasi pekee sio hoja ya msingi
yawezekana hao waliogongwa walikuwa na makosa na kama wasingegongwa wangesababisha ajali kubwa ilikuwa
njia ya kuokoa abiria, nadhani wafungue kesi mara moja kwa certficcate of urgency kupinga hiyo order mahakama
ina uwezo wa kubatilisha hiyo order na kuitamka kama ni batili isiyojali maslahi ya kibiashara na isioyozingatia hasara atakayopata mwendeshaji
pia mahakama inaweza kutengua hiyo sheria kandamizi ya SUMATRA.
BILA HIVO WAFANYABIASHARA WATAONEWA KWA UJINGA KAMA HUU.
 
Wameifungia Dar Express ila kwa Yesu Kila Goti LItapigwa. We waache tu.
 
Back
Top Bottom