SUMATRA: Marufuku abiria kuzungumza siasa, dini, biashara ndani ya basi!

Kuna laana imeikumba Africa. Inatafuna taifa Moja baada ya jingine. Tz zamu yetu..ila laana uwa inaingia kupitia mlango / upenyo kutoka kwa chochote/mtu/watu walio na influence ktk taifa. Laana hiyo yabidi aliyeiruhusu afe au atengwe au aondolewe kwenye ngazi hiyo yenye influence La sivo tutaumia Sana. Mnaodhani mko salama, jichunguzeni.. mwenye akili hufikiria with an open mind. Think twice.
Mungu atusaidie.
 
Kuna aliwahi kusema JPM anahujumiwa tukambishia sana.... Lakini kwa kauli kama hii... JPM anahujumiwa aisee.... Maana hii inasomeka hivi... SERIKALI YAPIGA MARUFUKU....... habar ya sumatra baadae....

Si yeye ndie anawapigia simu kuwapa muongozo, Mpango alikili bungeni sasa sie wananzengo tumkamate nani umbwa au mwenye Umbwa we mwenyewe fikiri. au "Ikikutwa bhangi shambani kwako ni yako, ikikutwa dhahabu ni mali ya serikali"
 
Yaani huyu bwana ngeve amekuwa wa ajabu. Anajua kwenye vyombo hivi kuna kuna tivi na radio ambazo hueaburudisha wasafiri kwa nyimbo za dini na muvi mbalimbali. Kweli ameshikiwa akili. Tatizo gani lilitokea kwa watu kuzungumzia siasa au dini wawapo safarini? Yeye kamamtaalam anaweza akaweka taarifa ya madhara ya kuingea dini na siasa abiria wawapo safari? Kweli anadhalilisha elimu yakr afadhari arudi Kidegambie Lupembe kula numbu.
 
Leo nimepanda basi kutoka Mwanza hapo stendi ya Buzuruga, basi nililopanda ni Musoma express nikiwa ndani ya basi ndio linataka kuanza safari Mara kondakta akasimama anasema namnukuu "jamani abiria hamjambo? Nawaombeni sana tumezuiwa kuwaruhusu abiria kuongelea mambo ya siasa, dini nakadhaka hivyo pigeni stori zozote ila sio kuhusiana na siasa" mwisho wa kumnukuu, sasa mi nawaza tu hii hali itakuwaje huko mbele daaah sina hamu na Serikali hii ya mihemko.
 
DAB atuandalie mijadala kwenye mabasi ama watupe colgate ma piPi maana midomo itanuka*
Watuandalie mijadala ya viwonder
 
Tatizo ni pale kila agizo likitolewa na serikali watu wanachukulia kisiasa kwanza hapo ndo tunafeli kwenye bus kuna watu tofauti wa dini na vyama mabishano yoyote ni kelo kwa wangine. Unakuta kwenye bus mch anahubili huku mwingine anatangaza biashara yake abilia wanbishana siasa hii haikubaliki.
Nasisi tunaokaa karibu ya misikiti? Hawa huanza saa tisa na nusu alfajiri kero yao ni kubwa kuliko mahubiri ya ndani ya basi.
 
Kuna jamaa yangu sahvi Yuko safarini mbeya anasema wao sahv wanapiga toli za kugegedna tu Mpk mwisho wa safari

Ova
 
Kweli mnafikiria kwa kutumia masaburi, kwa hiyo mnatupangia cha kuongea?? Yaani natoka kigoma saa 12 asbh nafika dar kesho yake saa 5/asbh masaa 29 nisiongee? Au ndo tuwe tunatongozana tuu! Hivi mbona viongoz wa inchi maskini wana matamko yasiyoeleweka kabisa! Mamaee.. Zenu
 

=======

MAMLAKA YA Usimamizi wausafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) imepiga marufuku abiria kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya biashara wawapo safarini.

Agizo hilo limetangazwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Lingadi Ngewe na kwamba abiria atakayebainika kufanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Agizo hilo linakuja baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwapo kwa mvutano wa kupinga kanuni mpya kati ya Sumatra na chama cha wamiliki mabasi yaendayo mikoani (TABOA) na wa usafiri Dar es Salaam (UWAMADAR).

Bila kutaja ni sheria na kanuni ipi, Mkurugenzi huyo amesema ufanyaji wa vitendo hivyo katika mabasi ni kinyume na kanuni za usafirishaji.

"Tutaanza kuzuia wasafiri wa wapo ndani ya mabasi kuacha kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya biashara. Tukibaini hilo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa abiria na dereva ikibidi," amesema na kuongeza

‘Kwa madereva hasa wa kwenda mikoani, njiani wanapandisha wafanyabiashara na kufanya biashara ndani ya basi, hatua kali zitachukuliwa kwa dereva na huyo anayefanya biashara.’

aah kwa vile mwisho chumbe sawa tu
 
Naomba kupatiwa MWONGOZO. Hivi kikundi fulani cha DINI wakikodi basi, humo ndani wasiimbe Kaswida, nyimbo na mapambio?
 
Back
Top Bottom