Bila tahadhari huu mkanganyiko kuhusu Muungano wetu unaweza kuwa kichocheo cha machafuko

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,099
22,827
Kabla ya Muungano mwaka 1964, kulikuwa na nchi mbili zilizojulikana kama Jamhuri ya Tanganyika ikiongozwa na Rais Julius K Nyerere na Jamhuri ya Zanzibar ikiongozwa na Rais Abeid A. Karume,

Chama kilichounda serikali ya Tanganyika kilikuwa ni Tanganyika African National Union Party, TANU. Hivyo hivyo chama kilichounda serikali ya Mapinduzi Zanzibar kilikuwa ni Afro-Shirazi Party, ASP.

Baada ya Muunngano huo, makubaliano yaliyofikiwa na hao viongozi wawili ni kuwa Rais wa Tanganyika ndio awe Rais na Rais wa Zanzibar awe makamu wake wa kwanza.

Jamhuri mpya iliyoundwa ikajulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na baada ya miezi sita ikafupishwa na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwaka 1965, Tanzania iliingia katika mfumo wa chama kimoja na kwa njia hiyo vyama vya TANU na ASP vikashika hatamu kama vyama pekee tawala Tanzania bara na Tanzania Visiwani.

Mwaka 1977 muungano mwingine ukatokea nchini Tanzania wa kuunganisha hivi vyama viwili na na kuasisi Chama cha Mapinduzi, CCM. TANU na ASP vikafutika na hadi leo ni historia.

TANU ilipotea na ASP ilipotea lakini cha ajabuTanganyika tu ikapotea lakini Zanzibar ikabaki! Hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari aliyelalamikia wala kuuliza kulikoni?

Linalozua tafrani isiyo na jibu ni vipi chama kimoja cha CCM kikaweza kuunda serikali mbili ndani ya Jamhuri moja! Kama huu sio uhuni ni kitu gani? Watanzania tulikubalije uhuni huu?

Naam, kwa miaka kumi na mitano hadi 1992 ikawa CCM. CCM, CCM tu. Kila kitu kikahodhiwa na CCM kuanzia Katiba, Serikali, Bunge na vyombo vyote vya dola. CCM ikawa kama dini!

Kuipinga, kuilaumu na kuikosoa vyote kwa pamoja vikaitwa uchochezi. Utaifa ukahusishwa na CCM, uzalendo ukahusishwa na CCM. Haki na usawa vyote vikawa kwa fadhila ya CCM.

This is craziness...
 
Huu muungano ata kama unakula mjani wa kule Kisimiri hauwezi uelewa
Kuna vitu vya kisanii vitayeyuka kama barafu siku CCM ikitoka madarakani
1. Muungano
2. Mbio za mwenge
3. Mikataba ya hovyo
 
Huu upumbavu unaoitwa muungano hauna faida yoyote kwa nchi yetu ya Tanganyika zaidi ni hasara tuu, unapaswa kuvunjwa kila mmoja abaki na yake watanganyika warudi nyumbani na hawa nyambilisi wasiokua na visogo warudi kwao
 
Inafaa tuchague moja kati ya haya matatu:-
1. Serikali 3
2. Serikali 1
3. Talaka

Nje ya hapo ni kudanganyana tu na kuendeleza kwa shuruti kisichowezekana.
Serikali 2 zimeshindwa kukidhi haja
Yeyote anayeutetea huu muungano kama ulivyo ni adui mkubwa wa Watanganyika. Watu milioni mbili kuburuza watu milioni sitini na wao wakakubali ni uhayawani,
 
VUNJILIA MBALI KILA NCHI IENDE KIVYAKE KULIKO KUDANGANYANA HUKU CHINI KWA CHINI HAKUNA ANAYETAKA HUU UPUMBAVU
Linalozua tafrani isiyo na jibu ni vipi chama kimoja cha CCM kikaweza kuunda serikali mbili ndani ya Jamhuri moja! Kama huu sio uhuni ni kitu gani? Watanganyika tulikubalije uhuni huu?
 
Rasimu ya Warioba irudi mezani, yafanyike marekebisho kidogo, hatimaye tupate tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Mungu ibariki Tanganyika.

Mungu ibariki Zanzibar,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amen
 
Lisu anaakili sana

Dr slaa na ajenda ya ufisadi na katiba mpya -chini ya chadema

Dr Tundu antpas Lisu _alichofanya ni kinyume ila kilekile katafuta kichocheo -MUUNGANO na UUzwaji Mali za nchi kiholela (Ufisadi) ,twende na LISU
 
Back
Top Bottom