Sultani Jamsheed hakukana kiti cha Usultani wa Zanzibar

naomba kuuliza, Hivi Jemshid hakuukana usultani Zanzibar, Vipi malkia wa Uiengerza alikana himaya yake kule USA? ikiwa anataka kuendeleza himaya USA, itakubalika?

Mimi huwa napenda kusoma habari, lakini chache sana huwa naziamini, hivi kufanya master yako kwa kutegemea vitabu (siasa) halafu ujisifu kuwa eti mimi ninajuwa, ndio unajuwa kulingana na kitabu, sio kwa kweli hasa, hebu kasome tena na pitia kwa Mazrui, yule wa Oxford atakupa zaidi

Kufanya dissertation kwa kutumia vitabu, articles, na data ndio kunakuwezesha kuzungumza jambo kwa uhakika na sio kuzua zua mambo tu. Sio kukaa vijiweni ambako mtu anaropoka tu halafu kila mtu anaamini. Umuhimu wa kuwa na reference ni kulinda academic integrity ya mtu kwasababu hawa jamaa walileta contribution katika literature ambayo imenufaisha jamii amasivyo narudia ule msemo wa economist wanasema No research no right to speak!!!!
 
Mdondoaji; unapenda serikali ya Zanzibar ya mseto irudi kama ilivyokuwa wakati wa Uhuru wa Zanzibar na kumrejeshea Sultani cheo chake cha heshima?
 
Hivi huyo Sultan atakuwa na nafasi gani katika JMT? Si ndipo atakapoambiwa kuwa yeye ni kama Chifu wa huku kwetu itakuwa kero nyingine ya Muungano!

Amandla......
 
unajua sidhani kama Sultani anataka kurudi au hata anaweza kurudi akipewa nafasi. Tatizo langu ni kuwa hata kama yeye Jamsheed hawezi kurudi watoto wake watapenda kurudi siku moja. Akifa Jamsheed, kuna atakayemrithi... sasa sijui atamrithi kama Sultani wa Zanzibar (ambayo haipo) au atamrithi tu kwa jina au vipi.

Sasa huyo atakaye mrithi akiamua kurudi Zanzibar nyumbani kwake nani anamkataza? Hivi, kwa mfano hata Jamsheed akiamua kuja Dar.. akatua uwanjani pale tutamfukuza? Na akiamua kupanda ndege kwenda Zanzibar hata kwa matembezi tu kuwasilimia watu alioishi nao n.k Zanzibar kutakalika?
 
Zanzibar ni mali yake?
Anaweza dai alinunua kisiwa hicho kwa kipande kirefu sana cha nguo, je thamani ya Wazanzibar waliokuwemo humo kisiwani ni shilingi ngapi??.
.
Kisiwa kilichonunuliwa kwa kipande cha nguo kilichozunguka kisiwa hicho ni Kilwa, sio Zanzibar, hapo angalau Sultan wa Kilwa, alilipa kitu, Sultan Said Said alipohamishia makao makuu yake toka Oman kuja Zanzibar 1822, hakulipa kitu, single cent hakutoa, tuseme ni kama alivamia, hoja ilikuwa eti Zanzibar, haikuwa na wenyewe!, hao wote weusi wote mnaowaona ni masalia ya watumwa waliokosa soko, na hao weupe, masalia ya waarabu, hao Washirazi na na point five, ni masalia ya intermariages kati ya mabwana wa kiarabu, na mabinti wa watumwa, waliokuwa vijakazi wao.

Soku kuu la watumwa wa Zanzibar lilikuwa Arabuni, soko kuu la watumwa wa West Afrika lilikuwa North Amerika, hebu shuhudieni kizazi cha watumwa wa Amerika ni African American, hebu jiulizeni kizazi cha watumwa waliopelekwa Arabuni.. masikini... wote walihasiwa!. Waarabu jamani.. waoneni hivi hivi...
Haya ya Mwanakijiji, yaoneni kama mzaha mzaha, subirini hiyo serikali ya umoja wa kitaifa, mtabaki mkishangaa!.
 
.
Zanzibar, haikuwa na wenyewe!, hao wote weusi wote mnaowaona ni masalia ya watumwa waliokosa soko, na hao weupe, masalia ya waarabu, hao Washirazi na na point five, ni masalia ya intermariages kati ya mabwana wa kiarabu, na mabinti wa watumwa, waliokuwa vijakazi wao.

QUOTE]

du hiyo kali ....yaani wale goi goi waliokusa soko...ndio hao wazanzibara...waliosalia wapwaa wao[yaani watoto ambao dada zao walizaa na waarab]...basi ndugu moja!!.....ila wakikuona watakupiga ngumi ya pua kwa kuwaita wao uzao wa makapi goi goi..[mdebedo]....
 
.
Kisiwa kilichonunuliwa kwa kipande cha nguo kilichozunguka kisiwa hicho ni Kilwa, sio Zanzibar, hapo angalau Sultan wa Kilwa, alilipa kitu, Sultan Said Said alipohamishia makao makuu yake toka Oman kuja Zanzibar 1822, hakulipa kitu, single cent hakutoa, tuseme ni kama alivamia, hoja ilikuwa eti Zanzibar, haikuwa na wenyewe!, hao wote weusi wote mnaowaona ni masalia ya watumwa waliokosa soko, na hao weupe, masalia ya waarabu, hao Washirazi na na point five, ni masalia ya intermariages kati ya mabwana wa kiarabu, na mabinti wa watumwa, waliokuwa vijakazi wao.

Soku kuu la watumwa wa Zanzibar lilikuwa Arabuni, soko kuu la watumwa wa West Afrika lilikuwa North Amerika, hebu shuhudieni kizazi cha watumwa wa Amerika ni African American, hebu jiulizeni kizazi cha watumwa waliopelekwa Arabuni.. masikini... wote walihasiwa!. Waarabu jamani.. waoneni hivi hivi...
Haya ya Mwanakijiji, yaoneni kama mzaha mzaha, subirini hiyo serikali ya umoja wa kitaifa, mtabaki mkishangaa!.

Thank God Pasco wewe si miongoni mwa wazanzibar ijapokuwa umekuwa kimbelele kujishauwa na kujipendekeza kwa Wazanzibar kwa sababu fulani fulani unakwenu ijapokuwa hutaki kukusikia , wazanzibar hawajawahi kukukana kwao juu ya shida zote na mnisukosuko wanayokumbana nayo, kutokea 1977 kunganishwa vyama vya ASP na TANU pale ndio watanganyika walipopata mwanyakuwa waongezi sana kuhusu zanzibar ,kabla ya hapo ilikuwa heshima ,na hiyo sasa ndio imo njiani kurejeshwa .
 
inahitajika somo ili kumjua vizuri huyu jamsheed, lakini siamini kama ana nguuv kiivyo katika enzi hii. walikuwepo machif na watemi na wamangi. wako wapi? uganda kuna mfalme, nguvu zake kisiasa ziko wapi? wazanzibar wakiamua kutaka kurudisha ufalme watakuwa na majuha wasiojua wanataka nini.
 
Mdondoaji; unapenda serikali ya Zanzibar ya mseto irudi kama ilivyokuwa wakati wa Uhuru wa Zanzibar na kumrejeshea Sultani cheo chake cha heshima?

MwanaKijiji,

Hakuna anayekutisha isipokuwa kwa mtu mwerevu kama wewe ambaye tunakusoma na kujifunza mengi kutoka kwako unapokuwa irresponsible lazima tukwambie. Inaonesha unatishwa sana kwa hiyo lolote linalokujia unadhani ni vitisho tu. Hapana ni mijadala na wakati mwingine ukubali unapokuwa wrong. Hapa upo wrong na kwa kiasi kikubwa historia yako kuhusu Zanzibar imejengwa na prejudices mbaya. Get out of that BOX and see things outside your own kachumba. Soma, soma na soma tena. Soma hata usiyoyapenda na unayoyaona ya kijinga utapata kitu.

Serikali ya mseto (ndio coalition) ya wakati wa uhuru sio aina ya serikali inayotaka kuundwa sasa kati ya CCM na CUF huko Zanzibar. Baada ya uhuru Zanzibar ilifuata demokrasia ya magharibi ambapo Bunge liliundwa na vyama vitatu ASP, ZNP na ZPPP. Hapakuwa na chama kilichoweza kuunda serikali peke yake kwani hawakuwa na wabunge wa kutosha. Hivyo chama kidogo kabisa kikawa decisive na ndiyo Shamte akaunda serikali kama Waziri Mkuu na Mkuu wa Serikali na Karume alikuwa Leader of the Opposition. Muundo wa Serikali ile ni kama ilivyo Danmark leo, Sweden, Portugal na itakuwa hivyo UK baada ya uchaguzi wa Mei kama vyama vikiendelea kuwa na halib ya sasa ya kukubalika ambapo kutakuwa na hung parliament. Kulikuwa na third party balancing two big parties.

Sasa hao mabwana wakubwa wa CUF na CCM wanataka kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ambapo hapatakuwa na upinzani Bungeni kwao kitu ambacho pia ni hatari kwa demokrasia.

Marehemu Babu alitaka a third force. Hii ndio ingeimarisha demokrasia Zanzibar kwani hata iwe nini hakuna chama kingeweza kuunda serikali peke yake.

Unaendeleza kupotosha unaposema mdondoaji anataka serikali ya mseto iliyokuwepo wakati wa uhru na kumrudisha Sultan. Bado unacheza ngoma ya CCM ya propaganda kali na mbaya dhidi ya Zanzibar na watu wake.
 
.
Kisiwa kilichonunuliwa kwa kipande cha nguo kilichozunguka kisiwa hicho ni Kilwa, sio Zanzibar, hapo angalau Sultan wa Kilwa, alilipa kitu, Sultan Said Said alipohamishia makao makuu yake toka Oman kuja Zanzibar 1822, hakulipa kitu, single cent hakutoa, tuseme ni kama alivamia, hoja ilikuwa eti Zanzibar, haikuwa na wenyewe!, hao wote weusi wote mnaowaona ni masalia ya watumwa waliokosa soko, na hao weupe, masalia ya waarabu, hao Washirazi na na point five, ni masalia ya intermariages kati ya mabwana wa kiarabu, na mabinti wa watumwa, waliokuwa vijakazi wao.

Soku kuu la watumwa wa Zanzibar lilikuwa Arabuni, soko kuu la watumwa wa West Afrika lilikuwa North Amerika, hebu shuhudieni kizazi cha watumwa wa Amerika ni African American, hebu jiulizeni kizazi cha watumwa waliopelekwa Arabuni.. masikini... wote walihasiwa!. Waarabu jamani.. waoneni hivi hivi...
Haya ya Mwanakijiji, yaoneni kama mzaha mzaha, subirini hiyo serikali ya umoja wa kitaifa, mtabaki mkishangaa!.

Pasco umewahi kujiuliza kizazi cha watumwa kilichopelekwa Argentina? Umewahi kumwona mtu mweusi Argentina? Chile?

You are too low on this. Kama hujaenda shule hivi maana sioni tofauti ya hoja unayojenga na hoja wanazojenga watu wa maskani pale Mchambawima
 
unajua sidhani kama Sultani anataka kurudi au hata anaweza kurudi akipewa nafasi. Tatizo langu ni kuwa hata kama yeye Jamsheed hawezi kurudi watoto wake watapenda kurudi siku moja. Akifa Jamsheed, kuna atakayemrithi... sasa sijui atamrithi kama Sultani wa Zanzibar (ambayo haipo) au atamrithi tu kwa jina au vipi.

Sasa huyo atakaye mrithi akiamua kurudi Zanzibar nyumbani kwake nani anamkataza? Hivi, kwa mfano hata Jamsheed akiamua kuja Dar.. akatua uwanjani pale tutamfukuza? Na akiamua kupanda ndege kwenda Zanzibar hata kwa matembezi tu kuwasilimia watu alioishi nao n.k Zanzibar kutakalika?

Jamshid ni Mzanzibari kama Wazanzibari wengine. Watoto wake kama hawajaukana Uzanzibari bado ni Wazanzibari na sioni sababu yeyote ya kuwazuia kurudi Zanzibar wakitaka. Walipunduliwa na Usultani kufutwa na hautarudi tena kwani Zanzibar ni Jamhuri ndigi chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama Kagame alivyomwambia aliyekuwa malme wa Rwanda kuwa ruksa kurudi Rwanda lakini huna ufalme wala uroyal family. Salmin alishamwambia Jamshid ruksa kurudi Zanzibar ila hakuna Usultani.

Whats a big deal?
 
Muungano hakuna mtu anautaka kama nyie mmeuchoka zanzibar ndio kabisa wazanzibar hawataki hata kuusikia basi tu ni CCM ndio inashikilia but mie sidhani kuuvunja ni busara la msingi ziwepo serikali tatu na muungano uwe shirikisho au jamhuri na sio hivi. Kila mmoja ajitegemee kivyake whether jamshid amerudi, queen elizabeth ii, babu amerudi zanzibar inachotaka ni maendeleo watu wamechoka!!!! Hatuhitaji sympathy ya mtu tunalolisema ni ukweli tu

Hakuna mtu anayeutaka muungano kakwambia nani? Umepima vipi au ndio sweeping statements tu za maadui wa muugano.

Mimi nautaka muungano na nipo tayari kufa mstari wa mbele kuulinda na kuutetea muungano. Kama wewe huutaki ni wewe peke yako. Tupo ambao hatutakaa kuona maadui wa umoja wa afrika wanavunja alama hii pekee ya umoja wa afrika
 
unajua sidhani kama Sultani anataka kurudi au hata anaweza kurudi akipewa nafasi. Tatizo langu ni kuwa hata kama yeye Jamsheed hawezi kurudi watoto wake watapenda kurudi siku moja. Akifa Jamsheed, kuna atakayemrithi... sasa sijui atamrithi kama Sultani wa Zanzibar (ambayo haipo) au atamrithi tu kwa jina au vipi.

Sasa huyo atakaye mrithi akiamua kurudi Zanzibar nyumbani kwake nani anamkataza? Hivi, kwa mfano hata Jamsheed akiamua kuja Dar.. akatua uwanjani pale tutamfukuza? Na akiamua kupanda ndege kwenda Zanzibar hata kwa matembezi tu kuwasilimia watu alioishi nao n.k Zanzibar kutakalika?
Kurudi kama sultani, KATIBA INAMKATAZA.
kurudi kama mzanzibari kuja kutembea kwao anakaribishwa (hata komandoo Salmin Amour aliwahi kumkaribisha jamsheed na familia yake kuja kutembea Zanzibar kwenye mkutano wake wa hadhara)
 
Pasco umewahi kujiuliza kizazi cha watumwa kilichopelekwa Argentina? Umewahi kumwona mtu mweusi Argentina? Chile?

You are too low on this. Kama hujaenda shule hivi maana sioni tofauti ya hoja unayojenga na hoja wanazojenga watu wa maskani pale Mchambawima
.
Bingilankana, mbona mimi nimetoa facts za issue ndogo tuu, no African Arabs kwa vile Waarabu waliwahasi watumwa, wakati African Americans wapo.

Nakubali I'm too low on this. Pia sijaenda shule, ila nimefuta tuu ujinga kwa kujua kusoma na kuandika. Kwenye kujenga hoja mimi ni mtu wa maskani ila siyo ya pale Mchambawima, ni maskani ya Kibandamaiti.

Kwa vile JF, ni mahali pa kuelimishana, nakiri sikijui kilichowapata watumwa waliopelekwa Ajentina na Chile, na sijawaona watu weusi huko, jee nao waliwafanya kama walichofanyiwa mababu zetu na Waarabu?.
 
Pasco umewahi kujiuliza kizazi cha watumwa kilichopelekwa Argentina? Umewahi kumwona mtu mweusi Argentina? Chile?

You are too low on this. Kama hujaenda shule hivi maana sioni tofauti ya hoja unayojenga na hoja wanazojenga watu wa maskani pale Mchambawima

Kibao! Angalia timu zao za mpira. Hakuna nchi ya Marekani kusini isiyokuwa na weusi. Na wanatambuliwa hivyo.

Uarabuni weusi wapo lakini wao wanajitambua kama waarabu. Hata India weusi wapo. Kote huko hawa wamekubali kuwa second class waarabu au wahindi na hawaenzi weusi wao. Hii ni tofauti na Marekani na Ulaya. Ukiangalia Janjaweed, wengi hawana tofauti kubwa na hao wanaowaita watwana isipokuwa pengine babu zao walikuwa waarabu! Kwa waarabu, mwenye damu ya muarabu ni muarabu lakini kwa wazungu mwenye damu nyeusi ni mweusi! Pengine Obama mama yake angekuwa muarabu angekuwa muarabu!

Amandla......
 
Hakuna mtu anayeutaka muungano kakwambia nani? Umepima vipi au ndio sweeping statements tu za maadui wa muugano.

Mimi nautaka muungano na nipo tayari kufa mstari wa mbele kuulinda na kuutetea muungano. Kama wewe huutaki ni wewe peke yako. Tupo ambao hatutakaa kuona maadui wa umoja wa afrika wanavunja alama hii pekee ya umoja wa afrika

Good for you! Nadhani uko peke yako znz Nipe sababu tano za kwanini wewe muungano unaoutaka na mie nitakupa sababu kumi kwanini siutaki. Unadhani kuvaa vizuri na tai shingoni wakati nyumbani kwako pana nuka njaaa ndio sahihi!!!
 
Mnao wajadili ni hawa au
 
Attachments

  • Sultans zanzibar.jpg
    Sultans zanzibar.jpg
    76 KB · Views: 72
Jamshid ni Mzanzibari kama Wazanzibari wengine. Watoto wake kama hawajaukana Uzanzibari bado ni Wazanzibari na sioni sababu yeyote ya kuwazuia kurudi Zanzibar wakitaka. Walipunduliwa na Usultani kufutwa na hautarudi tena kwani Zanzibar ni Jamhuri ndigi chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama Kagame alivyomwambia aliyekuwa malme wa Rwanda kuwa ruksa kurudi Rwanda lakini huna ufalme wala uroyal family. Salmin alishamwambia Jamshid ruksa kurudi Zanzibar ila hakuna Usultani.

Whats a big deal?

Hawezi kurudi kama Mzanzibari tu! anajitambua yeye ni Sultani na uzao wake unajitambua hivyo. Angekuwa na nia ya kurudi kama Mzanzibari angesharudi na familia yake.
 
Kibao! Angalia timu zao za mpira. Hakuna nchi ya Marekani kusini isiyokuwa na weusi. Na wanatambuliwa hivyo.

Uarabuni weusi wapo lakini wao wanajitambua kama waarabu. Hata India weusi wapo. Kote huko hawa wamekubali kuwa second class waarabu au wahindi na hawaenzi weusi wao. Hii ni tofauti na Marekani na Ulaya. Ukiangalia Janjaweed, wengi hawana tofauti kubwa na hao wanaowaita watwana isipokuwa pengine babu zao walikuwa waarabu! Kwa waarabu, mwenye damu ya muarabu ni muarabu lakini kwa wazungu mwenye damu nyeusi ni mweusi! Pengine Obama mama yake angekuwa muarabu angekuwa muarabu!

Amandla......

Nitajie mchezaji mmoja mweusi wa Argentina. Mmoja tu. Kilichowapata watu weusi huko hakisumiliki......
 
Back
Top Bottom