Sugu awatukana waandaaji wa fiesta kwenye facebook

Sugu yuko sahihi kabisa. Hawa Jamaa wanatumia jasho la wasanii kujinufaisha na kutembea vifua mbele.
 
Kwa mtaji wa wasanii hawa lazima clouds wawatie dole hawa wasanii....
 
Last edited by a moderator:
Na kuna habari za wadaku kama hizi

KINGKAPITA: MMBUNGE WA MBEYA AKA SUGU RUMANDE MPAKA FIESTA IPITE!!

JAFFARAI AMLIPUA SUGU KUHUSU FIESTA MBEYA (Hassbaby's (Mapacha))
Jaffarai amemlipua Sugu baada ya kauli yake ya kukataa kufanyika Fiesta mkoani mwake sasa jaffarai amjibu na kumwambia si kweli kwamba wakazi wa Mbeya hawaitaki yeye mwenyewe alisoma Mbeya na kitovu cha Hip Hop kipo Mbeya, funguka zaidi Hassbaby's (Mapacha)



Yetu macho, wababe wawili wakikumbana sie wanyonge tuko pembeni tukiangalia mshindi
 
Na kuna habari za wadaku kama hizi

KINGKAPITA: MMBUNGE WA MBEYA AKA SUGU RUMANDE MPAKA FIESTA IPITE!!

JAFFARAI AMLIPUA SUGU KUHUSU FIESTA MBEYA (Hassbaby's (Mapacha))
Jaffarai amemlipua Sugu baada ya kauli yake ya kukataa kufanyika Fiesta mkoani mwake sasa jaffarai amjibu na kumwambia si kweli kwamba wakazi wa Mbeya hawaitaki yeye mwenyewe alisoma Mbeya na kitovu cha Hip Hop kipo Mbeya, funguka zaidi Hassbaby's (Mapacha)



Yetu macho, wababe wawili wakikumbana sie wanyonge tuko pembeni tukiangalia mshindi
 
CHADEMA is led by a mobster Mboye, no wonder the surbodinates copy their prexy's ways. Mboye has yet to enoxerate himself from allegations that he is an infamous marijuana smoker. Imagine in the future having these type of hooligans acting as our ministers, this should never happen during my life time. I am not stupified when I see these 'leaders' coax desperate youths into deluging streets, doing vandalism under the umbrella of peaceful demonstrations.

You even don't know the name of CHADEMA leader! Those, who are not hooligans led us to this life we are lliving, you should regret for the life you are living now! I wish you would live the future life, full of INDEPENDECE AND SUCCESS! Magambazzzzzzzzzzzzzzz!
 
Hapa ndipo ule usemi wa ukipenda sana hata chongo utaona kengeza.
Sugu unamambo mengi sana na ya msingi kwa wananchi wako more than ur personal conflicts na clouds
 
Bangi mbaya sana:haya anayoyafanya sugu ni ushahidi wa waziwaziwa bangi
 
Kwa Mtazamo wangu ni bora alichoongea SUGU kuliko upumbavu wa huyu Mzee anayekwenda kwa jina la John Shibuda manake ni mpuuzi wa kutupwa......Sasa walichofanya Clouds ni sawa Kutumia Video ya Sugu? Msitete upuuzi humu kila mtu ana haki ya kuongea sehemu yoyote ila ki ukweli Clouds mi nishawachoka tu....Radio imejaa Mashoga kila kona. Na wewe unayetaka kuhama CDM kwa maneno ya sugu hama tu hukuitwa nenda katafute mabwana sehemu ingine kwanza vyama viko vingi unataka kuchukua reference ya maneno ya sugu kuhama chama hama. CDM haina wanafiki kama wewe.....Aluta Continua.
 
wakuu hata kama hiyo clip ni ya zamani lakini ukweli unabaki pale pale kwamba at one point in time aliiunga fiesta mkono na aliishabikia. Swali la kujiuliza ni kwa nini aliisaport fiesta then and why not now? au ni kwa vile ana ugomvi binafsi na ruge ndio maana amegeuza kibao? Mhe Mbilinyi siyo mkweli hata kidogo kwani hivi sasa ameanzisha hii movement kwa maslahi yake binafsi na kuwahadaa wananchi kwamba ana uchungu na wasanii wenzake. Hivi hao wasanii aliyowapeleka mbeya yeye amewalipa shillingi ngapi? sawa tunaweza kuwalaumu sana clouds kwamba wanawanyonya wasanii lakini ukweli lazima tuseme kwamba sugu hakuwa na nia ya kuwasaida wasanii kutoka moyoni mwake.

Ukweli ulio wazi ni kuwa anataka kugrab hii opportunity ya kuwasaidia wasanii ili apate public sympathy lakini akae akijua kwamba anaweza kuwahadaa wananchi kwa kipindi cha muda mfupi na baada ya muda ukweli utakuwa wazi. Clouds pamoja na mabaya yote sugu aliyoeleza juu yao lakini bado wanafanya kazi nzuri ya kuwapa changamoto wasanii watunge nyimbo nzuri ili zipigwe kwenye radio yao! na kusema ukweli wasanii wengi tu wamekuwa wanajitahidi kufanya hivyo ili watoe nyimbo nzuri. Lakini utakuta wakongwe wa muziki kama sugu, afande sele, danni msimamo, g solo, mkoloni wamekuwa wakiijifanya wanajua sana mziki na matokeo yake ngoma zao zimekuwa hazikubaliki na ndiyo maana zimekuwa hazipigwi clouds. Sasa hii ni hasira wanayotaka kuleta ili kuikomoa clouds lakini sidhani kama itasaidia lolote.

Nimeona interview yake akisema wahariri wa habari wamekuwa wakihongwa na clouds ili kuzima issue ya malaria na hii ni very serious allegation. Iwapo vyombo vya habari wakiona hii interview yake inaweza kumharibia na wakamgeuka mara moja. Pamoja na kwamba anadhani kwamba wanambeya wamemchagua kwa kura za kishindo lakini ni media ndiyo inaweza kumjenga au kumbomoa na akaishia pabaya sana. Hatakiwi hata kidogo kugombana na vyombo vya habari na hii ni soma si kwa nchini kwetu lakini dunia nzima. Tumeshuhudia viongozi wengi wakiangushwa na vyombo vya habari.

Status yake ya kwanza kwenye facebook alisema kwamba fiesta ni upuuzi na hawezi kukubali ifanyike mbeya kama sikosei aliapa kwamba haitafanyika mbeya. Hivi yeye ni nani mpaka aape kwamba fiesta haiwezi kufanyika mbeya? Leo hii ni mbunge tu na analeta vitisho kwani yote hiyo ni kujiamini kupita kiasi kwamba wapiga kura wake watampa support. Hapo ni kosa kubwa la kwanza alilofanya huyu mheshimiwa sana. Pamoja na kula kiapo tumeshuhudia fiesta ikifanyika mbeya bila ya tatizo lolote. Alitumia nafasi yake ya ubunge kufanya mkutano wa hadhara ili ahamasishe wakazi ya mbeya kuikataa fiesta na kibaya zaidi inasemekana hakuwa na kibali cha kufanya mkutano. Swali ninalojiuliza hivi je alifanya mkutano bila kibali kwa makusudi ili akamatwe na polisi na kuwekwa ndani ili apate public sympathy ya wakazi wa mbeya ili wafanye fujo? kosa kubwa ninaloliona kwa jeshi la polisi ni kumuweka ndani huyu mheshimiwa kwani bila ya hivyo issue hii isingepata headlines zozote alizokuwa anatarajia. Uzuri ni kwamba ametumia opportunity ya jeshi letu na pengine hata hakuwa na kibali tena kwa makusudi kabisa ili atimize malengo yake...all in all aliwekwa ndani na kisha akatolewa.

Taarifa yake kwa umma nimeisoma lakini sijaridhishwa nayo hata kidogo kwani imejaa ubabaishaji wa kutumia mgongo wa wasanii kitu ambacho si kweli hata kidogo. Ukweli ni kwamba sugu ni mtu mmoja hatari sana na tusipokuwa makini kuelewa dhamira yake tunaweza kujiingiza kwenye mtego ambao mwisho wa siku itakuwa mbaya sana. Mtu kama huyu inabidi kumuogopa sana na kuwa naye makini sana katika kile anachodai ni harakati zake za kukomboa wasanii.

kwa leo naomba niishie hapa lakini nasisitiza tena na tena tuwe makini sana na huyu mheshimiwa.

Kwani waandishi hawanunuliki? Kama wamenunuliwa acha awaseme, wao sio malaika, by the way news of the world uingereza chali hii inasuggest ama ina prove waandishi si malaika, to hell clouds wezi wa jasho la wasanii
 
Sugu namuunga mkono kwa kiasi kikubwa, yes, inaweza kuwa ni personal conflict lakini kwa vile keshapitia tatizo basi ameona njia sahihi ni kukabiliana nao kwa kuwapa maneno stahili, nadhani kuwaita wa.s.en ge na ma. sh.oga ni kuwa wanastahili kuitwa hivyo. hatuwezi kuendele kubembeleza u.senge. Kuhusu kuwa anafundisha nn vijana, rahisi, Anatueleza kuwa ukitia bidii katika kazi yako utafanikiwa na kamwe usiwape nafasi was. enge kama clouds &co wajitokeze mbele yako.
Namsikiliza Roma pia, kwa sasa tuna akili timamu na hatuhitaji tuzeeke ndo tujue haki zetu
 
Alichoandika mr 2 sugu kuhusu fiesta kwenye wall yake ya facebook



kama hii ndio chadema school of thought, muda si mrefu nitarudisha kadi niungane na mtikila.


Mods in jf tunasema "where we dare to talk openly"
so please if that is true then msiondoe hii thread.

Kama ungekuwa serious ungerudisha kadi kimya kimya. Hapa unafanya usanii wa kifiesta
 
Sugu ana sura 2 ktk jamii 1. Msanii 2. Mbunge
lakin kwa status aliyonayo no 2 hakutakiwa kutumia neno kali hvyo.

Hivi jamii ipi ya kipuuzi unayoizungumzia? Kuanzia Mkuu wa nchi hadi wafagiaji ni wasanii. Lugha sahihi inayoeleweka ni hiyo inabidi uvumilie.
 
Nimeiona kwa FB lkn sitaki kuamini kama kweli ni mheshimiwa katoa maneno yale maana hayakuhitajika asilani
 
Wanakuita sugu*3 (NANI)*2..sugu mtu wamavurugu palipo na dhuruma...nyie mnaoona Sugu amekosea hebu google Clintön vs Lewsky, Robin Hood..
 
Nahisi hapa tunazungumzia ushabiki kwa vikundi vya mziki na vyama.
Pengine Sugu angelikuwa SUGU tu kwenye fani yake, alichofanya kingekuwa sawa.
Lakini kama mbunge kijana, kioo cha vijana wengine, mtunga sheria, kama Mheshimiwa, hakupaswa kutukanana nao .
Angetumia, na bado nafasi anayo ya kutumia nafasi yake kama mbunge kupeleka mswada wa sheria bungeni kutetea haki za wasanii.
Ikiwa sheria tayari ipo na walichofanya hao wa walioandaa FIESTA ni kosa, adhabu yao nikiuwapeleka kwa Pilato na sio kurushiana maneno ya kashfa.
Je kama Clouds watarudisha mapigo ya kashfa, Mheshimiwa Sugu ataendelea kutukanana nao?
Iko siku nilitoa mfano wa mtu mwenye akili akiwa u.c.h.i kumfukuza mwendawazimu aliyemwibia nguo. Mheshimiwa Sugu asipokuwa makini, anaweza kupoteza heshima yake.
 
Back
Top Bottom