Subaru Forester Vs Mazda CX5

Hakika Tutafute Hela Kaka
Nje iyo design wao wanaiita Kodo design or Soul of Motion. Ilianza kwenye izo CX5 sahivi imesambaa kwenye lineup nzima ya Mazda.

Ndani wamechukua interior ya Mazda 6 (Atenza) za kuanzia 2016 aisee. Unyama sana .

View attachment 2938472

Mkuu, hii ni CX5 aisee. Sasa kuna vyuma vinaitwa CX50, CX9 na CX90.

Aisee tutafute hela sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio habari ya mjini Kwa wale wapenda magari mazuri

Hizi ni gari shindani kwa sababu zote zipo kundi moja la COMPACT SUV.

Zinafanana sifa katika utendaji kama vile:

1. Ukubwa wa umbo
2. Nafasi kubwa ndani
3. Ground clearance nzuri
4. Nguvu ya kutosha kustahimili
changamoto za barabara
ngumu

Baadhi ya Tofauti ambazo zinaweza kukusaidia kuchagua kati ya SUBARU FORESTER na MAZDA CX5 ni kama vile:
1. Muonekano, macho
yanatofautiana kila mtu ana
Upendeleo binafsi kati ya
Muonekano wa FORESTER na
MAZDA CX5

2. Matumizi ya mafuta, MAZDA
CX5 nyingi ni Diesel na
zinakwenda mpaka 18KM/L
wakati FORESTER ni Petrol na
zinakwenda 14KM/L. Kuhusu
utofauti wa injini ya Petrol na
Diesel unaweza kurejea somo
hilo lipo humu

3. Upatikanaji wa vifaa na
mafundi, Japo gari zote hazipo
kwa wingi sana, lakini subaru
ipo kwa wingi na hata vifaa ni
vingi na mafundi wapo wengi
pia kulinganisha na MAZDA
CX5

4. MAZDA CX5 zilizo nyingi ni
Non-Turbo lakini zinakuwa na
nguvu kubwa kuliko
FORESTER NON-TURBO (XS)
FORESTER XT inazalisha
nguvu kubwa zaidi kuliko
MAZDA NON-TURBO. Lakini
MAZDA CX5 TURBO inazalisha
nguvu kubwa kuizidi kidogo
FORESTER TURBO (XT)

5. Bajeti, MAZDA CX5 bajeti yake
ni kuanzia TSH 27M mpaka
TSH 30M wakati FORESTER
NEW MODEL zinaanzia TSH
25M mpaka TSH 28M lakini
pia FORESTER OLD MODEL
bajeti ni chini zaidi.

Bila shaka maelezo haya yanajitosheleza kukuwezesha kufanya Uchaguzi sahihi.

View attachment 2789002View attachment 2789003
Subaru ni 4x4 kawaida
Mazda ni FWD kawaida na 4WD kama uliorder. Si lazima ukaipata ya 4WD kwa second hand
 
Nina fundi wangu mmoja ninamkubali ila anasema engine za Mazda zina changamoto sana, toka zimeanza kuingia kwa wingi hizi Mazda anasema zimeletwa kwake zaidi ya nane kwa matatizo engine tena zote namba E'! Ni kweli au hao watumiaji hawana uelewa nazo.?
Watanzania sijui wapoje aisee. Yaani eneo la kuharibu magari wapo vizuri balaa.
 
Nje iyo design wao wanaiita Kodo design or Soul of Motion. Ilianza kwenye izo CX5 sahivi imesambaa kwenye lineup nzima ya Mazda.

Ndani wamechukua interior ya Mazda 6 (Atenza) za kuanzia 2016 aisee. Unyama sana .

View attachment 2938472

Mkuu, hii ni CX5 aisee. Sasa kuna vyuma vinaitwa CX50, CX9 na CX90.

Aisee tutafute hela sana.
Sijui nimekuaje siku hizi,gari zenye gear lever hata iwe Kali vipi Sina mzuka nazo,Basi tu ni maisha.Natamani wangeweka Kama za Jaguar XF,kitu unazungusha tu P,R,N,D kama redio vile.
 
Back
Top Bottom