Style mpya ya harusi: Mualikwa kufika ukumbini na pesa ya chakula na vinywaji

hapa shida naiona kwa wale ndugu wa pande Mbili ambao wao hata huwa awachangii mfano bibi pande zote mbili + mashangazi ma wengine huoni Kama huo mzigo bado upo juu ya mwenye harusi
Unaweza kuwatengea bajeti hao ndugu wachache cause am sure hawatokuwa wengi sana cause hutotaka kutumia gharama kubwa.
 
Vijijini mbona kawaida ndugu wanaleta mikungu ya nk kwa ajili ya harusi mwingine kuku mbuzi nk Anzeni kufanya harusi vijijini mlikozaliwa .Unakuta harusi imejaa magari na wavaa masuti ya bei unajiuliza hii familia wote matajiri kumbe wafanyakazi wenzie na marafiki zake.Ndugu waweza kuwa hawafiki hata kumi hawafiki wamejaa mapedeshee mashoga na wahuni wa mjini .Nimehudhuria harusi wakisema wababa wa bwana harusi wasimame wanasimama watu wa uhakika nikauliza wale ndio baba zake nikaambiwa wale ni baba zake wa hiari aliokutana nao kwenye mishe mishe zake wala hawatoki kijiji kimoja hataki kuharibu video yake ya harusi waonekane wachovu wa vijijini.Unakuta makaka,sijui mabinamu sijui madada wote fix tupu ni wa hiari hawa kuwaambia waje na hela ya vinywaji na vyakula sahihi kabisa. Wana harusi walishe wanaowahusu sio hao wa hiari
 
Mm mwanamke wangu nilimwambia mahari kwa utaratibu wenu itakua sh ngapi. Akanijibu m 1.5 Nikamjibu ok. Wiki iliyopita nikaibetia mahari yote ili nisiwasumbue kamati ya harusi, ilikua nishinde milioni 12 real Madrid akachana mkeka. hadi mda huu nishaghairi kuoa na akipiga cm sipokei. Mama nae nimemwambia kunamambo yameingiliana siwezi oa tena . Nitajipanga tena 5 yrs baadae kwa stand up wedding. Madrid manina zake.
 
IMG-20180119-WA0002.jpg
 
Nikija na ugali wangu kwa vimposo vilivyokaushwa kutoka ziwa hombolo na togwa langu ntakuwa nmekosea mkuu?!
 
Kiukweli mm mpaka sasa natumiwa mssg za kufa mtu kuhusu mchango
michango inaboa sana na ukiendekeza unaweza fanyia kazi michango,maana unajikuta una kadi 98 ndani ya miezi miwil na kila moja inataka laki sasa hapo si lawama
 
Taratibu tutanyooka tu. Angalia misiba ya kusafiri siku hizi wanaondoka saa tano Asubuhi. Sio saa tisa tena. Hakuna kula hapo. Vyuma vimekaza balaa.
Mwishowe, harusini itakuwa bites tu, tena mchana mapema. Saa moja usiku mchezo wote umeisha
 
Kiukweli mm mpaka sasa natumiwa mssg za kufa mtu kuhusu mchango
Kama walikuchangia changa watakutoa roho ukisambaza kadi mfano 100 uchangiwe jiandae kulipa madeni kuna kadi mia zitakuja zote zikitaka uchangie usipige yowe kakope uchangie hizo.Hela ulikuwa huna kilichokufanya usambaze mikadi mingi nini? Sasa zamu yako
 
Huu utaratibu ni mzuri lakini naona unaweza leta shida kidogo kwa mpishi au mtu wa vinywaji ikiwa waliobook hawatokuja kitakacho tokea ni yeye kupata hasara hasa kwa chakula....

Ninachopendekeza ni mualikwa kutanguliza 50% ya bei ya chakula anacho hitaji hii itasaidia watu kuja kweli kuliko ku book halafu chakula kimetengenezwa mtu ana kacha hiyo hasara hakuna sehemu unaweza kui cover wakati hukuruhusu michango labda utatoa hela yako mfukoni wewe mwenye sherehe....
Utaratibu ni mzuri lakini napendekeza watu kutanguliza parcent kwenye chakula halafu swala la mtu kuagiza chakula anachotaka pia inaweza kuwa changamoto kidgo kwenye mapishi....
Nafikiri kiasi cha fedha kita determine aina ya chakula hivyo watu wataambiwa tuu bei za chakula tofauti tofauti......
 
iko poa sana hyo aisee....
Pia watu waanze kufanya harusi vijijini kwao hazina gharama na ndugu hujisikia raha sababu hawawezi safiri watafute nauli ya kwenda na kurudi na malazi na mchango wa harusi.Lakini ukifanyia kijijini attendance ya ndugu inakuwa kubwa kuliko kujaza chapombe na wala chakula kama mchwa majirani,marafiki,wafanyakazi wenzio na wapiga deal na mapedeshee na wahuni wa mjini ndugu wakiwa hawafiki hata kumi.Kadi uchangishe waambie harusi kijijini parokia ya mtakatifu nanihii.Walau waweza baki na chenji nzuri kwenye michango
 
Swali langu Kama imetokea mtu katoa oda ya chakula atakachokula na kikaandaliwa, je akipata udhuru au asipokuja Wakati nyie mmeisha ingia gharama ya kukiandaa nani anawajibika na hasara hiyo?
Nimependekeza kuwe na malipo 50% ya bei ya chakula unacho hitaji..... hii itahepusha kukacha na kupunguza hasara
 
Back
Top Bottom