Stori ya mkazi wa Hanang aliyepoteza mke na watoto 4 imenibadilisha sana

Unaambiwa maisha yanaenda yanavyotaka na unapaswa kuyafata Huwezi lazimisha tope kupanda mlima Hanang.
Lets relax mim hii week nina mfululizo wa kupigwa matukio KO ila kuna mwamba kasema Tunaenda kikomando hakuna kumwaga chozi.
pole sana mkuu, wakati mwingine unashare ili kupata mawazo mapya na relief pia ndugu yangu
 
Kuna mtu jana kaleta uzi hakuna video za kutosha za hilo janga la Hanang, na ukifikiria ni kweli matukio mengine kama ziara yanakua na full coverage, hili halina.

Viongozi wamegeuza tukio kua PR yao, wanajisafishia majina, hakuna impact yeyote
kabisa kwa ground wahanga wanaumia sana, imagine huyo ni mmoja kati ya wengi, hakuna full coverage
 
Hopefully msaada wako utapokelewa kwani kuna viongozi waandamizi wa CDM walienda na misaada kwaajili ya wahanga na wakazuiwa na jeshi la Polisi kuingia Hanang then wakaamriwa warudi walipotoka.
nimepata namba ya mhanga, nitamtumia moja kwa moja, bahati nzuri majina yake ni hayo hayo
 
Watakwambia ni shetani ndo kasababisha maafa halafu eti Mungu yupo paleee anashuhudia na hafanyi lolote.

Wengine watakwambia kazi ya Mungu haina makosa, kazi gani hiyo sasa ya kuua watu na kusababisha majonzi kwa watu..
😁😁😁😁🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nimeona BBC kupitia mitandao ya kijamii, Jamaa anaitwa Fanuel John, amepoteza familia yake na mali zake zote familia yake ni mke wake, mtoto wa miaka 13, 10, 8 na miaka 4 kwa mfuatano kama kijana mwenye familia nimehuzunika sana, nimewaza sana kuhusu maisha, watoto wangu, mke wangu, kazi yangu, wazazi wangu, ndugu zangu, Nchi yangu na kila yeyote anayenizunguka.

Nimekumbuka kaka yangu mmoja ambaye hua kila akiambiwa aoe anajivuta vuta sahv ana miaka 43, na anasema yeye ataishi na kurudi mbinguni (kufa) kama alivyokuja duniani(peke yake), nimejisemea inamaana Fanuel anaenda kufanana na kaka ambaye yeye hajawahi kuoa wala kua na mtoto, inshort anajiwazia yeye tu?

Fanuel anaenda kuanza upya kabisa kujitafuta, kutoka kuitwa baba kila siku mpaka kuzika familia nzima, na kati ya hao watoto kuna mmoja hajapatika sasa hapo ndiyo mtihani, atakutwa hai ama amekufa, maana yake tayari kazikiwa watoto watatu na mke mmoja maana yeye yuko hospitali.

Kweli hii dunia haina huruma, nimeumia sana. Kwa nionavyo mitandaoni kwingine maisha yanaendelea vizuri kama kawa, sehemu za starehe zinafurika, kina Vunjabei wanafungua maduka yao mapya weekend wakiwa na kina Harmonize, ziara zinaendelea kama kawaida na hakuna kilichosimama.

Nimekumbuka ujumbe mmoja niliuona kwa yule kijana wa Singida anaitwa Joram nkumbi anasema maisha ni yako na kifo ni chako pia, usilalamikie mtu, wewe wakati utakufa hakuna kitakachobadilika, ratiba zote za nchi na dunia zitaendelea kama zilivyopangwa, ratiba pekee inaweza kubadilika kidogo ni ratiba ya familia yako nayo ni kwa siku chache then itaendelea kama kawaida, hivyo sisi wote ni wa kawaida sana japo ni wa thamani,

Madhira aliyopata Fanuel anahitaji psychotherapist haraka sana na wengine wengi wenye tatizo kama lake huko Hanang, la sivyo mtu anaweza kuamua kuifuata familia yake, moyo wa mtu kichaka usimuone anasimulia tu huwezi jua.

Nimejifunza mengi kutoka katika tukio hilo la mafuriko, nimegundua maisha haya si chochote wala lolote yanaweza kuyeyuka wakati wowote kama mshumaa tusali sana ndugu zangu kila mmoja kwa imani yake, wa kanisani asali huko, wa msikitini vile vile, waamini mizimu pia, suala ni kujiombea mwisho mwema haijalishi unaomba kwa njia gani, wapi na kwa nani, huyo unaemwamini atakusaidia.

Maisha ni nini, binadamu anawaka na kuzimika muda wowote, unapoteza familia yako nzima ndani ya masaa machache unakua mtu mwingine kabisa, kwann usichanganyikiwe, yote kwa yote ni kushukuru kwa kila jambo lakini hiyo shukran sidhani kama akielezwa Fanuel sasa hv ataelewa.

sijafuatilia namna ya kuwapa msaada watu wa Hanang, hasa wa kifedha maana niko mbali na nchi yangu, lakini naweza kutuma kwa mitanda kadhaa, naomba nielekezwe ama nipewe link nikatoe chochote kitu wakati nikiendelea kutafakari maisha vizuri, maana nahisi bado sijayajua vizuri, nahitaji kutuliza akili sana na kutafakari upya na upya tena.

Niwatakie nyote ijumaa njema, Mwenyezi Mungu aendelee kutusimamia maana hatujui siku wala saa
I came naked, hell yeah... naked I shall return. Living life with no expectations, regret, attachments and credits. Even my kids are actually not my kids, they belong to the universe.
 
inasikitisha sana kwa kweli!MUNGU anaeza kuamua tu ww ukawa mfano kwa wengine kwa ajili ya kujifunza au kutimilisha ukuu wake!ndo maisha japokuwa yanaumiza sana sana!
Mimi nikiangalia mauaji na mateso wanajifanya hao mnaita ndugu zenu Kwa Wapalestina inanisikitisha sana.

Huwa naona maisha hayana maana na kulikuwa hakuna sababu ya kuzaliwa na ndio hapo Huwa siwaelewi mnaposherekea kile mnaita birthday mnasherekea nini ikiwa Dunia hii Ina maumivu mengi sio tuu Yako hata ya jirani Yako.
 
Video zilitoka sana siku 2 za Mwanzo,Kwa Sasa ni usagishaji tuu pengine na picha za Jana baada ya Ziara ya Rais ndio zimeonesha jinsi tope liliporomokakutoka mlimani.

Video hazibadili chochote, pengine ni Janga la kwanza la matope ila sio Janga la kwanza Kwa Tanzania Kuna mv Bukoba,mv islander nk kote huko Kuna simulizi za kusikitisha.

Pia Kuna Mzee alipoyeza nyumba na Watoto,mke wote kwenye moto hapo Dar sembuse huyo Jamaa ni Kijana? Ajipe Moyo ingawa ni ngumu ndio Dunia kifo hakizoeleki guliowahi fiwa tunajua ukikumbuka utaumia.
mimi nimeiskia hii ndiyo maana nimeshare hapa, kwakua ni touching story kwangu na nimeumia, kila mtu anapitia madhila kwa nafasi yake, hivyo kwa huyu kijana pia, kwake si jambo jepesi, wakati mwingine wazee wanahimili matatizo kuliko vijana maana wao wameona mengi, ni sawa na mimi baada ya kuona tukio hili, mbeleni nikiona tatizo lingine kama hili, nitaumia lakini si kama hili, maana kwa umri wangu bado naendelea kujifunza
 
Mimi nikiangalia mauaji na mateso wanajifanya hao mnaita ndugu zenu Kwa Wapalestina inanisikitisha sana.

Huwa naona maisha hayana maana na kulikuwa hakuna sababu ya kuzaliwa na ndio hapo Huwa siwaelewi mnaposherekea kile mnaita birthday mnasherekea nini ikiwa Dunia hii Ina maumivu mengi sio tuu Yako hata ya jirani Yako.
upo sahihi!lakini HAMAS walivyowarushia mabomu na makombora ile siku ya tarehe 7 ulitegemea israel wawarudishie kwa kuwarushia MAUA??mm nasisitiza sana vita ni vibaya sana na havina macho maana matokeo ya vita wanaoteseka ni watoto, wazee na wanawake!so kuepusha haya majuto ni kuacha kuchokozana!maana unapomchokoza mwenye nguvu lazima atakuchapa tu!huezi kumpiga mtu ngumi utegemee akupige busu!haipo hvo
 
Hakuna Janga ambalo linakuwa expected,sio wa kwanza unamaanisha

Hakuna Janga ambalo linakuwa expected,sio wa kwanza hapa Tanzania.
uko sawa ndugu yangu, lakin kumbuka majanga yamegawanyika, kuna natural na artificial (man made), mfano hayo ya vita za Hamas unayoyazungumzia ni man made, ukianzisha vita unatarajia nn, mabomu ya Hiroshima ya miaka hiyo ni made, na mengine mengi,
hii ni natural disaster mzee, ni ajali kama ajali zingine ambazo ziko beyond our capability
 
Kwenye classifications za majanga vita ipo ,hakuna Cha man made au nini,Janga ni Janga tuu na maumivu ni Yale Yale.
 
upo sahihi!lakini HAMAS walivyowarushia mabomu na makombora ile siku ya tarehe 7 ulitegemea israel wawarudishie kwa kuwarushia MAUA??mm nasisitiza sana vita ni vibaya sana na havina macho maana matokeo ya vita wanaoteseka ni watoto, wazee na wanawake!so kuepusha haya majuto ni kuacha kuchokozana!maana unapomchokoza mwenye nguvu lazima atakuchapa tu!huezi kumpiga mtu ngumi utegemee akupige busu!haipo hvo
Sasa watu zaidi ya 15,000 waliouwawa ndio Hamas?
 
mimi nimeiskia hii ndiyo maana nimeshare hapa, kwakua ni touching story kwangu na nimeumia, kila mtu anapitia madhila kwa nafasi yake, hivyo kwa huyu kijana pia, kwake si jambo jepesi, wakati mwingine wazee wanahimili matatizo kuliko vijana maana wao wameona mengi, ni sawa na mimi baada ya kuona tukio hili, mbeleni nikiona tatizo lingine kama hili, nitaumia lakini si kama hili, maana kwa umri wangu bado naendelea kujifunza
Huyo Bado Kijana ana Nguvu ,Ukiwa Mzee yakikukuta na waondoke watu ambao ndio Msaada wako unadhani itakuaje?
 
Huyo Bado Kijana ana Nguvu ,Ukiwa Mzee yakikukuta na waondoke watu ambao ndio Msaada wako unadhani itakuaje?
angekua mzee na amefikwa na madhira kama hayo si sawa na kijana, kwa sababu yeye pia hana muda mrefu wa kukaa hapa mbinguni kwa mjibu wa umri wa biblia ukiachana na majanga,
lakini kwa kijana kama huyo kwa mjibu wa biblia bado lifespan yake ni ndefu sana, alitakiwa aendelee kuenjoy na hao awapendao angalau kwa umri mrefu zaidi. japo kibinadamu sasa hua hakuna tatizo dogo na tatizo kubwa, tatizo ni tatizo tu, kwako linaeza kua dogo kwa mwingine likawa kubwa and vice versa
ahsante
 
Kwa hiyo umalize maisha Yako Duniani Kwa mateso au? Acha ujinga

Huyu ana Nguvu za kutafuta
 
Nchi hata maomboleze ya siku 2 hakuna...basi hata ya siku 1 hakuna
Media zote wao ni singeli misondo amapiano udaku tu unaendelea
Anyway hili taifa ndiyo lishafikia hivyo

Ova
Umeona mbali sana
 
Back
Top Bottom