Steven Wassira vs Ester Bulaya wazozana bungeni

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Feb 3, 2010
230
57
Sakata hilo lilitokea nje
ya ukumbi wa Bunge
mara baada ya
kuahirishwa kwa kikao
juzi usiku, ambapo
Wassira alimfuata
Bulaya na kumhoji
kwamba kwanini alitoa
maneno ya kuipinga
bajeti ya Serikali.
Wassira ambaye pia ni
Mbunge wa Bunda
(CCM)
Alimwambia Bulaya:
“Mimi ndiye Mbunge
wa Bunda, wewe huwezi
kujifanya ndiye
uliyetumwa na
wananchi kuja kusema
maneno ya uwongo
hapa, eti unaipinga
bajeti ya Serikali, ni
nani aliyekutuma?”
Waziri huyo alikwenda
mbali na kumwambia
mbunge huyo kijana
kwamba, “wewe
tunakufahamu una
pande mbili (upinzani
na CCM) na kila siku
unashirikiana na Halima
Mdee (Kawe-Chadema),
tunakujua kwamba uko
CCM na Chadema.”
Kutokana na kauli hizo,
Bulaya alijibu mapigo
akimwambia Wassira
kwamba yeye akiwa
mbunge wa CCM ana
wajibu wa kukikosoa
chama chake na
hakuwa mtu wa kwanza
kukataa kuunga mkono
bajeti hadi hapo
marekebisho
yatakapokuwa
yamefanywa.
“Mimi nina haki ya
kuzungumza ndani ya
Bunge na kusema kile
ninachokiamini kama
mbunge, wala hakuna
mtu wa kuniwekea
mipaka. Halafu kama ni
uhusiano na wabunge
wengine mbona
wabunge wengi tu wa
CCM wanashirikiana na
upinzani?” alihoji
Bulaya.
Source mwananchi
 
Sakata hilo lilitokea nje
ya ukumbi wa Bunge
mara baada ya
kuahirishwa kwa kikao
juzi usiku, ambapo
Wassira alimfuata
Bulaya na kumhoji
kwamba kwanini alitoa
maneno ya kuipinga
bajeti ya Serikali.
Wassira ambaye pia ni
Mbunge wa Bunda
(CCM)
Alimwambia Bulaya:
“Mimi ndiye Mbunge
wa Bunda, wewe huwezi
kujifanya ndiye
uliyetumwa na
wananchi kuja kusema
maneno ya uwongo
hapa, eti unaipinga
bajeti ya Serikali, ni
nani aliyekutuma?”

Waziri huyo alikwenda
mbali na kumwambia
mbunge huyo kijana
kwamba, “wewe
tunakufahamu una
pande mbili (upinzani
na CCM) na kila siku
unashirikiana na Halima
Mdee (Kawe-Chadema),
tunakujua kwamba uko
CCM na Chadema.”
Kutokana na kauli hizo,
Bulaya alijibu mapigo
akimwambia Wassira
kwamba yeye akiwa
mbunge wa CCM ana
wajibu wa kukikosoa
chama chake na
hakuwa mtu wa kwanza
kukataa kuunga mkono
bajeti hadi hapo
marekebisho
yatakapokuwa
yamefanywa.
“Mimi nina haki ya
kuzungumza ndani ya
Bunge na kusema kile
ninachokiamini kama
mbunge, wala hakuna
mtu wa kuniwekea
mipaka. Halafu kama ni
uhusiano na wabunge
wengine mbona
wabunge wengi tu wa
CCM wanashirikiana na
upinzani?” alihoji
Bulaya.
Source mwananchi
hahahahaaa,,,,wassira mzee wangu duh
 
anaogopa kitu kinaweza kuingia cdm kikamng'oa, anataka wote wawe mazoba wananchi wakose..choice
 
Back
Top Bottom