kapotolo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2010
- 3,727
- 2,214
Katika hali ya kushangaza Kituo cha Television cha Star TV kimerusha hewani habari ya siku tano zilizopita kuhusu Mgomo wa madaktari. Katika taarifa hiyo walimuhoji Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Mbeya Dr Chomboko ambae kwa wakati huo alisema hakuna mgomo hapo. Na kwa kupotosha zaidi wakaonyesha picha ya Dr Chomboka lakini jina la Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dr Samky.
Sijaelewa Star TV wanakusudia nini kwa upotoshaji wa aina hii, kama walitaka kuonyesha madaktari hawajagoma si wangeenda hata kwenye hospitali za wilaya kwenda kuhoji AMOs ambao wanaendelea na kazi kuliko kutuletea taarifa ya zamani na kuudanganya uma kwamba ni ya leo.
Yahya Mohamed ni member humu, tunaomba star TV iwaombe radhi watanzania kwa uchakachuaji huu na kwa kweli vyombo vya habari kama star tv mkianza hivi ile imani tuliokuwa nayo kwenu itapotea.