Star Tv na Redio Free kupunguza wafanyakazi

Kampuni kongwe ya habari nchini, Sahara Media Group itapunguza wafanyakazi wake takriban 100. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyoitoa kwa wafanyakazi, Jumatatu hii.
f28a779a8b88e54abbd6867eac71684e.jpg

sahara-media-group-5
Mwenyekiti Mtendaji wa Sahara Media Group, Dr Anthony Diallo

Imesema inachukua uamuzi huo kutokana na kuhamisha matangazo yake kutoka analojia kwenda dijitali na kwamba nia yake ni kupunguza gharama za uzalishaji. Watakaoathirika ni pamoja na watangazaji, watayarishaji wa vipindi na wafanyakazi wengine.

Itatumia takriban vinane kupunguza wafanyakazi ikiwemo utendaji, elimu, umri, nidhamu na vingine na kutumia kipindi cha miezi mitatu kukamilisha mchakato huo.

Wakati huo huo Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Dr Anthony Diallo, amekanusha tetesi zilizoenea kuwa kampuni hiyo imenunuliwa na kampuni ya Nation Media Group baada ya kushindwa kulipa madeni yake.

Madeni hayo ni pamoja na KCB inayodai shilingi bilioni 28, deni la benki ya Mkombozi, malimbikizo ya mishahara na kodi ya TRA shilingi bilioni 4.

“Tuna asset net value ya zaidi ya bilioni 110. Tuna mkopo kama kampuni na benki ya KCB pekee na hatuna deni kama kampuni huko Mkombozi. Kuuza media company kubwa kama yetu unahitaji kibali cha TCRA,” alijibu Diallo,.

“Tunapunguza wafanyakazi kutokana na uwekezaji mkubwa kwenye automation na kutegemea ununuzi wa vipindi badala ya kuvitengeneza wenyewe, ubora wa vipindi vya kutengenezwa na wengine ni bora zaidi.”

Hadi sasa kampuni hiyo imeajiri wafanyakazi zaidi ya 400.

Source: Bongo5
mdololo wa uchumi
 
Mmh, hapo chacha ndo shida za kuajiriwa kwenye kampuni binafsi,bora mimi niliejiamulia kuajiriwa na serikali hapa mpaka nife,ila juma pumba maharagwe nae anatutisha
 
Doh... maskini... hiki kituo kilikuwa bize sana na kampeni za prezidaa. Nadhani atawakumbuka awaajiri kwenye sirikali yake tukufu isiyojaribiwa.
Akifunga kampeni nadhani ilikuwa mwanza, Mkemia aliwashukuru sahara media kwa kazi kubwa na aliahidi 'nitakusaidia'
 
Hapa ndipo pale ninapotafakari ukuu wa Mungu, anakuambia mtu akikupiga kofi upande wa kushoto mgeuzie na wa kulia, basi nenda zako acha yeye ashughulike nae mgomvi wako, hawa walitumika kumtuka sana Lowasa na hakuwahi kuwajibu kwa lolote, yameanza Dialo, sasa wengine wajiandae kina Mwakye..na wafuasi wao, siko la Mungu si zito lilisikia yote, atapunguza na hata ona faida mpaka arudi na atubu, lazima hii media ife tu hakuna namna.
 
Back
Top Bottom