Stand ya Mwenge kuhamishiwa Makumbusho,ni sawa?

Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
71,121
94,380
Nilikua nasikiliza Radio One asubuhi hii,nikasikia eti ile terminal ya mabasi pale Mwenge inahamishiwa Makumbusho...

Eti moja ya sababu ni kwamba wafanyabiashara wanaopanga bidhaa chini na mezani nyakati za jioni, wanasababisha kituo kuwa finyu.

Hivyo suluisho ni kuhamisha kituo chote wakiwemo na wafanyabiashara kwenda Makumbusho.

Je hii ni sawa? mbona hawa watunga sheria wanataka kututesa.
 
Inawezekana; lkn pale Makumbusho hakuna nafasi tena! ileOpen space iliyokuwepo awali imeisha vamiwa na wenye pesa na kujenga majengo yao ya nguvu;

au wana mpango wa kubomoa vijinyumba vya walala hoi walioko maeneo ya pembeni kuzunguka iliyokuwa Stand zamani??
 
binafsi naona ni vyema kituo cha mabasi kiendelee kuwepo kama kawaida.

Mwenge imeshakuwa moja ya vitongoji vyenye idadi kubwa ya watu wanaofanya biashara na shughuli za kiofisi...leo hii pakigeuzwa kama kituo kidogo na si terminal,watu hawa unawawekea mazingira magumu ya kupata usafiri.

Mabasi yatakua yanapita yakiwa yamejaa
 
Kwani watu kutoka na Kurudi Makazini Unahitajika kwenda stend Kufanya nini?

Nataka kwenda Ubungo kutoka Mwenge, Nipande Basi Hadi makumbusho ndio nitafute basi ya ubungo?

Mimi sijaelewa!! Labda unieleze ni stendi ya Kibaha, Bagamoyo na Mlandizi Ila sio kwa Town trips, Itakuwa ni Kupotezeana Muda
 
Wanachotakiwa wafanye wafidie Watu Pale Mwenge Lipatikane eneo Kubwa kwa kuwa stend, That is Good Intersection!!
 
Nilikua nasikiliza Radio One asubuhi hii,nikasikia eti ile terminal ya mabasi pale Mwenge inahamishiwa Makumbusho...
Eti moja ya sababu ni kwamba wafanyabiashara wanaopanga bidhaa chini na mezani nyakati za jioni,wanasababisha kituo kuwa finyu. Hivyo suluisho ni kuhamisha kituo chote wakiwemo na wafanyabiashara kwenda Makumbusho.
Je hii ni sawa? mbona hawa watunga sheria wanataka kututesa.

ukisema wanawatesa watakujibu ni serikali sikivu, hivi dawa ya tatizo ni kulikimbia ama kukisolve? Inamaana na makumbusho wakijaa watahamia moroko? Mwisho wake watafika k.koo
 
Kwani watu kutoka na Kurudi Makazini Unahitajika kwenda stend Kufanya nini? Nataka kwenda Ubungo kutoka Mwenge, Nipande Basi Hadi makumbusho ndio nitafute basi ya ubungo? Mimi sijaelewa!! Labda unieleze ni stendi ya Kibaha, Bagamoyo na Mlandizi Ila sio kwa Town trips, Itakuwa ni Kupotezeana Muda

labda kuna kitu unashindwa kukielewa ndugu...kuna bus stand na bus terminal..

Mwenge, kama ilivyo Posta, Kivukoni, Mbezi Mwisho, Tandika n.k ni kariba ya Bus Terminal...yaani mabasi yanaanza na kumalizia safari zake...

Magomeni Mapipa, Kwa mtogole, Tabata Relini n.k ni kariba ya Bus Stand...yaani basi linasimama kushusha na kupakia abiria..

Sasa unapotaka kuifanya Mwenge iwe ni Bus Stand wakati inahudumia watu lukuki, ni kutaka tu kuwatesa watu.

Mpaka sasa vile ilivyo ni terminal lakini inaelemewa kwa kuwa watu fulani miaka ya nyuma walishindwa kupanga mipango endelevu...

Wakabinafsisha maeneo ili wafanye biashara...leo hii wanakuja na mbadala wa kuhamisha Terminal
 
Nilikua nasikiliza Radio One asubuhi hii,nikasikia eti ile terminal ya mabasi pale Mwenge inahamishiwa Makumbusho...
Eti moja ya sababu ni kwamba wafanyabiashara wanaopanga bidhaa chini na mezani nyakati za jioni,wanasababisha kituo kuwa finyu. Hivyo suluisho ni kuhamisha kituo chote wakiwemo na wafanyabiashara kwenda Makumbusho.
Je hii ni sawa? mbona hawa watunga sheria wanataka kututesa.
Mbona makumbusho palishauzwa siku nyingi?
 
Yale majengo ya makumbusho stand ni ya nani? Kuna bar moja napendelea kwenda kunywa inaitwa "simba kapakatwa"...just around that area!
 
Back
Top Bottom