Spika: Wanawake jitoseni majimboni

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174

Spika: Wanawake jitoseni majimboni

Imeandikwa na Namsembaeli Mduma; Tarehe: 25th January 2011 @ 07:42

BAADHI ya wanasiasa wanawake katika vyama vya siasa wamekuwa hawajiamini kugombea ubunge majimboni na badala yake kusubiri uteuzi wa kuingia bungeni kwa viti maalumu.

Hata hivyo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, haoni kama viti hivyo vinakidhi demokrasia,na anawataka waache kusubiri uteuzi na badala yake wajitose majimboni.

Kificho anasema ni vema wanawake wakagombee majimboni kwa kuwa mazingira yaliyokuwa kikwazo kwa wanawake kupata ubunge kupitia njia ya demokrasia ya moja kwa moja ya kupigiwa kura na wananchi hayapo tena.

Kutokana na hali hiyo, amesema sasa kuna mazingira shawishi na mwanya wa kutosha kwa wanaojiamini kuingia ulingoni na kuomba ridhaa ya uongozi kwa watu wanaotaka kuwaongoza.

Akizungumza na HABARILEO ofisini kwake Mbweni mjini Zanzibar hivi karibuni, Kificho alisema kikwazo kimojawapo kilikuwa ni imani potofu miongoni mwa wananchi kwamba wanawake hawawezi kuongoza.

Lakini alisisitiza kuwa hali hiyo imetoweka na imethibitika hivyo, baada ya waliojaribu kuudhihirishia umma kuwa hakuna aliyeumbiwa kushindwa.

“Nisingevipendelea zaidi viti maalumu, kwa sababu haviwakilishi demokrasia ya moja kwa moja na vilianzishwa wakati ule mwanamke alipokuwa akikandamizwa na mfumo wa utamaduni ulioamini kuwa mwanamume pekee ndiye anayeweza uongozi, mambo hayo kwa sasa hayapo.

“Ni vema ikafahamika kwamba mazingira yaliyopo ni tofauti sana na ya wakati ule kwamba yanampa mwanamke uhuru sawa wa kugombea na kuchaguliwa kuwa kiongozi, ili mradi aithibitishie jamii anayotaka kuiongoza kuwa hataiangusha,” alisema Kificho.

Alifafanua kuwa utamaduni uliosababisha jamii kuamini kuwa mwanamke yuko chini kiuchumi na kisiasa (uongozi) ndio uliosababisha wawepo wawakilishi na wabunge wa upendeleo (viti maalumu) katika Bunge na Baraza la Wawakilishi, jambo analosisitiza kuwa limepitwa na wakati.

“Ilikuwa enzi hizo, mwanamke wa sasa ana bidii ya kujiinua kiuchumi na si dhaifu wala wa kukandamizwa na mwanamume tena, hayo ni mabadiliko na yanaweza kabisa kumsukuma aweze kusimama jimboni, kuomba kura za wananchi na kupitishwa,” alisema.

Alisisitiza kuwa haamini katika viti maalumu na angependa busara zaidi itumike kwa wanawake wenyewe kuamua kuleta mabadiliko sahihi ya kuachana na upendeleo huo na kugombea majimboni.

“Wengi waliojaribu waliweza na ninadhani waliowachagua waanaona na kufurahia uwajibikaji wao, wengine nao wafanye hivyo, hiyo ndiyo demokrasia ya moja kwa moja,”alisema.



Jumla Maoni (1) Maoni Ukweli hivi viti vya wabunge maalum serikali ingeviondoa,maana sasa wanawake wanaweza kujipigia debe na kufanikiwa kunyakuwa jimboni, hakuna haja ya kujiongezea gharama zisizo na msingi leo kila mbunge ukiangalia gharama zake za mshahara na marupurupu ni zaidi ya million 12 sasa kwa wabunge zaidi ya 100 kwa mwezi ni Billion 1.2 kwa miaka 5 ni billion 6 hapo bado gharama ndogo ndogo za vikao na safari !! Tuliangalie hili nadhani ktk katiba mpya iondolewe kifungu cha wabunge maalumu,ingawa kuvifuta inakuwa ngumu kwani waliopo madarakani wanjifagilia viwepo,wakija kuanguka huku wabebwe huku!!
 
Hongera sana kwa kificho kwa kutoboa ukweli ya kuwa....................................mbeleko za viti maalumu siyo demokrasia na vinasababisha uwakilishi haramu kwenye jamii......................hizi busara dada yetu Anne makinda kamwe hawezi kuthubutu kuzitamka hadharani na ataendelea kudai.........fifty-fity bila ya kujali matakwa ya wapigakura..................................
 
Back
Top Bottom