Spika Tulia: Bunge litajadili ushirikiano wa DP World na Bandari

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson amesema azimio la Bunge kuhusu kuridhia ushirikiano wa uendelezaji na uboreshaji wa utendaji wa bandari Tanzania, litawasilishwa bungeni Juni 10, 2023 kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa na wabunge.

Azimio hilo ni mapendekezo ya kuridhia makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya katika uendelezaji na uboreshaji wa utendaji wa Bandari Tanzania la 2023.

Akizungumza leo Alhamisi Juni 8, 2023, Dk Tulia amesema kuwa azimio hilo bado liko katika kamati ya pamoja ya Bunge inayojumuisha Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) na Miundombinu ambayo bado inaendelea kupokea maoni ya wadau ambao hawakuweza kufika Juni 6, 2025.

Amesema maoni ya kuhusu azimio hilo yanapokewa kupitia pia anwani za barua pepe zilizowekwa katika barua ya kuitisha maoni ya wadau.

“Azimio sasa bado liko katika ngazi ya kamati ya pamoja kwa mujibu wa kanuni na mara baada ya kamati kumaliza kazi yake azimio hilo limepangwa kuingia bungeni Juni 10, 2023 kwa ajili ya mjadala na kupitishwa na Bunge,” amesema.

Amesema Bunge litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza uchumi na maendeleo Tanzania.

“Bunge liko tayari kupitia kamati zake kupokea na kujadili na kutoa maoni yale ambayo wananchi wameileta kule yenye lea kuboresha utekelezaji wa mipango ya Serikali,”amesema.

MWANANCHI
 
The decision of the Tanzanian government to give DP World the management of its ports is a complex one with both potential benefits and risks.

On the one hand, DP World is a well-respected global port operator with a proven track record of success. The company has invested heavily in port infrastructure and technology, and it has a strong focus on customer service and efficiency. This could potentially lead to significant improvements in the performance of Tanzania's ports, which could boost trade and economic growth.

On the other hand, there are concerns that giving DP World control of Tanzania's ports could lead to increased costs and decreased transparency. DP World is a private company, and it is not subject to the same level of government oversight as a public entity. This could make it difficult for the Tanzanian government to ensure that the company is acting in the best interests of the country.

Ultimately, the decision of whether or not to give DP World the management of Tanzania's ports is a political one. The government will need to weigh the potential benefits and risks carefully before making a decision.

Here are some of the potential benefits of giving DP World the management of Tanzania's ports:

Improved efficiency: DP World has a proven track record of improving the efficiency of ports. This could lead to shorter waiting times for ships, lower costs for businesses, and increased trade.

Increased investment: DP World is likely to invest in the port infrastructure, which could create jobs and boost the economy.

Improved technology: DP World is a leader in port technology. This could lead to the adoption of new technologies that could improve efficiency and safety.

Here are some of the potential risks of giving DP World the management of Tanzania's ports:

Increased costs: DP World is a private company, and it is likely to charge higher fees than a public entity. This could lead to higher costs for businesses and consumers.

Decreased transparency: DP World is a private company, and it is not subject to the same level of government oversight as a public entity. This could make it difficult for the Tanzanian government to ensure that the company is acting in the best interests of the country.

Loss of control: Giving DP World control of Tanzania's ports could lead to a loss of control over the country's maritime assets. This could have implications for national security and sovereignty.

The Tanzanian government will need to carefully weigh the potential benefits and risks of giving DP World the management of its ports before making a decision.
 
Skia wote tunajua Wewe spika ni miongoni mwa wanufaika wa royal family. Hiyo bandari ilikuwepo hapo kabla hamjashika madaraka na mtaondoka mtaiacha hapo.

Wewe jinadi utaendelea kuunga mkono juhudi ipo Siku utajuta.
 
Kashasema wanapitisha, kuunga mkono juhudi zote za awamu ya 6.
Yaani kaongea utop..o, tetesi zinasema hili jambo limesainiwa tangu October Mwaka jana, na Mwaka huu wabunge wameenda Dubai.. Inasemekana nao wamekabidhiwa Asante nafikiri hiyo tarehe kumi wataacha kupitisha kama wao wanasapoti jitihada zote za serikali? Tumepigwa... Ila wote walio husika watajuta wao na vizazi vyao... Ni swala la muda tu... 😭😭😭
 
Ukisikia tuu , "Bunge litaendelea kuonga mkono Juhudi za Serikali......."

Ujue hapo hamna kitu.
 
Yaani kaongea utop..o, tetesi zinasema hili jambo limesainiwa tangu October Mwaka jana, na Mwaka huu wabunge wameenda Dubai.. Inasemekana nao wamekabidhiwa Asante nafikiri hiyo tarehe kumi wataacha kupitisha kama wao wanasapoti jitihada zote za serikali? Tumepigwa... Ila wote walio husika watajuta wao na vizazi vyao... Ni swala la muda tu...
Hawawezi watu wanarundika mali wanasahau kama wataziacha mungu atawatokomeza wote kwa njia anayoijua yeye.
 
Hayo maoni ya nini wakati Mkataba (MoU) tayari umeshasainiwa? Au kuna mkataba mwingine? Kwa nini hayo maoni hayakukusanywa mapema kabla ya mkataba kusainiwa? Haya maoni yanayokusanywa yatasaidia nini tena?

Yaani kama vile Mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani Kisha akahukumiwa kifungo cha kutumikia jela bila ya mtuhumiwa huyo kupewa nafasi ya kujitetea. Akiwa jela anatumikia kifungo chake ndio anaambiwa kwamba sasa unaweza kuanza kujitetea kwa makosa yako uliyotuhumiwa na kuhukumiwa nayo.

Very strange moment indeed!!
 
Ziko taarifa kuwa Masheikh na wanazuoni wa Kiislamu katika mikoa yote wanapanga kusoma Albadir usiku leo kama sehemu ya kumshitakia mwenyezi Mungu kwa tukio la kuuza bandari kwa Waarabu linalofanywa na wabunge kesho.

Wanazuoni hao wamefikia hatua hiyo baada ya kuona njia zote walizotumia kuwashauri wabunge wakatae jambo hilo kushindikana baada ya kuwepo taarifa za kuwepo mashinikizo makubwa ya fedha walizopewa wabunge hao ili waone hilo ni jambo jema kwa nchi.
 
ZIKO taarifa kuwa Masheikh na wanazuoni wa Kiislamu katika mikoa yote wanapanga kusoma Albadir usiku leo kama sehemu ya kumshitakia mwenyezi Mungu kwa tukio la kuuza bandari kwa Waarabu linalofanywa na wabunge kesho...
That will do nothing, ni physical confrontation kama sudan
 
Back
Top Bottom