Spika Tulia anasema wamepitisha makubaliano na sio mkataba. Swali langu kwani makubaliano sio mkataba?

Hennes kolon

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
673
1,287
Binafsi sijamuelewa Mhe. Spika anaposema kilichofanywa na waheshimiwa wabunge ni kupitisha makubaliano tu Kati ya serikali na DP WORLD, hivi mle ndani ya mkataba si ndo makubaliano yenyewe!?

Na Kama makubaliano sio mkataba kwa nini wapoteze muda kujadili makubaliano ambayo kwa tafsiri ya Mhe. sio mkataba wenyewe!?

Halafu ilikuwa na haja gani Rais kuweka signature kwenye makubaliano ambayo kimsingi (kwa tafsiri ya Mhe. spika)sio mkataba halisi?

wataalamu hebu tusaidieni darasa la Saba , tafsiri ya mh. spika.
 
Hawa ndio wanaomchimbia shimo Rais Samia.

Rais Samia akiwasikiliza hawa wanafiki wanaompotosha badala ya kuwasikiliza watu wakweli, wenye weledi na upeo mpana, hatakuwa na wa kumlaumu. Watu wamemtafunia kila kitu kumwonesha kila upuuzi kwenye huo mkataba wa kishenzi.

Hawezi kujitetea kuwa hakujua. Amepewa ushauri wa bure na watu wenye wenye uelewa mkubwa na mpana. Akiamua kuwasikiliza watu mbumbumbu ba wanafiki, atakuwa amechagua mwenyewe kwa hiari yake, na Taifa ajue halitakubali waliyoyapanga yatokee.
 
binafsi sijamuelewa mh. spika anaposema kilichofanywa na waheshimiwa wabunge ni kupitisha makubaliano tu Kati ya serikali na DP WORLD, hivi mle ndani ya mkataba si ndo makubaliano yenyewe!? na Kama makubaliano sio mkataba kwa nn wapoteze muda kujadili makubaliano ambayo kwa tafsiri ya mh. sio mkataba wenyewe!? ,halafu ilikuwa na haja gani rais kuweka signature kwenye makubaliano ambayo kimsingi (kwa tafsiri ya mh. spika)sio mkataba halisi .

wataalamu hebu tusaidieni darasa la Saba , tafsiri ya mh. spika.
Makubaliano ni agreement, mkataba ni contract, kila contract ni makubaliano ila sio kila makubaliano ni contract Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!.

Kilichopitishwa ni Bunge ni IGA ni Bunge kuridhia serikali yetu kuingia mkataba na DPW. Mkataba ni HGA, huu bado haijaingiwa.

P
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Una akili sana mkuu
 
Hajui anachoongea huyo
Dhamiri yake mwenyewe inamkataa
Anatumia nguvu nyingi kuaminisha watu kuwa ni makubaliano na si mkataba kwa kuwa yeye ni mwanasheria anajua kabisa limkataba lao halina sifa ya kuwa mkataba ndiyo maana amelibatiza kuwa ni makubaliano

Ukimsikiliza kila wakati alipotaka kusema makubaliano alikosea na kusema mkataba alafu ndiyo sasa ajisahihishe
Siyo lazima kuwa mwana saikoloji ili kujua anachokiongea ni tofauti na uhalisia
 
Binafsi sijamuelewa Mhe. Spika anaposema kilichofanywa na waheshimiwa wabunge ni kupitisha makubaliano tu Kati ya serikali na DP WORLD, hivi mle ndani ya mkataba si ndo makubaliano yenyewe!?

Na Kama makubaliano sio mkataba kwa nini wapoteze muda kujadili makubaliano ambayo kwa tafsiri ya Mhe. sio mkataba wenyewe!?

Halafu ilikuwa na haja gani Rais kuweka signature kwenye makubaliano ambayo kimsingi (kwa tafsiri ya Mhe. spika)sio mkataba halisi?

wataalamu hebu tusaidieni darasa la Saba , tafsiri ya mh. spika.
Kuna Mkataba usiokuwa Makubaliano? Makubaliano yenye commitment ambazo usipotimiza itakuwa umetengeneza mgogoro ni mkataba. Hii IGA ina commitments za serikali zote mbili na kama hazitatimizwa zitaishia Johannesburg kwenye arbitration.

Hawa maprofesa wanasiasa wasitake kutuchanganya. Wakiri tu kuwa walifanya makosa kuupitisha na sasa kuna uwezekano mkubwa wa kutakiwa kulipa kama tutataka kurekebisha vifungu vilivyomo.

Amandla...
 
Mkataba ni makubaliano yenye nguvu kisheria. Si kila makubaliano yana nguvu kisheria. Kwa hiyo kila mtakaba ni makubaliano lakini sio kila makubaliano ni mkataba.
 
Makubaliano ni agreement, mkataba ni contract, kila contract ni makubaliano ila sio kila makubaliano ni contract Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!.

Kilichopitishwa ni Bunge ni IGA ni Bunge kuridhia serikali yetu kuingia mkataba na DPW. Mkataba ni HGA, huu bado haijaingiwa.

P

Unapitishaje makubaliano ya kipuuzi kama yale? Makubaliano ya kipuuzi huzaa mikataba ya kipuuzi na hayo hufanywa na watu wapuuzi wasio na akili
 
Binafsi sijamuelewa Mhe. Spika anaposema kilichofanywa na waheshimiwa wabunge ni kupitisha makubaliano tu Kati ya serikali na DP WORLD, hivi mle ndani ya mkataba si ndo makubaliano yenyewe!?

Na Kama makubaliano sio mkataba kwa nini wapoteze muda kujadili makubaliano ambayo kwa tafsiri ya Mhe. sio mkataba wenyewe!?

Halafu ilikuwa na haja gani Rais kuweka signature kwenye makubaliano ambayo kimsingi (kwa tafsiri ya Mhe. spika)sio mkataba halisi?

wataalamu hebu tusaidieni darasa la Saba , tafsiri ya mh. spika.
Mkataba=Makubaliano ya kisheria
Yule spika ni kilaza kabisa, hujui nini maana ya mkataba.
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Salute mkuu.Natamani haya yawafikie Watanzania wengi iwezekanavyo.
 
Makubaliano ni agreement, mkataba ni contract, kila contract ni makubaliano ila sio kila makubaliano ni contract Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!.

Kilichopitishwa ni Bunge ni IGA ni Bunge kuridhia serikali yetu kuingia mkataba na DPW. Mkataba ni HGA, huu bado haijaingiwa.

P
Pascal unadanganya tena. Makubaliano yote yenye commitment ni mikataba. Ndoa ni makubaliano lakini kwa vile ina commitment inahesabika kama mkataba. Kuna gharama za kuivunja.
Katika huu mkataba wa IGA serikali hizi zimeteua kampuni za TPA na DPW kama agents wao wa kuutekeleza. Utekelezaji wa huu mkataba utakuwa kupitia HGAs ambazo TPA na HGA zitaweza kuingia zikiongozwa na masharti yaliyomo katika mkataba mama wa IGA.
Bunge limeridhia mkataba kati ya serikali za Tanzania na Dubai. Baada ya huo mkataba, agents wa hizi serikali ndio wataweza kuingia katika mikataba tofauti ya utekelezaji.
Itakuwaje haujui tofauti kati ya HGA na IGA wakati wewe ni mwanasheria na sisi wengine ni ngumbalu?
Btw Makubaliano ya Awali ( MoU) yaliisha ingiwa kati ya TPA na DPW na yametajwa katika IGA. Kuiita IGA kuwa ni MoU ni kututukana.

Amandla...
 
Ni makubaliano ya kukubaliana - haya ndiyo sheria mama na ndiyo maana yakatiwa saini na Waziri kwa niaba ya Mkuu wa nchi kwa kiapo rasmi cha kisheria, na ndiyo maana yakapelekwa Bungeni kubarikiwa kuwa Sheria kabla ya utekelezaji wake kuanza.

Tumepigwaaaaaa !!! Prof. Shivji kashasema kama tunataka kujitoa ni lazima jambo hili liende Bungeni tena liwe revoked, hakuna mamna nyingine kwa sasa, We're in.
 
Kwahio wamekubaliana vitu ambavyo watakuja kuvikataa kwenye Mkataba ?

Yaani wameingia kwenye gharama zote hizi kukubaliana vitu ambavyo havina mashiko, Ili wakae tena wakubaliane vya kuwekwa kwenye mkataba; au hatua inayokuja ni ya kuweka vitu official ?

Kwahio wabunge wamekubalia kabisa kwamba haya makubaliano yanafaa, alafu nani atakuja kuyakataa kwenye Mkataba kwamba hayafai ? Malaika ?!!!!

Na kama yanafaa kwanini yabadilishwe kwenye Mkataba ?
 
Back
Top Bottom