Spika Makinda Kaishitukia Serikali Ya Kikwete Haina Huruma na Mtanzania

Na bado hapo ndio wataelewa sasa kwanini wananchi hatukupenda wajiuzie nyumba za serikali, mtakumbuka Makamba alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar alifikia hotelini hadi akaibiwa Redio yake, laiti nyumba za serikali zingekuwepo hii dhahama kwa wnanchi wala tusingeijua.
Hizi hoteli wanazofikia zinaweza pia kuwa dili la wafanya biashara wenye fungate na serikali,wanajihakikishia wateja ambao ni viongozi wa serikali,hapakosi maslahi binafsi hapo
 
sio hivyo tu hiyo ndio njia pekee wakati njia,
kwa maana nyingine mvua zikianza watu hawana njia
mimi namsapoti kuhama hotelini lakini hiyo njia ifunguliwe

mmmmmhhhhhhhh awafungie njia watu......that is so unfair...kwani si ana fedha za kutosha atafute a different place...where she does not disturb local population and the population will not disturb her instead of inconveniencing wananchi to foot 45 mns daily instead of 5-10 mns....ukizidiwa hizo dakika kwa idadi ya watu utapata masaa mengi sana wasted na hiyo ni hasara kwa watu na pia kwa jamii
 
ana nusuru hela ya serikali au anataka hela anayo lipia hotel aweke mfukoni
kwake?
sioni tofauti yoyote,atuambie pia alikua anatumia kiasi gani hotelini
 
hiyo hawezi kusema hila ni rahisi kujua
tafuta quotation za hotel hapo DAR
VIP room kwa siku ni kiasi gani?
am working on it

ana nusuru hela ya serikali au anataka hela anayo lipia hotel aweke mfukoni
kwake?
sioni tofauti yoyote,atuambie pia alikua anatumia kiasi gani hotelini
 
tukichukua nchi yetu hawa Miungu watu watapata shida sana, fungeni tu hata mkiamua kaanzieni Chalinze Kabisa
 
Serikali imepata hasara kubwa ya shilingi 200 bilioni kutokana na uamuzi wa kifisadi wa Mkapa na Magufuli wa kuuza nyumba za Serikali. Pesa hizi ni kuwalipia malazi na chakula Wafanyakazi na familia zao. Kama uamuzi huo wa kifisadi usingefanyika basi hizi shilingi bilioni 200 zingeweza kutumia katika sekta nyingine zenye umuhimu zaidi kama elimu, umeme au mahospitalini.

Huyu Makinda anadhani yeye ni nani hadi aamue kufunga barabara?
 
kwa new africa hotel, hapo ni room tu ni kuanzia $140
bado msosi na mambo mengine kama internet......
kwa heshima yao nadhani wanatumi hiyo suite $190


ana nusuru hela ya serikali au anataka hela anayo lipia hotel aweke mfukoni
kwake?
Sioni tofauti yoyote,atuambie pia alikua anatumia kiasi gani hotelini
 
hapo na familia zao ndipo tunapoliwa zaidi, maana tafasiri ya familia kibongo ni utata, weka na ufisadi, mimi niko sure toka waziuze ni zaidi ya bilioni 200,
bado najiuliza kwa nini waliuza kama walijua wataitaji kutoa nyumba kwa wafanyakazi wao, kikwete na mkapa wote walikuwepo kwenye hiyo cabinet lengo ilikuwa ni nini?

serikali imepata hasara kubwa ya shilingi 200 bilioni kutokana na uamuzi wa kifisadi wa mkapa na magufuli wa kuuza nyumba za serikali. Pesa hizi ni kuwalipia malazi na chakula wafanyakazi na familia zao. Kama uamuzi huo wa kifisadi usingefanyika basi hizi shilingi bilioni 200 zingeweza kutumia katika sekta nyingine zenye umuhimu zaidi kama elimu, umeme au mahospitalini.

Huyu makinda anadhani yeye ni nani hadi aamue kufunga barabara?
 
kwa hiyo mpaka muheshiwa aone huruma ????????? kwa nini utaratibu /sheria kama hizi zisiondolewe??????????
MASKINI TANZANIA YANGU -MUNGU MBARIKI MKWELE
 
hii sio sheria mkuu, ni maamuzi yao yakutojari watu , hawana huruma na pesa ya umma, sijui utaweka sheria gani kwa hawa
kwa hiyo mpaka muheshiwa aone huruma ????????? kwa nini utaratibu /sheria kama hizi zisiondolewe??????????
MASKINI TANZANIA YANGU -MUNGU MBARIKI MKWELE
 
any way, hvyo ndvyo halimashaur ya kchwa chake imemtuma. Hawa ndio viongozi tunaotegemea watutoe ktk lind la umaskini unaotukabili...............:pound:
 
tukichukua nchi yetu hawa Miungu watu watapata shida sana, fungeni tu hata mkiamua kaanzieni Chalinze Kabisa
Kila lenye mwanzo lina mwsho, hata wakoloni walikula bata ndani ya Tanganyka(TANZANIA) leo wako wap????????
 
Huko hotelini alipokuwa anakaa nako walifunga njia zote? Upumbaf huu

Hao watu wa usalama waimarishe ulinzi wao,kama ni askari waweke idadi kubwa zaidi au njia nyingine watakazo ona zinafaa! Yani ile mitaa ilivo ukifunga njia,n usumbufu mkubwa,tunajua tatizo la miundo mbinu nchini kwetu.

Sinza aliikuta bwana na ipo pale siku zote,hio post yake ina mwisho
 
yawezekana walifunga na kulipia floor nzima kuna mengi yatakuja kulipuka siku mafisadi wakiachia ikulu
Huko hotelini alipokuwa anakaa nako walifunga njia zote? Upumbaf huu

Hao watu wa usalama waimarishe ulinzi wao,kama ni askari waweke idadi kubwa zaidi au njia nyingine watakazo ona zinafaa! Yani ile mitaa ilivo ukifunga njia,n usumbufu mkubwa,tunajua tatizo la miundo mbinu nchini kwetu.

Sinza aliikuta bwana na ipo pale siku zote,hio post yake ina mwisho
 
Kila mtu ana mambo yake biafsi. Yaani spika kila kitu akiulizwa anamtupia k/ wa bunge ajibu. Ndo maana namuunga mkono msekwa alivyosema kuwa spika wa bunge ni vizuri awe mwanasheria. Huyu mama mbumbumbu kabisa.
 
Hivi mawaziri wote wakiishi kwenye nyumba zao na viongozi wengine wa juu serikalini, Wakafunga njia Dar kutakalika tena??Au ndo tutapelekwa kuishi Tandahimba ili viongozi waishi Dar ?Nadhani kuna taratibu maalum za nyumba za viongozi kuishi maeneo fulani.Kama hazitoshi basi wawachukulie viwanja huko Mkuranga na Kimbiji kwani wana magari ya kufika huko! Inanikumbusha kule Harare ,Mugabe hufunga njia ipitayo karibu na makazi yake na muda wote hulindwa na kikosi maalum cha Mizinga hata kama hayupo!!! Ni gharama gani hizo kwa walipa kodi?Acha usumbufu kwa raia!!!!

CCM wamezoea. Makao ya chama Dodoma baadhi ya barabara za za kuzunguka zimefungwa. Manispaa, CDA wanajua na wamehusika
 
Tatizo viongozi wetu hawa wanajionaga miungu watu!!..kama hataki usumbufu ni bora ahame uko uswahilini na akaishi masaki..kwani hana nyumba huko!
 
  • Kahamia kwenye nyumba yake Sinza kutoka Hotel alikokuwa anaishi
  • Asema anaokoa pesa ya umma
  • Amewafungia njia wananchi wa Sinza
  • Je matumizi kama haya ni moja ya sababu ya serikali yetu kuwa mufilisi
  • Kwa nini na mawaziri wasirudi kwenye nyumba zao kuepusha gharama kubwa tunazolipa kwa siku

GAZETI MWANANCHI

Makinda azuia watu kutumia barabara

Joseph Zablon

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda anadaiwa kufunga njia inayounganisha eneo la Kijitonyama na Sinza, Dar es Salaam na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji.Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na baadhi ya wakazi wa sehemu hiyo zimeeleza kuwa kutokana na kufungwa kwa njia hiyo, sasa wanalazimika kutumia dakika 45 kufika Sinza kwa miguu badala ya dakika tano hadi 10 walizokuwa wakitumia awali.

Mkazi wa eneo hilo, Juma Mbegu alieleza kuwa njia hiyo imefungwa katika Mtaa wa Sahara, jirani na Kituo Kidogo cha Polisi cha Mabatini: "Njia hiyo imefungwa eti kuruhusu ujenzi wa nyumba yake ya ghorofa moja. Unajua mtu hadi agundue kuwa njia hiyo imefungwa, inambidi atembee kama dakika tano hivi ndipo akutane na uzio wa mabati."

Kwa mujibu wa Mbegu, kibao kilichowekwa mwanzoni mwa Mtaa wa Sahara jirani na Kituo hicho cha polisi kuonyesha kuwa barabara imefungwa, nacho kina utata kwani watu wengi wanajua kuwa imefanyika hivyo kwa magari pekee. Alisema kufungwa kwa njia hiyo inayopita jirani na Kiwanja namba 630 katika Kitalu namba 47, kinachomilikiwa na Makinda, kumesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo na vitongoji vyake.

Mkazi mwingine ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema kutokana na kufungwa kwa njia hiyo, watu wanalazimika kuzunguka hadi Barabara ya Shekilango eneo la Afrika Sana, ili kufika eneo la Mori, mwendo ambao ni takriban dakika 45.

Kauli ya uongozi wa Mtaa
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya alipoulizwa jana kuhusu suala hilo alisema hana taarifa ya kufungwa kwa njia hiyo."Sina taarifa na ndiyo kwanza nasikia kwako. Mbona hawajanifahamisha?" alihoji mwenyekiti huyo na kuongeza:"Njia hiyo imekuwa ikitumika pia wakati wa mvua kwani njia inayounganisha ile inayopita katika Kituo Kidogo cha Polisi Mabatini, huwa haipitiki kutokana na ubovu."

Mwenyekiti huyo alisema anachojua ni kuwa Mei mwaka jana, wakazi wa eneo hilo kwa kumtumia Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wao, Athanas Mapunda waliwasilisha maombi ya kutaka kufungwa kwa njia hiyo kwa sababu za kiusalama, ombi ambalo hata hivyo, lilikataliwa.

"Walileta ombi la kutaka hilo lifanyike lakini kikao cha kamati ya maendeleo ya kata kilikataa ombi hilo kwa sababu ni njia pekee katika eneo hilo ambayo inaunganisha maeneo mawili tofauti," alisema.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, aliwashauri watafute jinsi ya kufanya ikiwa ni pamoja na kuweka lango la kuingilia katika mtaa huo na walinzi.

"Pia nilishauri waweke muda wa kupita kwa watu wote na muda wa kupita wenyeji tu. Niliwaambia waweke geti, walinzi na waaandike muda wa mwisho kupita kwa watu wa kawaida lakini siyo kufunga njia."

Mwenyekiti huyo aliahidi kufika katika eneo la tukio kujionea kinachoendelea akieleza kuwa kisheria, kabla ya kufunga barabara hiyo, mmiliki alipaswa kuwasiliana na ofisi yake.

"Ngoja nifike hapo baadaye nitakupigia. Unajua wakati mwingine kuna watu huwa wanatumia njia za mkato kwenda manispaa kuomba vibali bila kushirikisha mamlaka nyingine halali. Huu ni ukiukwaji wa utaratibu na ni kinyume kabisa na misingi ya utawala bora."
Kauli ya Spika
Spika Makinda alipigiwa simu kutoa ufafanuzi wa madai hayo. Hata hivyo, mara baada ya mwandishi kujitambulisha kwake na kabla ya kumweleza lolote alisema: "Naomba niacheni kwanza. Wasiliana na katibu, tafadhali sana."

Alipodokezwa kuwa suala lenyewe halihusu ofisi yake, bali yeye binafsi tena ni kuhusu kudaiwa kufunga barabara na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo, alikata simu.Baadaye Msaidizi wa Spika, Herman Berege alipiga simu na kukiri kufungwa kwa barabara hiyo akisema hatua hiyo imefikiwa kwa sababu za kiusalama na bosi wake alifuata taratibu zote.

Alisema Makinda alipeleka maombi ya kufanya hivyo katika Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni ambako kwa kuwashirikisha maofisa wa mipango miji na watendaji wengine, walikubali kuifunga njia hiyo. Alipoelezwa kauli ya mwenyekiti wa mtaa kwamba maombi hayo yalipelekwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata lakini yakakataliwa, msaidizi huyo wa Makinda alisema si kweli.


"Tulikwenda na hadidu za rejea za kikao kilichopitisha uamuzi wa kufungwa kwa njia hiyo na makubaliano yalikuwa ama yawekwe matuta, ziwekwe nguzo kuzuia magari au uzio. Barabara hiyo ilikuwa lazima ifungwe kuzuia vitendo vya uhalifu."Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Spika Makinda kutaka aishi nyumbani kwake awapo Dar es Salaam badala ya kukaa hotelini kwa gharama za Serikali.

"Lengo la mheshimiwa ni zuri tu, kunusuru pesa ya Serikali ambayo ingetumika kulipia anapoishi," alisema na kuongeza:"Alikopa kutoka taasisi tofauti ili kujenga nyumba hiyo na kulingana na hadhi yake, watu wa usalama waliona kuna haja ya kuifunga njia hiyo."
"Nasisitiza kwamba utaratibu ulifuatwa na kama manispaa hawajaifahamisha serikali ya mtaa, hilo si kosa lake

Message iliyoko kwenye title ya thread ni nzito sana ukilinganisha na thread yenyewe.Hata hivyo kama wewe ni mwandishi wa habari sishangai sana.
 
kwa mkuu mimi sio mwandishi wa habari, mimi ni mtanzania niliyechoshwa na ukandamizaji,
pili hakuna kilichofunguzwa wala kuongezwa, kuna mambo mawili hapo barabara kufungwa na
spika kuokoa pesa ya umma, kitu ambacho ni sahihi lakini serikali ya kikwete na wizara yake ya fedha wao wabaona sawa tu kutumbua pesa yetu hotelini
wakati wa kuuzwa nyumba za watumishi wa umma kikwete alikuwa kwenye baraza la mawaziri na mwandosya, magufuli na marry nagu
lakini leo hao hao wanakwenda kuishi hotelini?
ina maana walipokuwa wakubaliana kuuza hizo nyumba walikuwa na lengo au mpango gani baadaye
?

Message iliyoko kwenye title ya thread ni nzito sana ukilinganisha na thread yenyewe.Hata hivyo kama wewe ni mwandishi wa habari sishangai sana.
 
Back
Top Bottom