Spika Makinda Kaishitukia Serikali Ya Kikwete Haina Huruma na Mtanzania

Fedha gani ameokoa? Kwanini asingekaa palepale alipokuwa anakaa kabla ya kuwa spika badala yake akahamia hotelini? Hivi kweli zile nyumba za serikali ziliuzwa na magufuli? Hapana, yeye alitekeleza maamuzi ya baraza la mawaziri chini ya rais, maamuzi ya pamoja.Hivyo sio sawa kumtupia lawama hizo magufuli, bali wote waliopitisha uamuzi huo. Kwamba magufuli aliwauzia nyumba hizo hawara zake sio tatizo, kwa kuwa hata angemuuzia hawala yako ni sawa tu kwa kuwa suala hapa ni nyumba kuuzwa kutoka mikononi mwa serikali nani alitoa maamuzi hayo?
 
  • Kahamia kwenye nyumba yake Sinza kutoka Hotel alikokuwa anaishi
  • Asema anaokoa pesa ya umma
  • Amewafungia njia wananchi wa Sinza
  • Je matumizi kama haya ni moja ya sababu ya serikali yetu kuwa mufilisi
  • Kwa nini na mawaziri wasirudi kwenye nyumba zao kuepusha gharama kubwa tunazolipa kwa siku
GAZETI MWANANCHI

Makinda azuia watu kutumia barabara

Joseph Zablon

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda anadaiwa kufunga njia inayounganisha eneo la Kijitonyama na Sinza, Dar es Salaam na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji.Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na baadhi ya wakazi wa sehemu hiyo zimeeleza kuwa kutokana na kufungwa kwa njia hiyo, sasa wanalazimika kutumia dakika 45 kufika Sinza kwa miguu badala ya dakika tano hadi 10 walizokuwa wakitumia awali.

Mkazi wa eneo hilo, Juma Mbegu alieleza kuwa njia hiyo imefungwa katika Mtaa wa Sahara, jirani na Kituo Kidogo cha Polisi cha Mabatini: "Njia hiyo imefungwa eti kuruhusu ujenzi wa nyumba yake ya ghorofa moja. Unajua mtu hadi agundue kuwa njia hiyo imefungwa, inambidi atembee kama dakika tano hivi ndipo akutane na uzio wa mabati."

Kwa mujibu wa Mbegu, kibao kilichowekwa mwanzoni mwa Mtaa wa Sahara jirani na Kituo hicho cha polisi kuonyesha kuwa barabara imefungwa, nacho kina utata kwani watu wengi wanajua kuwa imefanyika hivyo kwa magari pekee. Alisema kufungwa kwa njia hiyo inayopita jirani na Kiwanja namba 630 katika Kitalu namba 47, kinachomilikiwa na Makinda, kumesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo na vitongoji vyake.

Mkazi mwingine ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema kutokana na kufungwa kwa njia hiyo, watu wanalazimika kuzunguka hadi Barabara ya Shekilango eneo la Afrika Sana, ili kufika eneo la Mori, mwendo ambao ni takriban dakika 45.

Kauli ya uongozi wa Mtaa
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya alipoulizwa jana kuhusu suala hilo alisema hana taarifa ya kufungwa kwa njia hiyo."Sina taarifa na ndiyo kwanza nasikia kwako. Mbona hawajanifahamisha?" alihoji mwenyekiti huyo na kuongeza:"Njia hiyo imekuwa ikitumika pia wakati wa mvua kwani njia inayounganisha ile inayopita katika Kituo Kidogo cha Polisi Mabatini, huwa haipitiki kutokana na ubovu."

Mwenyekiti huyo alisema anachojua ni kuwa Mei mwaka jana, wakazi wa eneo hilo kwa kumtumia Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wao, Athanas Mapunda waliwasilisha maombi ya kutaka kufungwa kwa njia hiyo kwa sababu za kiusalama, ombi ambalo hata hivyo, lilikataliwa.

"Walileta ombi la kutaka hilo lifanyike lakini kikao cha kamati ya maendeleo ya kata kilikataa ombi hilo kwa sababu ni njia pekee katika eneo hilo ambayo inaunganisha maeneo mawili tofauti," alisema.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, aliwashauri watafute jinsi ya kufanya ikiwa ni pamoja na kuweka lango la kuingilia katika mtaa huo na walinzi.

"Pia nilishauri waweke muda wa kupita kwa watu wote na muda wa kupita wenyeji tu. Niliwaambia waweke geti, walinzi na waaandike muda wa mwisho kupita kwa watu wa kawaida lakini siyo kufunga njia."

Mwenyekiti huyo aliahidi kufika katika eneo la tukio kujionea kinachoendelea akieleza kuwa kisheria, kabla ya kufunga barabara hiyo, mmiliki alipaswa kuwasiliana na ofisi yake.

"Ngoja nifike hapo baadaye nitakupigia. Unajua wakati mwingine kuna watu huwa wanatumia njia za mkato kwenda manispaa kuomba vibali bila kushirikisha mamlaka nyingine halali. Huu ni ukiukwaji wa utaratibu na ni kinyume kabisa na misingi ya utawala bora."
Kauli ya Spika
Spika Makinda alipigiwa simu kutoa ufafanuzi wa madai hayo. Hata hivyo, mara baada ya mwandishi kujitambulisha kwake na kabla ya kumweleza lolote alisema: "Naomba niacheni kwanza. Wasiliana na katibu, tafadhali sana."

Alipodokezwa kuwa suala lenyewe halihusu ofisi yake, bali yeye binafsi tena ni kuhusu kudaiwa kufunga barabara na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo, alikata simu.Baadaye Msaidizi wa Spika, Herman Berege alipiga simu na kukiri kufungwa kwa barabara hiyo akisema hatua hiyo imefikiwa kwa sababu za kiusalama na bosi wake alifuata taratibu zote.

Alisema Makinda alipeleka maombi ya kufanya hivyo katika Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni ambako kwa kuwashirikisha maofisa wa mipango miji na watendaji wengine, walikubali kuifunga njia hiyo. Alipoelezwa kauli ya mwenyekiti wa mtaa kwamba maombi hayo yalipelekwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata lakini yakakataliwa, msaidizi huyo wa Makinda alisema si kweli.

"Tulikwenda na hadidu za rejea za kikao kilichopitisha uamuzi wa kufungwa kwa njia hiyo na makubaliano yalikuwa ama yawekwe matuta, ziwekwe nguzo kuzuia magari au uzio. Barabara hiyo ilikuwa lazima ifungwe kuzuia vitendo vya uhalifu."Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Spika Makinda kutaka aishi nyumbani kwake awapo Dar es Salaam badala ya kukaa hotelini kwa gharama za Serikali.

"Lengo la mheshimiwa ni zuri tu, kunusuru pesa ya Serikali ambayo ingetumika kulipia anapoishi," alisema na kuongeza:"Alikopa kutoka taasisi tofauti ili kujenga nyumba hiyo na kulingana na hadhi yake, watu wa usalama waliona kuna haja ya kuifunga njia hiyo."
"Nasisitiza kwamba utaratibu ulifuatwa na kama manispaa hawajaifahamisha serikali ya mtaa, hilo si kosa lake
Hongera Kwa uamuzi wa Makinda japo siku zote maamuzi yenu yasiwaumize wengine kitendo
cha kufunga njia tayari unaleta usumbufu kwa nini usikae kwenye Moja ya Magorofa yako pale Msasani jirani na Mwalimu ili kuepusha usumbufu ukizingatia hakuna idadi kubwa ya Watu hapo au unaona bora upangishe na ww ukawasumbue walalahoi Sinza.
 
hawezi kwenda kukaa hapo tutamuuliza alipata wapi pesa?
wengi wana nyumba nzuri ila walizijenga kwa pesa chafu
dawa ni kutaja ziliko,
wanajifanya malofa hali wanalipwa mamilioni kila mwezi

Hongera Kwa uamuzi wa Makinda japo siku zote maamuzi yenu yasiwaumize wengine kitendo
cha kufunga njia tayari unaleta usumbufu kwa nini usikae kwenye Moja ya Magorofa yako pale Msasani jirani na Mwalimu ili kuepusha usumbufu ukizingatia hakuna idadi kubwa ya Watu hapo au unaona bora upangishe na ww ukawasumbue walalahoi Sinza.
 
Barabara iliyofungwa na Spika Makinda yafunguliwa
Sunday, 15 May 2011
Joseph Zablon
BARABARA iliyokuwa imefungwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda katika eneo la Kijitonyama, Dar es Salaam, imeifunguliwa.Barabara hiyo inayounganisha maeneo ya Sinza na Kijitonyama ambayo inapita nje ya nyumba anayoijenga imeanza kupitika jana lakini ulinzi umeimarishwa katika eneo hilo.

Makinda alifunga barabara hiyo na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na watumiaji wengine kwa kile kilichodaiwa kuwa sababu za kiusalama.

Barabara hiyo imefunguliwa siku moja baada ya gazeti hili kuripoti kufungwa kwake. Kibao kilichokuwa kinaonyesha kuwa imefungwa, kimeondolewa.Mwandishi wa gazeti hili alifika katika eneo hilo na kukuta kibao cha kuifunga kikiwa kimeondolewa lakini ulinzi wa askari polisi ukiwa umeimarishwa

“Kaka weka kamera yako katika mkoba, picha hairuhusiwi eneo hili. Askari wa doria wakikukuta na hiyo kamera hapa huenda ukapata matatizo," alisema msamaria mwema mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina na kuongeza kuwa polisi wamekuwa wakifanya doria eneo hilo usiku na mchana.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya alisema barabara hiyo imefunguliwa jana ingawa alidai kuwa suala hilo limemletea matatizo.“Habari za huku mbaya, hali si shwari na ile barabara imefunguliwa,” alisema.

Komanya alisema hali katika mtaa wake si shwari kuhusiana na suala hilo akidokeza kwamba juzi alikuwa na kikao na wajumbe wake wa Serikali za Mitaa lakini hakutaka kueleza kwa undani walichojadili.

Hatua ya kufungwa kwa barabara hiyo ililalamikiwa na wakazi wa eneo hilo na wengine waliokuwa wakiitumia kwa kuwa iliwalazimu kuzunguka hadi Barabara ya Shekilango eneo la Afrika Sana ili kufika eneo la Sinza Mori kwa kutumia takriban dakika 45 badala ya kati ya dakika tano mpaka 1o kupitia hapo.

Alhamisi iliyopita gazeti hili lilimkariri Komanya akisema Mei mwaka jana wakazi wa eneo hilo kwa kumtumia mjumbe wa serikali ya mtaa wao, Athanas Mapunda, waliwasilisha maombi ya kutaka kufungwa kwa njia hiyo kwa sababu za kiusalama ombi ambalo lilikataliwa.

Hata hivyo, Msaidizi wa Spika, Herman Berege alisema kuwa bosi wake alifunga barabara hiyo baada ya kufuata taratibu zote.Alisema Makinda alipeleka maombi Manispaa ya Kinondoni ambako kwa kuwashirikisha maofisa wa mipango miji na watendaji wengine walikubali kuifunga njia hiyo.

Alisema: "Barabara hiyo ilikuwa lazima ifungwe kuzuia vitendo vya uhalifu."Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Spika Makinda kutaka aishi nyumbani kwake awapo Dar es Salaam badala ya kupangishiwa na serikali hotelini."Lengo la mheshimiwa ni nzuri tu, kunusuru pesa ya serikali ambayo ingetumika kulipia anapoishi," alisema.


maoni yangu : media muhimili wa nne na nguvu yake ni dhaili hapa,
viongozi wetu ni wa binafsi na wakurupukaji hawana uzalendo wala kujali jamii inayowazunguka
peopleeeeeeee powerrrrrrrrr
 
Hana lolote sasa kwanini afunge njia kama anauchungu na wananchi wa nchi hii? usalama gani nani anashida nae....ukute anajiongezea umaarufu ili na yeye aje agombee uraisi wa nchi hii gombaniwa na viongozi wabovu...
 
kumbe njia haikufunduliwa

Mipango Miji yambana Spika afungue barabara
Spika wa Bunge, Anne Makinda
Joseph Zablon
MWENYEKITI wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira Manispaa ya Kinondoni, Abbas Tarimba ametaka barabara iliyofungwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda ifunguliwe akisema hakuna mwenye mamlaka ya kujenga juu ya barabara.

Akizungumza baada ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika juzi, Tarimba alisema siyo sahihi kwa barabara hiyo inayounganisha eneo la Kijitonyama na Sinza kufungwa.

“Unaweza kuifunga barabara kwa muda tu, ama kwa kuwa unajenga au kuna tatizo la kijamii kama vile msiba au kitu kingine cha namna hiyo,” alisema Tarimba akisisitiza kuwa hata mambo ya namna hiyo yana taratibu zake.
Tarimba alisema hakuna mtu ambaye ana mamlaka ya kuifunga barabara moja kwa moja kisha akafanya ujenzi katika eneo hilo la njia.

Alisema ingawa suala hilo halikuwa ajenda ya kikao cha kamati yake, walilijadili baada ya kuwasilishwa na Diwani wa Kata hiyo, Ulole Juma Athuman.

licha ya kusema kwamba kitendo cha kuifunga barabara hakikuwa sahihi, alimtaka diwani huyo kuwa na subira huku akimsihi kutoitisha mkutano wa wananchi kama alivyoahidi.

“Najua anataka kutumia ile ‘people’s power’ (nguvu ya umma) lakini nimemtaka awe na subira kwanza wakati suala hilo linashughulikiwa,” alisema Tarimba.hata hivyo, Diwani huyo alisema kuwa dhamira yake iko palepale huku akitangaza kuitisha mkutano wa wakazi wa eneo Jumapili jirani na eneo la tukio.

Alisema amechukua hatua hiyo kwa kuwa kinachoonekana ni kutupiana mpira baina ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Manispaa ya Kinondoni, huku wananchi wanaoendelea kupata adha wakidai majibu kutoka kwake. “Walinituma kulalamikia hali ya kufungwa kwa barabara hiyo, nimeleta malalamiko kunakohusika. Hatua za maana zisipochukuliwa, nalirudisha jambo hili kwao waamue,” alisema Ulole.

Diwani alisema haoni sababu ya kuendelea kusubiri wakati sheria na taratibu zipo wazi:
“Hivi kama ningekuwa mimi ndiye nimeziba barabara, hadi sasa wangekuwa wanajadili kweli jambo hilo?” Alihoji na kuongeza kuwa anarudisha majibu kwa mabosi wake ambao ni wananchi siku hiyo ya Jumapili.

Alisema kwamba wananchi wanaitafsiri hatua ya kufungwa kwa barabara hiyo kama ni kuporwa kipande cha ardhi ya barabara na kugeuza kuwa ni sehemu ya kiwanja cha kiongozi huyo jambo ambalo linawapa adha kubwa wakazi wa eneo hilo na lile la jirani.

“Safari ya dakika tano kutoka Kijitonyama kwenda Sinza leo unaifanya kwa dakika zaidi ya 45, kisa! Barabara imefungwa na mtu mmoja kwa matakwa yake. Hiyo haiwezekani,” alisema.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda alisema kuwa suala hilo limeshatoka kwake na lipo mikononi mwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema juzi kuwa baada ya ofisi yake ilichunguza sababu za kiusalama ambazo zimetajwa kuchangia kufungwa kwa barabara hiyo, ilibaini kuwa hazipo.

“Nilijaribu kuwasiliana na ngazi za juu kidogo pengine kulikuwa na maagizo yoyote ya kiusalama, lakini hakuna kitu kama hicho hivyo suala hilo wanalo wenyewe manispaa,” alisema Rugimbana.Spika alifunga barabara hiyo inayopita jirani na nyumba anayojenga katika kiwanja namba 630 Kitalu 47, mnamo Mei 13, mwaka huu kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni za kiusalama.
 
MANISPAA ya Kinondoni imemwomba diwani wa Kata ya Kijitonyama, Ulole Athuman kuahirisha mkutano na wakazi wa eneo hilo kujadili na kuchukua uwaamuzi kuhusiana na kufungwa kwa barabara inayounganisha Sinza na Kijitonyama kulikofanywa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda.
Akizungumza na Mwananchi jana, diwani huyo alisema mkutano huo umeahirishwa baada ya kuombwa kutoa muda zaidi wa kushughulikia suala hilo ambalo limewaletea adha kubwa wakazi wa eneo hilo na vitongoji vyake ambao walikuwa wakitumia barabara hiyo.

Diwani alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji ya Manispaa Kinondoni, Tarimba Abbas alimwomba kutoa muda za siku nyingine mbili ili wakamilishe utaratibu wa kufikisha uwamuzi uliofikiwa na manispaa hiyo dhidi ya Spika Anne Makinda kwa ajili ya utekelezaji.

“Tarimba kaniomba niwape siku mbili zaidi nami kwa kuwa ni sehemu ya manispaa nimekubali ombi hilo, hivyo tumeamua kuahirisha mkutano huo”alisema na kuongeza kuwa hakutakuwa na muda zaidi baada ya hapo na ana matumaini kuwa manispaa itazitumia vizuri siku hizo mbili walizotaka.

Wiki iliyopita, mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira Manispaa ya Kinondoni, Abbas Tarimba alitaka barabara iliyofungwa hiyo ifunguliwe kwa kuwa hakuna ambaye ana mamlaka ya kujenga juu ya barabara.

Tarimba aliimbia Mwananchi kuwa kikao cha kamati hiyo kimeona si halali kwa barabara hiyo inayounganisha eneo la Kijitonyama na Sinza kufungwa. Alisema barabara inaweza kufungwa kwa muda tena kwa kufuata taratibu husika na inaweza kuwa kwa sababu za kiusalama kwamba kuna ujenzi unaendelea au shughuli za kijamii.

Tarimba pia alimwomba kuwa na subira na asiitishe mkutano wa wananchi kama anavyotaka. Hata hivyo, taarifa zilizopatikana wakati tunakwenda mitamboni zinaeleza kuwa diwani huyo wa Kijitonyama alikamatwa na polisi na kuhojiwa kufuatia taarifa za kuandaa mkutano huo wa wananchi.
 
hata nyoka huvua gamba, lakini haachi kuwa nyoka! Tena sumu ile ile!

ubinafsi , ubinafsi, ubinafsi na ubinafsi ndio unaimaliza ccm na serikali yake...

Hainiingii akilini spika wa bunge, anayepika sheria za nchi, kwenda kinyume na sheria, kwa kitendo cha kuwafungia njia maelfu ya wananchi ili kulinda maslahi yake tu! Kwa nini asiombe ulizi kutoka kwa serikali iliyomwingiza madarakani?
Je ingalikuwa ni mwananchi wa kawaida kaifunga njia hiyo - kauli za kuweni na subira zingesikika?

Wananchi wenzangu poleni sana ... Ila tukumbuke kuwa ndani ya serikali ya ccm wanyonge hatuna watetezi..... Hivyo tuwakatalie hata na blabla zao wanapohitaji supporti zetu wananchi

watundawangu.
 
Hali hii imeonyesha Spika alivyokuwa limbukeni wa madaraka makubwa. Kupata uspika basi yeye anadhani watanzania tutamdhuru!!!
 
worse!and i wonder how should we put confident on her in executing our parliament if she fails on this simple resoning in weighing out her pesonal interest out of public interest. we need to the leader who at least have beautif minds to serve and deliver public interest first.
 
Back
Top Bottom