Spika Makinda awachefua Wazee wa Kibena na Njombe

ccm wao wanasema wako juu ya mamlaka ya Mungu mkuu huoni wanaua, wanaiba hela, wanafanya wanavyotaka kwa kifupi hawa jamaa wako juu sana ila kila kitu kina mwanzo na mwisho

Ewaa,kwa ufupi ni kwamba hawamhitaji Mungu,Ni wajenzi huru,Freebuilders or Freemasons au labda mawakala wao.
 
Mkuu we nikaribishe tu hapo kwa babu tale nije nile kuku choma,au kama vipi tuende kwa macheche .
 
huyu mama si ndiye member wa frustrated group ya wabunge maskini wa kutupwa!!!
aise Njombe fanyeni kweli 2015 siyo kutudanganya hapa!
 
Kipimo cha kwanza cha uwezo wa kuongoza katika jamii ni jinsi mtu alivyofanikiwa kusimamia familia yake. Kama hana familia mlimpimaje hata kumpa ubunge na baadaye kupewa uspika?
Rushwa ya rubisi,vi elfu mbili mbili na ndumba ndio mategemeo ya magamba kupata cheo,ila sasa njia zote hizi zitapigwa ban ndio watakapojampa
 
Mnataka Spika Anna Makinda aongozaje jamani? Anaongoza kwa kufuata matakwa ya waliomuweka. Hivyo tusitegemee jambo jipya toka kwa huyu mama mkongwe kisiasa na ukongwe wake ukawa hautusaidii watanzania tulio wengi badala yake unawasaidia MAFISADI WALIOMPATIA RUNGU, awakoseshe haki walio wengi. Inasikitisha sana. Bunge limekuwa kama kijiwe
 
Wana-JF,
Nipo hapa Njombe mjini mitaa ya Chaugingi karibu kabisa na Sangamela Bar (Talley)sasa nimekutana na wazee wawili wastaafu waliokuwa wanafuatilia mijadala inayoendelea bungeni. Jambo lisilo la kawaida ni kwamba wanamlaani sana mbunge wao Anne Makinda kuwa anawaaibisha Wabena hasa kwa kutoonyesha hulka ya unyenyekevu ambayo ni desturi ya Wanawake wengi wa Njombe kwenye kusimamia ukweli. Wanasema ubabe na hasira za kipuuzi anazoonyesha ktk kupindisha maudhui ya msingi wa hoja wanasema ni aibu kwa Wabena wote kwani litabaki kwenye vitabu vya historia. Wanasema wameshangazwa na kauli za kumkemea waziri Muhongo huku ukweli uko wazi kwamba kuna biashara haramu iliyokuwa ikifanyika kati ya TANESCO na baadhi ya wabunge wa Kamati ya nishati!

waambie wamuoe atulie vinginevyo hataacha ubabe
 
Makinda mzinguzi sana,kuhusu kuolewa hayo ni maisha yake hayatuhusu atajua mwenyewe !
 
Kipimo cha kwanza cha uwezo wa kuongoza katika jamii ni jinsi mtu alivyofanikiwa kusimamia familia yake. Kama hana familia mlimpimaje hata kumpa ubunge na baadaye kupewa uspika?

Kweli usilolijua ni kama usiku wa giza!! Aliyekwambia kuwa Makinda hana familia ni nani? Makinda hapo alipo ana binti yake wa kike anayeishi kwa Obama na hapo alipo ni BIBI yaani ana wajukuu!! Kaeni kimya msiseme mambo msiyoyajua!!
 
By Zimamoto<br />
Kipimo cha kwanza cha uwezo wa kuongoza katika jamii ni jinsi mtu alivyofanikiwa kusimamia familia yake. Kama hana familia mlimpimaje hata kumpa ubunge na baadaye kupewa uspika?
<br />

Wa kufikia au?Kuwa na familia sio kigezo cha kupewa ubunge,kina Zitto,Halima Mdee,Nassari wana familia wale?!
 
Hao wazee wawili wa Njombe, hawawezi kuwa ndo kipimo cha wana Njombe wote juu ya Mbunge wao. Nimekuwepo Njombe hali halisi ni kwamba kwa ujumla watu wanataka mabadiliko. Lakini mabadiliko thabiti yanahitaji maandalizi yaliyoratibiwa vilivyo. Kazi kubwa bado inahitajika kufanyika hususani vijijini ili pamoja na mabadiliko wanayoyataka ni vyema wakaelewa mwelekeo ni upi wenye kuleta matumaini kwa maisha yao.
 
Kweli usilolijua ni kama usiku wa giza!! Aliyekwambia kuwa Makinda hana familia ni nani? Makinda hapo alipo ana binti yake wa kike anayeishi kwa Obama na hapo alipo ni BIBI yaani ana wajukuu!! Kaeni kimya msiseme mambo msiyoyajua!!

"anabinti yake wa kike?"
Kumbeeee!
 
Tunaomba hoja za msingi. mambo ya familia ni yake na familia yake kwao.
Kama hakuna hoja za msingi ni bora usiandike kitu.
 
Kipimo cha kwanza cha uwezo wa kuongoza katika jamii ni jinsi mtu alivyofanikiwa kusimamia familia yake. Kama hana familia mlimpimaje hata kumpa ubunge na baadaye kupewa uspika?

Kweli we zimamoto! inaama wagumba aka tasa na wengine wasiopenda kuwa na familia ima kwa hiari au viapo vya useja hawawezi kuongoza? vipimo vya kichawi hivo havitumiki dunia ya sasa
 
maeneo yenyewe uliyokutana nao ni karibu na bar!!labda tayari wapikuwa wameshalewa!!
 
sasa nani mwenye nafuu kati ya anna na ndugai? nadhani kwa wazee wawili tu kutoa dukuduku zao juu ya spika si ishara ya kukataliwa chama na watu wote katika mkoa huo
 
Back
Top Bottom