Spika aondolewa ulinzi

Kuna wakati kulitokea tafrani na wananchi jirani na nyumba ya huyu mama baaada ya kuwa amejenga na kuziba njia ya wananchi. Bila shaka aliomba ulinzi ili kuzuia mob justice dhidi ya nyumba yake. Ni sahihi kama sasa kama hali sasa ni shwari hasa baada ya Jiji kuingilia kati na kumtaka arekebishe na kuruhusu njia hiyo ipitike.
 
Sijajua mpaka sasa tafsiri yake ni nini, lakini lililotokea ni kwamba wale askari wa FFU waliokuwa wanailinda nyumba ya Mh. Spika wetu kipenzi wamepewa amri ya kuondoka na kuacha lindo hilo la nyumba binafsi ya Mh. Spika.

Kwa barua waliyosomewa Askari hao ni kwamba kwa sasa Mh. Spika inabidi ajitafutie walinzi binafsi wa kuendelea kutoa ulinzi nyumbani kwake eneo la Kijitonyama Dar es Salaam.

Source:
Ni rafiki yangu ambaye mdogo wake ni mmoja wa Askari waliokuwa wanailinda nyumba ya Mheshimiwa.
Kipenzi chenu we na nani? acha kujibaraguza
 
fafanua unamaanisha makinda au mzee sitta maana ndio spika kipenzi.
..Sasa na wewe unachanganya mambo hapa kwa hiyo statement yako nani kipenzi hapo unadhani?........hako kabibi acha tu wakaondolee ulinzi si kalitaka eti kutufungia barabara kisa anataka kujenga ka-ghorofa....Kuna wamasai kibao anaweza kuwarundika tu pale kwake!!
 
Mimi Huwa nashangaa na kusikitika sana!! Hata watu ambao hawana Faida yoyote katika Taifa wanapewa Ulinzi!! so What?? Bora wameliona Hilo!!
 
Kwani ile barabara ya kwenda kwa Spika ishamalizika? Maana ile benz yenye plate number S naona kama ilikuwa inakuwa inapata taabu sana pale kwenye ingilio la Barabara ya kuja Sayansi.
 
Back
Top Bottom