DAR: Afisa Afya Buguruni ashtakiwa kwa Ubadhirifu wa Tsh. Milioni 62

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,617
Shauri la Uhujumu Uchumi namba 534/2024 - Jamhuri dhidi ya Bw. Renatus Anatory Rwehabura-Afisa Afya wa Kata ya Buguruni katika Halmashauri ya Manispaa Ilala limefunguliwa Januari 10, 2024 mbele ya Mhe. Rehema Lyana (SRM) katika Mahakama ya Wilaya Ilala.

Mshtakiwa ameshtakiwa kwa kosa la Ubadhirifu na Ufujaji wa fedha kiasi cha Tsh. 62,292 000/= kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA 329 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi, Sura ya 200, R.E 2022.

Mshtakiwa amekana kosa na kupelekwa mahabusu baada ya kutokukidhi masharti ya dhamana.

Kesi imeahirishwa hadi Januari 24, 2024 kwa ajili ya kusoma Hoja za Awali.

Chanzo: TAKUKURU
 
Daah Takukuru ingefutwa tuu tupate Taasisi itakayosimamia wezi wa Fedha za Umma sio hawa wapo busy na rushwa za elfu kumi mahamani mara upotevu wa chaki shuleni huku majambazi makubwa yakiachwa huko...
 
Ninajaribu kupiga picha hadhi ya Afisa Afya wa Kata (Siyo Jiji) na kiasi cha pesa anachodaiwa lakini sipati jibu.

Afisa Afya wa Kata ana fungu? Labda uniambie Mganga Mkuu wa Kata.

Kuna kesi nimewahi kuikuta makamani ambapo Afisa Mazingira alikuwa na kesi ya rushwa.

Taarifa za nje ya Mahakama ni kwamba Afisa Mazingira huyo aliwahi kumpiga fine Afisa TAKUKURU kuhusu uchafuzi wa mazingira, hivyo jamaa wa TAKUKURU akaamua kumkomoa jamaa wa Mazingira.

Niliusoma mwenendo wa ushahidi nikagundua kwamba ni ushahidi wa kubumba, na kwa kuwa nilikuwa kwenye nafasi ya kuandika hukumu ile, nilimuachia huru Afisa Mazingira kwa kuainisha matobo ya ushahidi uliotolewa.

Ukiona mwenzako kafunguliwa kesi usikurupuke kuhukumu. Dunia ina mambo!
 
ILi nalo likaangaliwe upya
Kuna habari kwenye Jukwaa moja la jamii forum linahabarisha yakuwa Afisa Afya wa kata ya Buguruni amefunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi na kufikishwa mahakamani na amekana kosa na kurudishwa mahabusu kwa kutokidhi vigezo vya dhamana.

Je watanzania mmerogwa na nani?yaani Mpaka Afisa Afya wa Kata nae anawapiga?
 
Kwani maafisa afya wao ni malaika?
 
ILi nalo likaangaliwe upya
Kuna habari kwenye Jukwaa moja la jamii forum linahabarisha yakuwa Afisa Afya wa kata ya Buguruni amefunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi na kufikishwa mahakamani na amekana kosa na kurudishwa mahabusu kwa kutokidhi vigezo vya dhamana.

Je watanzania mmerogwa na nani?yaani Mpaka Afisa Afya wa Kata nae anawapiga?
Kwani imeshathibitishwa ameiba? Hii ni tuhuma tu kama ambavyo naweza kukutuhumu kwamba umeiba mke wa mtu kwa sababu sikupendi tu.
 
ILi nalo likaangaliwe upya
Kuna habari kwenye Jukwaa moja la jamii forum linahabarisha yakuwa Afisa Afya wa kata ya Buguruni amefunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi na kufikishwa mahakamani na amekana kosa na kurudishwa mahabusu kwa kutokidhi vigezo vya dhamana.

Je watanzania mmerogwa na nani?yaani Mpaka Afisa Afya wa Kata nae anawapiga?
Hiki siyo kipindi Cha jpm ambapo yeye ndo alikuwa mahakama na pia rais. Tuhuma siyo uthibitisho Bali ni tuhuma na itabaki kuwa tuhuma untill proven beyond reasonable doubt. Ingekuwa enzi zile za Giza tayari tuhuma ingekuwa kosa
 
Ninajaribu kupiga picha hadhi ya Afisa Afya wa Kata (Siyo Jiji) na kiasi cha pesa anachodaiwa lakini sipati jibu.

Afisa Afya wa Kata ana fungu? Labda uniambie Mganga Mkuu wa Kata....
Nilitamani sana kujua sana hizo pesa Mil 62 zimefika vipi kwenye mikono ya Afisa Afya wa Kata, hii habari ikamilishwe vizuri!!! Kwani hawa watu wanakuwa na mafungu!?
 
Nilitamani sana kujua sana hizo pesa Mil 62 zimefika vipi kwenye mikono ya Afisa Afya wa Kata, hii habari ikamilishwe vizuri!!! Kwani hawa watu wanakuwa na mafungu!?

Changamoto wa wandishi wetu huwa hawatoi mwendelezo wa habari.

Wana mtindo wa kuruka ruka
 
Back
Top Bottom