ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
DUUU!! umenikumbusha mbali..hususan hilo Ford ambalo kwa wakati huo lilikuwa linaendeshwa na dereva mtanashati -maarufu dereva Ally. Gari hilo lilikuwa maarufu songea kwa vile lilikuwa linabeba wanandinga wa box 2 ambao katika miaka ya 70 hadi mwanzoni mwa 90 shule hiyo ilikuwa ndiyo club bingwa ya mkoa...Du sijui pale kwa Chenjela bado hai! maana viazi na mihogo ya pale vilikuwa vinasupplement diet hasa ya wanafunzi waliokuwa wanaishi katika mabweni ya Nile, Niger na Congo.
Kibu ulikuwa Kaigo nini wale Tamsala,Tamso majina yalikuwa yanageuka kutokana na nyakati kwani Songea Girls wanafunzi wa kwanza waliletwa kutoka Msalato ,baadaye wakaja wale ambao hawakuhamia ndio Tamso loo kaka machozi yananitoka nikikumbuka disco la box 2 na Tamsala ,huku box kulikuwa na wanaume wa ukweli, na kule Tamsala kulikuwa na wanadada wa ukweli,ingawa wachezaji wa majimaji walikuwa watuzidi kwa kuopoa kwa kuwa walikuwa na vijisenti ilihali sisi mtaji mkubwa ulikuwa Mali kauli,unaimbisha wee unapata mzigo baada ya mwezi ,ukipata hela ya kwenda chamber unakuwa huna inabidi uahirishe gameMademu wenu wa Songea Girls nao wapo kwenye FB?
Kapongo hapo kwenye RED pamenivunja mbavu ,naam diet ya mbufu,kuna siku kwenye disco na tamsala kuna dada alikuwa anaringa sana,na alwahi kuwaita wana box 2 NATO (ukitaka kuwaudhi box 2 waite NATO)alimwagiwa mustini mzima wa mchuzi mbufu ilibidi disco alikose akae kwenye gari hadi saa nane usiku(enzi hizo disco lilikuwa usiku kabla hali ya hewa haijachafuka)DUUU!! umenikumbusha mbali..hususan hilo Ford ambalo kwa wakati huo lilikuwa linaendeshwa na dereva mtanashati -maarufu dereva Ally. Gari hilo lilikuwa maarufu songea kwa vile lilikuwa linabeba wanandinga wa box 2 ambao katika miaka ya 70 hadi mwanzoni mwa 90 shule hiyo ilikuwa ndiyo club bingwa ya mkoa...Du sijui pale kwa Chenjela bado hai! maana viazi na mihogo ya pale vilikuwa vinasupplement diet hasa ya wanafunzi waliokuwa wanaishi katika mabweni ya Nile, Niger na Congo.
Du! Mmenikumbusha mbali saaana. Nimelikumbuka hilo kwama la shule ambalo tulikuwa tunalitumia usiku kupeleka wagonjwa hospitalini na kwenda kaigo, maposeni, paramiho na Ruvuma kwenye mpira na debate. Nimeona mabweni ya Azimio na uhuru na vitanda vyetu vya madeka. Sikuona tu Ukumbi wa misosi na mikutano ambako maharage ya binga yalikuwa yakitumika. Sikuona mashamba ya mahindi, maharage na malegea. Mimi nilikuwepo huko enzi za utawala wa Mzee Mbao. Walikuwepo akina Mwanyigu, HP wa Mkinga, Ndimbo, Mwihava, Marehemu Mahinya, Maunga na Clamp.
Du! Mmenikumbusha mbali saaana. Nimelikumbuka hilo kwama la shule ambalo tulikuwa tunalitumia usiku kupeleka wagonjwa hospitalini na kwenda kaigo, maposeni, paramiho na Ruvuma kwenye mpira na debate. Nimeona mabweni ya Azimio na uhuru na vitanda vyetu vya madeka. Sikuona tu Ukumbi wa misosi na mikutano ambako maharage ya binga yalikuwa yakitumika. Sikuona mashamba ya mahindi, maharage na malegea. Mimi nilikuwepo huko enzi za utawala wa Mzee Mbao. Walikuwepo akina Mwanyigu, HP wa Mkinga, Ndimbo, Mwihava, Marehemu Mahinya, Maunga na Clamp.
Duh!! Kumbukumbu zako ni sahihi. Form Five unakaribishwa na uvunaji wa marejea, kidogo niingie chaka, sikujua kama ni bonge la skuli. Ila umemsahau mzee wa dispensary anaitwa Kidato. Hilo Isuzu tulikuwa tunaliita Mustini. Mdau hajatutendea haki kuiacha picha ya bwalo letu na uwanja wetu wa Basketi wenye sakafu ya matofali. Nakumbuka maji yakikatika tulikuwa tunakwenda kuoga chemchem.
Nakumbuka vijana waliokuwa wakitoka kusini tulikuwa tunawaita Mawia. Tulikuwa tukishinda Mbuzi ya ligi ya mabweni wanakula mpaka ngozi ya mbuzi. Vyoo vya DANIDA tulikuwa tunaviita Milango, ukitaka kwenda ni lazima uvue nguo zote la sivyo hautaweza kukaa na wenzako tena maana utakuwa unanuka mavi.