Songea boys

Wee mchokozi sana, umenikumbusha mambo mengi hasa lile bweni, nimekiona kitanda changu, siku moja hokololo akiwa mwalimu wa zamu alitushukia alfajiri kutuamusha kwa bakora eti alikuwa anajiita bulldozer. Vipi ugali na small mbofu?


Kwani mzee ulikuwa Azimio? Maana siku huyo naikumbuka sana
 
Duh!! Kumbukumbu zako ni sahihi. Form Five unakaribishwa na uvunaji wa marejea, kidogo niingie chaka, sikujua kama ni bonge la skuli. Ila umemsahau mzee wa dispensary anaitwa Kidato. Hilo Isuzu tulikuwa tunaliita Mustini. Mdau hajatutendea haki kuiacha picha ya bwalo letu na uwanja wetu wa Basketi wenye sakafu ya matofali. Nakumbuka maji yakikatika tulikuwa tunakwenda kuoga chemchem.

Nakumbuka vijana waliokuwa wakitoka kusini tulikuwa tunawaita Mawia. Tulikuwa tukishinda Mbuzi ya ligi ya mabweni wanakula mpaka ngozi ya mbuzi. Vyoo vya DANIDA tulikuwa tunaviita Milango, ukitaka kwenda ni lazima uvue nguo zote la sivyo hautaweza kukaa na wenzako tena maana utakuwa unanuka mavi.

Tehe tehe tehe, kweli leo nimekwenda mbali sana baada ya kuona school langu. Kiukweli nakumbuka nikiwa njuka 1993 mtu fulani akiwa form 6 alinitupia taulo baada ya jamaa kutaka kutufanyia kitu mbaya.

Yaani kama namuona mwl Mwanja akisisitiza kukata nyasi za ng'ombe halafu naona msululu wa ndoo kisimani kwa ajili ya kupeleka jikoni umbali takribani 0.8km toka jikoni hadi kisima kilipo.

Nilikwenda kuchukua cheti kipindi fulani nilikuta shule imechoka lakini leo nilivyoiona katika picha kidogo inaonyesha kuna kaukarabati.

Waruhula mpoooooooo?

 
Mzee umesahau vyoo vya Danida watu tulikuwa mpaka tunalia bondo! Vyoo vya kuvua nguo na kuziba pua vilikuwa vinaitwa milango saba. Pale ilikuwa nguo unaziacha umbali kama wa mita mia. Ukitoka unatoka mbio ili usitoke na upepo wa milango saba. Mawia we acha tu walikuwa moto wa kuotea mbali. Wengi wao walikuwa o'level. Siku ya punga walikuwa wanaruka mpaka juu ya meza! Du hizi srori raha kweli. (TWO MAMBO?- Hivi yuko wapi siku hizi?). (Na mzee wa kuchota?)


M

Mzee usinkumbushe, enzi za chingambo mayao ndiyo yalikuwa kimbilio letu. Tshs 20 unapata mayao yako mane unapeta baadae unajiandaa na dona la saa tisa kabla ya kwenda kulipia saa kumi.

 
huyu mzee mbao nafikiri ndio alihamia mkwawa high school,

Nakumbuka mwaka 1994 tuligoma kabla ya mashule mengine nayo kugoma kutokana na kulishwa chakula kibaya huyo HM Mbao alitokota sana. Ingekuwa siku hizi tungemwita fisadi kutokana na kitambi alichokuwanacho.
 
Nyerere aliona mbali sana katika kujenga Utaifa, ni jambo la kujivunia kuona watu kutoka makabila mbalimbali na dini tofauti wakitafutana na kuzungumza kama familia moja...RAHA SANA!!
 
Mwanangu nilikuwepo pale 1999-2001, nakumbuka siku tulipochinja Bull, jamaa waliiba nyama na kwenda kuchoma. Mwalimu mwanja alikuwa Mnoko kweli. Mwalimu Deo alikuwa anatuingiza chaka kwenye Physics. mkumbukene Mwalimu Maps ( Marehemu kwa sasa), Madam wa Biology Adv yuko wapi?
 
Dah..! BOX 2...thanks guys kwa kunikumbusha mbali!!nilipita hapo 2000-2002....
Mustini...sitolisahau hili lori, wakati nakaribia final paper form6 niliumwa mbaya, liliniwahisha regional hospital hili kwa matibabu...
MAPS...leo baada ya kuiona hii thread ndio nimejua kwa alifariki. Alinikunja one day pale town wkt nipo na mtamsala sina uniform.RIP Maps!!
Mama wa biology advance...nimemsahau jina, but last time i mate her pale azania,ndipo anafundisha......sitomsahau huyu mama ktk life yangu...nimekuwa mtu muhimu ktk fani yangu kutokana na misingi yake..!
I learned a lot pale mahali....HAKUNAGA
 
Dah..! BOX 2...thanks guys kwa kunikumbusha mbali!!nilipita hapo 2000-2002....
Mustini...sitolisahau hili lori, wakati nakaribia final paper form6 niliumwa mbaya, liliniwahisha regional hospital hili kwa matibabu...
MAPS...leo baada ya kuiona hii thread ndio nimejua kwa alifariki. Alinikunja one day pale town wkt nipo na mtamsala sina uniform.RIP Maps!!
Mama wa biology advance...nimemsahau jina, but last time i mate her pale azania,ndipo anafundisha......sitomsahau huyu mama ktk life yangu...nimekuwa mtu muhimu ktk fani yangu kutokana na misingi yake..!
I learned a lot pale mahali....HAKUNAGA
Uhuru 2...dah, was so funny!
Vp matogolo wajameni?
 
Nilikuwepo pale 2002-2005 o'level,Mtaliban na Conja ndo walikuwa role model wangu teh teh
 
mmmmm....... 2000-2002
haaaa, kuna siku MAPS aliibuka saa nane ya usiku pale UHURU 2 huku yuko tungi..... aliaamsha wanafunzi wote.....mimi nilikuwa bado nimelala kile kitanda cha minyonyororo nikiingia kinakuwa level....hakuniona!!! kuja kushituka anamwaga mikwara...loooooo!!!!!!!
 
Duuuh Box 2,nami nimekumbuka mbali.Nilihamia pale mwaka 1994 nikiwa form one na kumalizea 1997. RIP Maps. Hutu Maps aliwahi kunipa adhabu ya fimbo na kung'oa visiki kisa eti kwa nini nimenyoa upara kama huu anaonyoaga January Makamba.Mpaka leo nikikumbuka kama kunyoa upara ni kosa nashindwa kupata jibu kwani mpaka sasa licha ya nafasi kubwa niliyonayo kwenye Serikali hii ya kifisadi lakini bado upara ndio hair style yangu!!!
Nilikuwa Azimio 4,daah kipindi hicho nilikuwa navuta NDUMU balaa,hakika ujana ni maji ya moto!!!nakumbuka nikiwa form one nimetoka zangu kula MSUBA form two mmoja anaitwa GODWIN akaja unaniletea za kuleta kisa mimi NJUKA,akanipiga kibao,daah niliokota wembe uliokuwa juu ya Loka langu nikamchanachana mwili mzima,alivuja damu balaa!!!!daah Box 2 Forever
 
Back
Top Bottom