Somo: Chagua mapema makazi yako ya kudumu kwa ajili ya familia yako

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,554
Kutokana na sehemu tulizokulia, kusoma n.k, watu wengi wamekuwa na tabia ya kuhangaika huku na huku bila kujua wapi ataishi na familia yake. Hapa namaanisha location (Wilaya, Mkoa)!

Kwanza tuelewane, hapo ulipo ndo unaishi hivyo na miaka inakwenda hivyo, mwisho wa siku unastaafia/kuzeekea hapo...

Chagua, Chagua ya wapi uishi ni tatizo la watu wengi sana.

Mtu amekulia Dsm, akipangiwa kazi Katavi huko Tanganyika, anajipa moyo eti "hapa mimi napita tu, lazima nihame"!

Kwahiyo kwa mentality hiyo, mtu huyo hawezi kutafuta fursa za kiuchumi na kuwekeza, kwasababu anaamini anapita tu!

Hapo ulipo sasa hivi ,tafuta eneo jenga makazi yako, fungua biashara, tafuta fursa zingine maana ndo hapo unapoishi kwa wakati huu. Jikite hapo kiakili na mengineyo mengi. Hamishia familia yako hapo maisha yaende.

Kuna wazee kuzeeka halafu mwisho wa siku unakuta kaacha viwanja huko mikoani, havijaendelezwa, unawapa matatizo familia (hasa akifa).
 
Vipi ukiwa sehemu ambayo utahamishwa kila baada ya miaka 3 au 5?

Wazo la kuchagua sehemu ya kudumu ni zuri ila ukiwa Katavi huko ndani ndani usalama wa familia yako unamwachia nani?
 
Wazo zuri chagua wapi pa kuzeekea yaani zunguka Tz nzima,dunia nzima lakini makazi yako ya kudumu yawe sehemu au mkoa, wilaya ,kata fulani
 
Kuna mama anafanya kazi serikalini.

Kwa miaka aliyokaa serikalini amehamishwa mikoa 11 nako huko amejenga nyumba na kuwekeza.

Sahivi anakaribia kustaafu ameamua arudi Moshi mazima.

Investment zake zote zimekosa msimamizi anafikiria hata kuziuza. Manake mtoto wake hana hata muda wa kuzihangaikia.
 
Back
Top Bottom