Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,554
Watu wengi hasa wafanyakazi wanaohama hama au kuhamishwa kutoka eneo moja au jingine, wamekuwa wakizeeka na kuchapika sana kimaisha kutokana na kutokuwa na msimamo wa wapi unaishi.
Kuna kada ambazo kuhamishwa ni lazima kama askari, hakimu, wakurugenzi wa halmashauri, DC, DED, DAS , wakuu wa idara etc.
Unakuta mtu kila anakohamishiwa au kuhama, anatamani pori la shamba au kiwanja ananunua na kuacha hapo. Anamwaga tu mawe.
Unakuta miaka inaenda. Familia iko Songea, wewe unafanya kazi Mara na umepanga sababu kila mahali we unanunua viwanja, unaweka mawe na kuhamishwa..Au pengine hata kujenga nyumba.
Swali, ni lini utajitawanya kuishi sehemu zote hizo? Kwanini usiwekeze sehemu moja au mbili vizuri zaidi ili ukija kustaafu urudi huko?
Unastaafu maskini, then umeacha viwanja na mashamba mikoa kibao huko. Muda wa kufanya follow up hauna, umezeeka, familia imechoka, unakufa then unaowaacha wanadhurumiwa!
Amua mapema ni wapi utaishi na familia yako.