Somalia yaomba kujiunga na Afrika Mashariki

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,798
12,239
Somalia ambayo imekua ikijaribu kujikwamua toka vita vya miaka 20 imetuma maombi yakutaka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kenya ambayo ndio mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo imethibitisha kupokea maombi ya Somalia.

Somalia inakuwa nchi ya tatu baada ya Sudan Kusini na Sudan Khartoum kutuma maombi ya kutaka kujiunga na Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.Taarifa kutoka serikali ya mpito ya Somalia inasema kuwa wameamua kujiunga na jumuiya hiyo kutokana na hali ya kiusalama nchini Somalia kuimarika na utulivu kuanza kushuhudiwa.

Hata hivyo azma ya Sudan kutaka kujiunga na jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki imekataliwa.
Kwa sasa jumuiya ya Afrika Mashariki inajumuisha nchi tano, Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.
Mbali na nchi wanachama kuwa na ruhusa ya kufanya biashara bila vikwazo vyovote kwa wakati huu zinapanga kuwa na sarafu moja kufikia mwaka mwezi Juni mwaka huu wa 2012

Source: bbc

Je Somalia inaweza kuwa mshirika wa kuaminika? TUJADILI...
 
Back
Top Bottom