Solar power conditioning unit (PCU) ni nini?

cyber ghost

JF-Expert Member
May 8, 2015
239
158
Umeme wa uhakika kwa masaa 24 kwa Tanzania bado ni tatizo sana kwa sehemu nyingi, pia kwa watu wanaoishi maeneo yenye joto kali kama mikoa ya dar es salaam hulazimika kuwa na fan au air conditioners ili kukabiliana na hali ya joto, nyumba yenye air conditioner zaidi ya mbili hua hata gharama za umeme zinakuwa juu sana kwa siku.

Leo nataka nielezee umuhimu wa hiki kifaa na kinasaidiaje kupambana na gharama kubwa za umeme au kukabiliana na hali ya umeme kukatika katika kwa muda mrefu hivyo kusababisha uharibifu wa bidhaa kwenye friji.

Ili kuweza kutumia hiki kifaa utatakiwa kuwa na solar panels pia, kifaa hiki(PCU) kinafanya kazi kama inverter ya kawaida lakini kinakuwa na vitu vingine vingi ambavyo vimeongezwa ndani yake kuweza kuitofautisha na inverter ya kawaida.

JE NDANI YA SOLAR PCU KUNA NINI?

Ndani ya solar PCU kuna vitu sita ;
1:solar charge controller(mppt)
2:inverter
3:Grid (mains utility) charger
4:eek:utput selector mechanism
5:battery bank
6:control algorithm

Vitu hivyo vitano ni vitu vya kawaida sana kuonekana kwenye mifumo ya solar ya kawaida ila hiyo control algorithm kwenye namba sita ndio kitu kinachoitofautisha solar PCU na inverter ya kawaida au na solar charger.

Control algorithm ndio inakuwa inachagua chanzo cha umeme kuweza kuchaji betri labda iwe solar panels au grid au vyote kwa pamoja ,control algorithm pia inaweza kuamua chanzo cha umeme unaotoka nje ya PCU kupitia kwenye output selector mechanism kwenda kwenye vifaa vyako utoke kwenye inverter au kwenye grid .

Solar PCU inaweza kufanya kazi kwenye mifumo kama miwili hivi;
1: solar - battery - grid
2: solar - grid - battery

>kwenye mfumo wa kwanza wa SOLAR - BATTERY - GRID, umeme unazalishwa kutoka kwenye panels unapitia kwenye solar charger controller ambayo ndio itachaji betri pia umeme mwingine kutoka kwenye panels utaenda kwenye inverter moja kwa moja na vifaa vyako vitaendelea kufanya kazi kupitia inverter. Jua linapozama solar panels zako hazizalishi umemetena, PCU itaamua kuchukua umeme wa solar ulohifadhiwa wakati jua linawaka kutoka kwenye betri na kuupeleka kwenye inverter kwaajili ya kuendelea kuvipa power vifaa vyako, pindi hii energy ilohifadhiwa kwenye betri ikipungua mpaka kufikia asilimia hamsini(50%) inveryer ita stop kufanya kazi na vifaa vyako vitahamishiwa kwenye umeme wa grid(tanesco).

Utaona kwenye mode hii ya operation kwamba PCU italazimisha umeme kutoka kwenye solar panels ndio utumike kwanza hata kama umeme wa tanesco utakuwepo na jua litakapozama solar PCU italazimisha umeme ulokuwa umehifadhiwa kwenye betri ndio utumike ambapo nao ukiisha ndio PCU itagamishia vifaa vyako vilivyo kwenye matumizi kutumia umeme wa tanesco, so utaona kwenye mfumo huu solar ndio inapewa kipaombele cha kwanza na battery inapewa kipaombele cha pili na grid (tanesco) imepewa kipaombele cha mwisho kulingana na control algorithm yenyewe ilivyo programiwa.

Mfumo huu wa kwanza unafaa kutumika maeneo ambayo umeme wa tanesco upo muda wote yani haukatiki katiki , LENGO KUU LA MFUMO HUU NI KUPUNGUZA GHARAMA ZA UMEME (saving electricity bill cost)

>mfumo wa pili wa SOLAR - GRID - BATTERY utaona bado solar ndio imepewa kipaombele cha kwanza na grid kipaombele cha pili halafu kipaombele cha mwisho ni battery.

Kwa hiyo kwenye mfumo huu utaona kwamba solar panels wakati jua lipo zitazalisha umeme ambao utapitia kwenye charge controller ili kuweza kuchaji betri katika kiwango kinachotakiwa, pia wakati huo huo solar panels zitapeleka umeme inayozalisha kwenye inverter kwaajili yakuwezesha vifaa vyako kufanya kazi, inapotokea jua limezama solar panels hazizalishi tena umeme, solar PCU itahamishia vifaa vyako kwenye grid(umeme wa tanesco) kwa kutumia ile output selector mechanism ( changeover). Betri kwavile kwenye hii mode ya pili lenyewe ni last priority halitatumika mpaka pale umeme wa tanesco utakapo katika ndio solar PCU itaamua kuchukua umeme ulokuwa umehifadhiwa kwenye betri kwenda kwenye inverter na kuendelea kuvipa power vifaa vyako.

Huu mfumo wa pili unafaa kufungwa maeneo ambapo umeme wa tanesco huwa unakatika katika lakini mteja anataka kutumia huo umeme wa tanesco pindi ukiwepo.Pia kwenye huu mfumo utaona betri linakuwa reserved kuja kutumika wakati umeme wa tanesco umekatika.

LENGO KUU LA MFUMO HUU NI KUWA NA UMEME MUDA WOTE, na huu mfumo unawafaa watu wanaofanya biashara ambazo hazitaki umeme kukatika maana bidhaa zao zitaharibika.
 
Mkuu nakumbuka katika uzi wako fulani ulisema solar PCU ni somo tosha hivyo linahitaji Muda kufundisha. Nadhan sasa umetimiza ahadi. Nimejifunza Mengi kupitia huu uzi.

Lakini nna swali kidogo tofauti na hapa. Je inawezekana kuabadirisha ile Transformer ya kwenye Voltage regulator au Stabilizer na kusuka circuit ya Invetor na ile system yote iwe invetor???

Sababu naiona ile Transformer ya 1000 VAmp inafaa sana kwa matumizi ya kawaida
 
Mkuu nakumbuka katika uzi wako fulani ulisema solar PCU ni somo tosha hivyo linahitaji Muda kufundisha. Nadhan sasa umetimiza ahadi. Nimejifunza Mengi kupitia huu uzi.

Lakini nna swali kidogo tofauti na hapa. Je inawezekana kuabadirisha ile Transformer ya kwenye Voltage regulator au Stabilizer na kusuka circuit ya Invetor na ile system yote iwe invetor???

Sababu naiona ile Transformer ya 1000 VAmp inafaa sana kwa matumizi ya kawaida
Swali lako bado sijalielewa vizuri mm nilivyokuelewa kidogo ninkwamba unataka kutumia hilo box/housing ilokuwa ya stabilizer kuweka circuit ya inverter?
 
Habari zenu wadau wapi naweza pata Solar Unit ambayo
1. Inaweza run pump ya kisima (iliyozamIshwa )
2. Bulb zisizozidi 6
Nataka kujua ni watts ngapi zitatosheleza ?
Na solar panel za ukubwa gani zitatosha ?
Jee itagharimu kiasi gani ?
HP 2. Kisima urefu 70m
 
Habari zenu wadau wapi naweza pata Solar Unit ambayo
1. Inaweza run pump ya kisima (iliyozamIshwa )
2. Bulb zisizozidi 6
Nataka kujua ni watts ngapi zitatosheleza ?
Na solar panel za ukubwa gani zitatosha ?
Jee itagharimu kiasi gani ?
HP 2. Kisima urefu 70m
Pump ni ya watts ngapi? Ni single three phase?
 
Mkuu battery inakuwa ndani ya PCU? itakuwa na ukubwa gani?
 
Habari zenu wadau wapi naweza pata Solar Unit ambayo
1. Inaweza run pump ya kisima (iliyozamIshwa )
2. Bulb zisizozidi 6
Nataka kujua ni watts ngapi zitatosheleza ?
Na solar panel za ukubwa gani zitatosha ?
Jee itagharimu kiasi gani ?
HP 2. Kisima urefu 70m
Naweza kudesign hiyo system kama upo vizuri tutafutane.
 
Nimefanya wiring ya nyumba ya mama kijijini ambapo kutokana na kutokuwepo umeme karibu nimeopt kumwekea umeme wa Solar. Kipindi fulani tuliwafuata hawa wataalam wa ENSO kupata mwongozo na kujua bei zao za vifaa ambapo baada ya maongezi marefu waltuambia haya yafuatayo:-
1. Wiring yetu tulitumia wire wa 1.5 badala ya 2.5 hivyo system yetu inaweza isifanye kazi vizuri ipasavyo kwani umeme mwini utapotea (Taa zinaweza kuwa zinaungua mara kwa mara)
2. Walishauri tununue Invetor kubadili umeme wetu wote toka DC kwenda DC
Mimi siyo mtaalam hivyo naomba yeyote anayeweza kutoa ushauri wa nyongeza anipatie nami nitaupokea kwa unyenyekevu. Pia nahitaji kupata mwongozo wa wapi naweza kununua vifaa genuine vya Solar kwa bei nafuu.

Ahsante
 
Back
Top Bottom