Soko huru lenye ushindani kamili

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
643
PERFECT COMPETITION (Ushindani kamili)

Hili soko lina sifa zifuatazo:

1.Wauzaji wote wanauza bidhaa sawa au zinazofanana.

2. Wanunuaji wote wanajua bei ya bidhaa na wapi zinapopatikana.

3. Hamna viziuzi kuwa muuzaji au mnunuzi.

4. Wauzaji ni wengi.

5. Uzalishaji ni sawa na uhitaji wa bidhaa (Supply = Demand)

Mara nyingi ni ngumu kupata faida kwenye hili soko, Hii biashara ni ile ambayo gharama zake za uzalishaji zinalingana na mapato unayopata (zero profit) kama unavyoona kwenye mchoro.

Kiuchumi wanasema hili soko halijawai kutokea duniani japo zipo biashara ambazo zina tabia ya hili soko walau asilimia 90.

Mfano:

Wauza chips, wauza vitafunio, wauza vocha, wauza mazao, wauza matunda nk

Karibuni kutoa mifano ya biashara ambazo zinaendana na hili soko.

#perfectcompetition #marketstructure #economics #uchumi #sokohuru
 
OUT OF TOPIC

SOKO LA SUBSTITUTE PRODUCTS HIVI HAPA LINAWEZA KUFANANA KWELI?

MFANO PEPSI VS COCA COLA

IPHONE VS SAMSUNG
ADIDAS VS NIKE VS UMBRO

TOYOTA VS NISSAN
 
Hili soko ni imaginary na sizani kama lina exist katika dunia ya leo.

Anyways!! Thanks kwa kuikumbusha Economic 01.
 
Hili soko ni imaginary na sizani kama lina exist katika dunia ya leo.

Anyways!! Thanks kwa kuikumbusha Economic 01.
Hali exist kwa 100% ila kuna bidhaa kama matunda, mazao, vocha za kampuni flani zina tabia nyingi za hili soko
 
Hali exist kwa 100% ila kuna bidhaa kama matunda, mazao, vocha za kampuni flani zina tabia nyingi za hili soko
Buyers are aware on the prices of goods and services offered.

Many sellers and buyers at market.

Nafikiri hizi points mbili ndio zinazofanya hii market iwe Imaginary na hai exist.

Kwasababu kikawaida ni ngumu sellers kua wengi katika market na buyers kujua bei ya bidhaa husika.

Mtazamo tu!!
 
ni kweli kabisa
 
Back
Top Bottom