Soka la Zanzibar lazidi vituko, timu yashinda 50-0, nyingine 46-0 zikiwania kupanda daraja la kwanza

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,897
4,816
Na @abubakarkisandu Zanzibar.

Jana katika Michezo ya mwisho ya kuitafuta timu moja itakayopanda Daraja la Kwanza Kanda Unguja kutoka Ligi ya Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo Mchezo nambari 113 ulichezwa katika Uwanja wa Mau B timu ya Umoja wa Mbuzini ilishinda jumla ya mabao 50-0 dhidi ya New City na mchezo mwengine nambari 114 uliochezwa uwanja wa Mau A timu ya Kundemba ilishinda mabao 46-0 dhidi ya Muungano Rangers.

Kwanini wakafungana idadi hiyo ya mabao?

Hatua hiyo ilikuwa ni 4 bora inatafutwa timu 1 itakayopanda daraja la kwanza kutoka Mkoa, kabla ya mechi hizo za mwisho ambapo Kundemba ilikuwa inaongoza hatua hiyo ikiwa na alama 4 na mabao 2 ya akiba sawa na Umoja ya Mbuzini yenye alama 4 pia lakini ina bao 1 la akiba.

Kundemba na Umoja wa Mbuzini ndizo timu pekee zilizokuwa na tamaa ya kupanda daraja na kila timu ilihitaji ishinde ili ipande, lakini akili zao kwa vile michezo yote imechezwa wakati mmoja na Viwanja vya karibu yani Mau A na B basi ikapelekea idadi ya mabao kuongezeka kwa maana likifika bao la 10 uwanja wa pili wanaambiwa huku linaingia la 11, wakifika la 11 kule linaaingia la 12 na ikaenda hivyo mpaka kufika idadi hiyo ya mabao 😭.

Kwa mujibu ya Kanuni ya Mashindano ya Soka Zanzibar Msimu wa mwaka 2020-2021 zile timu zilizoachiana jana kwenye Ligi ya Mkoa wa Mjini Magharibi huenda zikapewa adhabu hii.

Kanuni inasema "Timu itakayoshiriki kwenye kupanga matokeo kwa tafsiri ya kanuni hii ya matokeo ya mchezo huo yatafutwa na hakutakuwa na timu itakayopata point na timu hio itatozwa faini ya Shilingi Milioni moja (1,000,000) ambayo itapaswa kulipwa si zaidi ya wiki moja".

Vipi kanuni mpya ya msimu wa mwaka 2021-2022 iongezee adhabu ili kukomesha upuuzi uliofanywa jana wa kupanga matokeo? Au irejeshwe kama ile kanuni iliyopita ya kwamba timu ikithibitishwa kupanga matokeo ishushwe madara mawili chini?

Credit Shaff Dauda
 
Hii imekaaje hii je FIFA walijua hili? waingize ktk rekodi zao za matukio Rare kutokea
 
Kuna goli kipa aliruka ili mpira upite tobo, huku beki akiukwepa halafu kuna mtu upande wa timu iliyofungwa akapiga makofi, daaah!
 
Zanzibar haikustahili kabisa kuitwa Nchi! Kulitakiwa kuwe na Mikoa miwili tu; Mkoa wa Pemba na Unguja.

Na timu zao zilitakiwa kupambana kama zilivyo timu kutoka Mikoa mingine ya Tanzania! Ila hii tabia ya kuibeba beba na kuichekea, madhara yake ndiyo haya!

Wanakunywa tu urojo kila sehemu!
 
Back
Top Bottom