Elections 2010 Slaa ndani ya Mtera

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
302


Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, amelia akitoa machozi kutokana na hali ngumu inayowakabili wakazi wa jimbo la Mreta mkoani Dodoma.

Kwa muda mrefu sasa, jimbo hilo limekuwa likiwakilishwa na Mbunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Samwel Malecela.

Dk. Slaa alionyesha kusikitishwa na hali duni ya maisha ya wananchi hao, hasa walipomueleza kwamba wanakabiliwa na ukosefu wa huduma za kijamii kama vile maji, shule na hospitali.

Walisema huduma ya afya wanayoitegemea kwa uhakika ni inayotolewa katika hospitali ya misheni ya Mvumi iliyo mali ya kanisa.

Dk. Slaa alisema jimbo la Mtera limekuwa na bahati ya kuwa na Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, (mstaafu), Malecela, bwawa la maji linalozalisha umeme, lakini wananchi wake ni maskini na hawana uwezo wa kupata angalau mlo mmoja kwa siku.

“Hapa tunakabiliwa na ukame ndio maana kila mwaka hatuna chakula, hamna mvua,” alilalamika mwananchi mmoja.

Hata hivyo, Dk. Slaa alisema kilimo kinachofaa kwa mkoa kama Dodoma ni cha umwagiliaji, kwa kuwa ardhi inaonekana kuwa na maji pamoja na bwawa kubwa la Mtera.
“Hatuwezi kulima kwa kutegemea mvua, kinachotakiwa hapa ni ubunifu wa namna ya kutengeneza fursa na kutumia vyanzo vya maji tulivyonavyo,” alisema.

Alitoa mfano kuwa Israel ni nchi ambayo ni jangwa lakini inazalisha mazao yanayotengeneza bidhaa zinazouzwa hadi nje ya taifa hilo.“Nenda supermarket (maduka makubwa) leo, unakuta kuna matunda kutoka Israel, wao ni wabunifu, wala hatuhitaji kumtafuta mchawi hapa,” alisema Dk. Slaa.

Dk. Slaa alihoji: “Hivi hawa viongozi wa mwenge wakija hapa huwa wanawaeleza nini, kwa sababu maana ya mwenge ni kuleta matumaini pasipo na matumaini, amani penye vurugu na upendo penye chuki, sasa ninyi hamna chakula mnaletewa mwenge wa kuleta matumaini gani?”

Alisema mwenge unapaswa kuwekwa kwenye makumbusho ya taifa ili kuweka kumbukumbu za kihistoria badala ya kuzunguka nchi nzima bila kuleta mabadiliko.

Dk. Slaa aliwataka pia wananchi wa wilaya ya Chamwino, hususani wa jimbo la Mtera, kufuatilia mapato na matumizi ya halmashauri yao na kuwaeleza kwamba kwa mwaka huu, halmashauri hiyo imetengewa Sh bilioni 11.9.

“Hatuwezi kuendelea kuezeka nyumba kwa udongo, tukitumia vibatari wakati Watanzania wengine wanatumia umeme kutoka hapa, hebu fuatilieni matumizi ya fedha hizi,” alisema.

Mgombea wa ubunge katika jimbo la Mtera (Chadema), Lamecky Lubote, alisema iwapo atapata fursa ya kuwawakilisha wananchi hao bungeni, atasomesha watoto wasio na uwezo.

Dk. Slaa anaendelea na kampeni zake ambapo leo atakuwa jimboni Chilonwa na baadaye ataelekea mkoani Manyara.

Wakati huo huo, kibao cha madai ya kutoa matusi katika siasa za kuelekea Uchaguzi Mkuu, sasa kimemgeukia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba.
Makamba alikaririwa na vyombo vya habari jana, akikishutumu Chadema kwamba kilitumia lugha ya matusi dhidi ya mgombea urais wao, Rais Jakaya Kikwete.

Mkurugenzi wa Kampeni za Chadema, Profesa Mwasira Baregu, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, Makamba anastahili lawana kwa kuanzisha lugha ya matusi.

Kwa mujibu wa Profesa Baregu, kitendo cha Makamba kumuita mgombea urais kupitia Chadema, Dk Willibroad Slaa kuwa ni mbumbumbu kama alivyokaririwa na baadhi ya vyombo vya habari, hakikuwa cha kistaarabu.

“Kauli hii imetolewa na Makamba kuwa, mgombea urais wetu ni mbumbumbu, lakini kama ni umbumbumbu na usomi, mimi naweza kulizungumzia zaidi kuliko Makamba,” alisema.

Profesa Baregu aliongeza: “Mimi nina PhD nimejifunza kuwaheshimu watu, kwa sababu kila mtu anazaliwa na akili yake, kusoma ni kumnoa mtu zaidi, lakini haimaanishi asiyesoma basi ni mbumbumbu,” alisema.

Profesa Baregu alisema inapofikia hatua ya Katibu Mkuu wa chama kama Makamba kumzungumzia mtu (mgombea) na kumuita mbumbumbu, inamaanisha hata wanaompigia kura ni hivyo hivyo.

“Ukisema mtu ni mbumbumbu unamaanisha wanaokupigia kura nao ni mbumbumbu, kwa sababu kati ya wapigakura wa Tanzania wapo ambao hawajapata nafasi ya kupata elimu, kauli iliyotolewa na Makamba dhidi ya mgombea wetu ndio matusi,” alisema.

Kuhusu matangazo ya uzinduzi wa kampeni za Chadema kukatwa katika Televisheni ya Taifa (TBC) Profesa Baregu, alisema hapakuwa na matumizi ya lugha ya matusi iliyotolewa na chama hicho kinyume cha makubaliano.

“Kilichosemwa na wagombea wetu ni ukweli na sio matusi, na Chadema hatuwezi wala hatuna nia ya kuingia makubaliano ya kuficha ukweli uliopo kwa wananchi, tutawaeleza ukweli,” alisema na kuongeza kuwa:

“Hayati Mwalimu Julius Nyerere, enzi za uhai wake aliwahi kusema kuwa, CCM inanuka rushwa na kwamba chama hicho sio mama yake, je, kauli hiyo ilikuwa tusi kwao?
“Matamshi yaliyotolewa na Chadema ni ukweli mtupu na hatuna sababu ya kuomba radhi,” alisema.

Aliongeza kuwa, baadhi ya watu waliotajwa na wagombea wa Chadema siku ya uzinduzi, kuhusiana tuhuma za Akaunti na Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuwa hawakuchukuliwa hatua, hawakuingilia uhuru wa mahakama kwa sababu hawana kesi mahakamani.

“Hatuna sababu ya kuomba radhi juu ya hilo, wakuu wa nchi walihusika moja kwa moja kwenye sakata hilo la EPA, wagombea wetu waliwataja (anawataja majina), lakini orodha hii ilishatolewa majibu yake muda mrefu, hawajaanza kutajwa leo,” alisema.

Pia alisema kuhusu suala la kilimo, mgombea wao siku hiyo alikuwa akizungumza kwa uzoefu wake aliokuwa nao zaidi ya miaka 10 bungeni.

“Upande wa elimu, tatizo lililopo limechukuliwa kama mzigo unaopaswa kubebwa, sisi Chadema tunaitumia elimu iwe ndio nyenzo ya kubeba mambo mengine kama umaskini na maradhi,” alisema.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari yaliyoulizwa kuhusiana na hali ya unyumba wa Dk. Slaa na uaminifu wake kwa Kanisa Katoliki, Profesa Baregu, alisema mgombea huyo aliacha upadre kwa kufuata taratibu za kanisa hilo na suala hilo linajulikana hadi Vatican.

“Naomba nizungumzie suala la unyumba na kanisa hilo la uaminifu na sio hilo la uaminifu, Dk. Slaa alipata baraka zote nimewahi kuzungumza na mapadre nao waliniambia kuwa wanamheshimu sana kutokana na uamuzi huko aliouchukua, kuliko angelidanganya kanisa,” alisema.

Alisema kuhusu suala la uaminifu, Chadema haina muda wa kufanya kampeni kwenye vyumba vya watu kujua nani ameoa ama kuacha.

“Sijui kwa Makamba au Kikwete vyumba vyao vikoje, Chadema hatuna muda wa kuchunguza familia za watu wanaishi vipi au wameoa wake wangapi au kuacha, Makamba anataka kutupeleka (Chadema) vijiweni kwenye masuala ya umbea,” alisema.

“Chadema tunasema hatuna muda wa umbea, tuna mambo mengi ya kufanya kwa Watanzania,” alisisitiza Profesa Baregu.

Akizungumzia kuhusu pingamizi waliloliwasilisha juzi kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, dhidi ya mgombea urais kupitia CCM, Kikwete, alisema kuwa wanaamini maamuzi yatakayofanywa juu ya pingamizi hilo yatakuwa ya haki.

Katika hatua nyingine, Profesa Baregu, ametoa angalizo kwa uchaguzi huu kuwa kama kuna mtu ana nia ya kuiba kura au kupindisha matokeo inawezekana Watanzania wasikubaliane naye.

“Tukikumbuka wenzetu Wakenya uchaguzi uliopita mambo yaliyotokea, sasa kwa uchaguzi wetu kama kuna mtu ana nia hizo mbili hapo juu, aachane nazo, uadilifu uende hadi wakati wa kuhesabu kura,” alisema.

Profesa Baregu alisema ikiwa haki itatendeka katika uchaguzi huu, mtu atakayeshindwa akubaliane na matokeo na pasiwepo ishara ya kuchezea haki za msingi za Watanzania.
Habari hii imeandikwa na Restuta James, Dodoma na Romana Mallya, Dar .
 
Last edited by a moderator:
jamani tuna hitaji na picha za huko anakozunguka kwani tv zote ni za ccm
Ni kweli. Tunaomba communication team ya Chadema watuletee angalau picha hapa JF au pia watuwekee clips za video za mikutano kwenye youtube. Natamani kufahamu wapiga picha katika maeneo yote ya nchi hii ili niwashawishi waniletee picha.
 
Alisema kuhusu suala la uaminifu, Chadema haina muda wa kufanya kampeni kwenye vyumba vya watu kujua nani ameoa ama kuacha.

"Sijui kwa Makamba au Kikwete vyumba vyao vikoje, Chadema hatuna muda wa kuchunguza familia za watu wanaishi vipi au wameoa wake wangapi au kuacha, Makamba anataka kutupeleka (Chadema) vijiweni kwenye masuala ya umbea," alisema.

"Chadema tunasema hatuna muda wa umbea, tuna mambo mengi ya kufanya kwa Watanzania," alisisitiza Profesa Baregu.
Tunahitaji majibu kama haya ya kistaarabu mtu anajibu katulia si kama Makamba ambavyo huwa anajibu, kwa hili tuseme ukweli CCM ijifunze ustaarabu wa Chadema.
 
Nilipofika Mtera mwaka 2008 sikuamini kabisa kuwa hili ndiyo jimbo lilioongozwa na "kisiki" ktk serikali ya TZ kwa muda mrefuna ambaye kawahi shika nafasi zote kuu nchini TZ isipokuwa tu U-Rais;sikuelewa na hadi leo sielewi zile kauli za Mzee JCM kuwa kawaletea maendeleo wana Mtera alikuwa anatumia vigezo gani!

Kiufupi;wana Mtera ni sawa na "biafra"mpya ya TZ,maana ingawaje wana utunza mradi wa umeme mkubwa"pengine"kuliko wote nchini TZ lkn wakazi wa mji ule wala hawafaidiki na lolote kutoka ktk mradi huo wakiachiwa tu uchafuzi mkubwa wa mazingira unaotokana na matumizi ya ufufuaji umeme wa bwawa lao!

These constituents need masive change in deed!
 
Du! Dk. Slaa kumbe ana machozi ya karibu kama PM Pinda?

Tofauti ni moja anawalilia masikini na mwingine Albino . . . .

Mwaka huu tutaona na kusikia mengi.
 
Yaani acha tu: Baregu amesema nini? "...Ukisema mtu ni mbumbumbu unamaanisha wanaokupigia kura nao ni mbumbumbu, kwa sababu kati ya wapigakura wa Tanzania wapo ambao hawajapata nafasi ya kupata elimu, kauli iliyotolewa na Makamba dhidi ya mgombea wetu ndio matusi..."
Mh Makamba(hapana Bw Makamba) anawatukana watanzania! Takwimu zinaonyesha sasa hivi wasiojua kusoma na kuandika (tukiamini aliyepata darasa la saba atajua kusoma) ni zaidi ya 40%, na wale ambao wamesoma zaidi ya darasa la saba hawafikii 20% hivyo Makamba amewatukana zaidi ya watanzania 80%! Makamba, unatutukana!!!!

Dr Slaa pole pole, machozi yakikutoka yaondoe haraka, vuta ujasiri, uone jinsi ya kuwasaidia hawa watu. Mahali kama Mtera ambako kuna maji mengi hapapaswi kuwa na ukame. Nyanda zile za juu zinaweza kumwagiliwa kwa kuchimba visima kina chake kifikie mabonde ya Mto Mtera na vianzio vingine. Ni ubunifu tu!!!
 
Unajua, ukitembelea Tanzania, hasa vijijini unaweza kugundua kwanini Dr. Slaa anawalilia wananchi, kutokana na maisha kuwa magumu na jinsi walivyo kata tamaa. Kwa sababu ya uduni wa elimu hawaelewi kwanini maisha yao yako hivyo!
 
Unajua, ukitembelea Tanzania, hasa vijijini unaweza kugundua kwanini Dr. Slaa anawalilia wananchi, kutokana na maisha kuwa magumu na jinsi walivyo kata tamaa. Kwa sababu ya uduni wa elimu hawaelewi kwanini maisha yao yako hivyo!

Alafu ni hao hao walikuwa wanadanganywa na Kikwete juzi juzi tu na wanashangilia:confused2:
 
It is very touching! ni kweli maisha ya mtanzania tu anaeishi dar es salaam bado ni maisha duni sana kwa standard za maisha binadamu anayostahili kuishi ndani ya nchi huru na yenye amani sasa hebu tujiulize mtu wa mtera au ikwilili yatakuwa katika standard gani, yaani nyumba wanazoishi hata mnyama hastahili kuishi kwa sababu ya kuwa na viongozi wasiokuwa na uchungu na vision kwa taifa letu kama wakina makamba, kinana, JK, Malecela na wengine wengi wamejaa kwenye system.

Na tatizo la umaskini wa wanyonge kama hao ndo mtaji wa ki siasa wa CCM, wewe angalia watu wenye kiu ya kuleta mabadiliko na wafuasi wa CHADEMA au CUF ni watu waliopata elimu na wanauelewa wa juu sana, but kundi linalosapoti CCM wengi ni mafisadi wana mrija ndani ya serikali au CCM ama ndugu zao na kundi lingine ni watu maskini, wanyonge, wasiokuwa na elimu na hawana ufahamu wa kutosha wa kupambanua mambo, hivyo ni dhahiri kabisa CCM wananufaika moja kwa moja na umaskini wa watanzania wanyonge.
 
Back
Top Bottom