nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Na Mwandishi wetu - Tanzania Daima
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbord Slaa, amelipua kombora jingine kwa kuziweka hadharani kampuni zilizoshindwa kurejesha fedha za madeni ya malipo ya nje (EPA) kwa kile alichokiita kukingiwa kifua na vigogo wa serikali.
Hatua ya Dk. Slaa imekuja ikiwa ni siku mbili tu tangu alipomshukia Rais Jakaya Kikwete akimsakama kwa kushindwa kuwashughulikia watuhumiwa wa ufisadi na kutatua matatizo ya kiuchumi ambayo yameiyumbisha nchi.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Dk. Slaa alisema kuwa pamoja na kauli za ukali zilizotolewa na Rais Kikwete muda mrefu uliopita, akiwataka waliokwapua fedha za EPA kuzirejesha kwa hiyari yao wenyewe na kutishia kuwachukulia hatua za kisheria, hadi sasa ni kampuni nane tu kati ya 21 zilizorejesha fedha hizo.
Alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa Rais Kikwete amekaa kimya bila kuchukua hatua wala kusema chochote dhidi ya kampuni zilizodharau agizo lake na kwamba inaonyesha ni jinsi gani serikali na CCM imeelemewa na ufisadi na imeshindwa kuchukua hatua kwa kuwa ufisadi umejikita katika mfumo mzima unaowagusa pia viongozi waandamizi katika chama na serikali.
Alionya kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kutekeleza wajibu huo, namna pekee ya kusimamia uwajibikaji ni kwa kuunganisha nguvu za wananchi katika kutetea rasilimali za taifa.
Slaa alitaja kampuni zilizorejesha fedha hizo na kiasi katika mabano kuwa ni Bencon International Ltd iliyorejesha sh bilioni 7.96 kati ya bilioni 10.56 ilizokwapua; Njake Hotels and Tours & Njake Enterprises Ltd iliyorejesha fedha zote sh bilioni 2.225; na Ndovu Soap sh bilioni 1.548 ambazo ni kiasi chote ilichokuwa imekichukua.
Nyingine zilizorejesha fedha zote zilizokuwa zimechotwa ni pamoja na Kagoda Agriculture, (bilioni 34.781), VB & Associated (bilioni 9.227), VB Holdings Ltd (bilioni 5.148), Venus Hotels & Apartments Ltd (bilioni 4.050) na Bora Hotels & Apartments Ltd (bilioni 5.779).
Hata hivyo, alizitaja kampuni 13 ambazo zimegoma kurejesha fedha hizo (majina tunayo) na kwamba hazijalipa jumla ya fedha zote zinazokisiwa kufikia sh bilioni 50.
Dk. Slaa alidai kuwa CHADEMA ilitarajia kwamba mwaka 2011 ulikuwa wa kukamilisha uchunguzi na uchukuaji wa hatua dhidi ya wahusika katika kashfa mbalimbali ili kurejesha utamaduni wa uwajibikaji. Badala yake serikali imeendelea kuahirisha kuchukua hatua kamili serikalini, bungeni na hata ndani ya chama chenyewe.
Aliongeza kuwa katika hali ya kusikitisha Rais Kikwete katika hotuba yake kwa taifa ya Disemba 31, 2011 hakuzungumzia hatua ambazo serikali yake imefikia katika kushughulikia mafisadi.
Juzi akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na hotuba ya Rais Kikwete ya kufunga mwaka, Dk. Slaa alidai kuwa hali ya uchumi inazidi kudorora na serikali haionyeshi mikakati yoyote ya kulinusuru taifa.
Alisema kuwa badala yake, Rais Kikwete amekuwa akitoa majibu yanaisukumia lawama hali mbaya ya uchumi ya kidunia, wakati angeweza kufanya jitihada za kuondokana na hali hiyo, na hasa kuwachukulia hatua watu wote wanaotuhumiwa kuhujumu mali ya taifa.