Siyo TANESCO tu hata TTCL ni Kichefuchefu kingine

senzighe

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
1,979
1,512
TANESCO hawana jina zuri kwa sasa mbele ya wananchi kutokana na kukatika ovyo kwa umeme lakini hawa TTCL ni wa ovyo na wazembe kupindukia. Maeneo ya Oysterbay takriban mita miatatu hivi kutoka ofisini kwao kuna nguzo ya simu ilianguka yapata siku kumi hivi zimepita.

Hii nguzo imeangukia kwenye makazi ya watu na inaonekana kwa chini ilishaoza. Hii sehemu watoto wa hili eno huwa wanacheza mara kwa mara lakini jambo la kushukuru hii nguzo ilianguka wakati watoto hawapo.

Jambo la kushangaza walikuja TTCL wakaliona tatizo na nyaya za simu wakaziunganisha nguzo ikiwa imelala chini hapohapo ili simu ziendelee kufanya kazi. Toka siku hiyo wameondoka hawajarudi tena na nguzo imelala chini na nyaya zake katikati ya makazi ya watu. Tunawataka wahusika wachukue haraka kuliondosha hili tatizo.
 
Back
Top Bottom