Sitta: Wabunge wamedhalilishwa

kwani wabunge wana kinga yoyote kisheria??, au wao wako juu ya sheria??, huyu 6 vipi!.

Tatizo la kukurupuka.... Tofautisha kati ya KINGA ya KISHERIA na KUWA JUU YA SHERIA.

Soma maelezo ya 6 utaelewa

Walimu mna kazi kwelikweli na ndo maana kuna mtu wa kwanza na wa Mwisho.
 
Hosea alishawambia wabunge siku mmoja kwenye kikao live, kuwa "wanamfuata fuata sana" nayeye atawachunguza wanavyochukua posho mbili mbili za serikali ofisi ya bunge na kwenye mashirika ya umma.

Lakini hii kama alifikiri litamsaidia waogope kumsulubu bungeni , basi amechemcha, Hosea ameingia choo ya kike!!! Ajaribu kupima ufisadi unaoongelewa hapa ni wa Bilions of money, nayeye anaongelea viposho vya vikao havizidi laki 2!!! wapi na wapi!!!!!!!!!!!!

Hiyo maana yake Hosea alikuwa anakiri kwamba yeye ni mhalifu, lakini kwa kuwa wabunge wanamfuatafuata nayeye atawaanika wabunge na madhambi yao.

Very funny! Kauli kama hiyo ni sawa na mtoto mdogo asemapo anaiba matunda kwenye friji kwa sababu anamwona kaka yake naye akiiba humo. Anajua ni kosa lakini analihalalisha ili kukosea na yeye pia.

Leka
 
Nilikuwa mtu wa mwanzo humu kulizungumzia hili suala la posho haramu wanazopewa Wabunge na Mawaziri wetu kutoka kwenye taasisi za UMMA. Msidhani ni posho za kawaida ni mamilioni. Jumla yake kwa mwaka ni zaidi ya pesa za EPA mnazopigia kelele humu. Kwa Mawaziri na taasisi na zilizo chini ya wizara zao ni kufuru kabisa.
Hivyo ndivyo unaweza ukaueleza utajiri wa wanasiasa wetu wengi kama akina Prof Kapuya na NSSF yake; Mwandosya na mamlaka za maji mijini; Kawambwa na mameneja wa TANROADS, THA,...;
Hizi "posho" ndizo zimemtoa Sumaye wakati ule na Tume ya JIJI.
 
wellsaid Mkuu maana naona watu wengi wanawatetea wabunge hizi si pesa kidogo ati! Ishu hapa ni kua mtu kaenda kinyume na taratibu so haijalishi kama ni hosea au mbunge...vilevile naomba niulize ivi Kinga ya Mbunge ni akiwa bungeni akijadili hoja ua hata Nje ya Bunge bado inaapply?
 
"Niliwaambia kuwa kweli nimechukuwa posho hiyo kama takrima na wala si kosa kwani ni taasisi tofauti kama ingekuwa ni ofisi moja hili lingekuwa ni kosa.

Mkuki kwa nguruwe matamu, kwa binadamu... Mie naona hilo ni ukosefu wa maadili na ni rushwa. Kuita takrima ni kulainisha tu lugha tu. Yaani makelele yote kumbe wanatafuta ulaji wao kiaina ila ni nafasi tu hawajapata.

Sita awaache takukuru wawashugulikie na huo ndio mwanzo kuacha sheria ifuate mkondo wake.
 
hapo wote wana makosa,kwanza Six alivyojibu ni as if wabunge ni untouchables, kitu ambacho ni wrong, pili PCCB kuhoji vihela wanavopewa wabunge vya posho tena kazi wanayoifanya sio sahihi, hilo lingeishia bungeni kwa wabunge kupewa muongozo kuwa posho itolewe either bungeni au wherever basi, hiyo naweza kuiita sio rushwa bali malipo yasiyo sahihi, yani double payment,haijafanywa kwa siri ikumbukwe wala hawajagushi nyaraka yoyote, so ilikuwa ni karipio basi.PCCB mbona hawadeal na kina RA? nani asimjua huyu jamaa hata kupanga uongozi wa nchi as if yeye ni team coach? kuna siri au woga gani hapa? PCCB wanachemka hapa, na hili ndo tatizo la wao kuwajibika kwa raisi direct, hiki chombo kingetakiwa kuwajibika bungeni direct, tena waingie na vikao vya bunge watoe live conv.
 
Hii issue ya posho kwanini itokee wakati huu wakiwa wanajiandaa kwenda bungeni kwenye mambo ya Richmond?? Huyu Hosea kwanini hajaanza na Mawaziri wanaoongoza kupokea hizi posho mara mbili ya hawa wabunge??

Nimesoma gazeti la Rostam (Mtanzania) akikoleza hii issue kuwa Mwakyembe abanwa, ni Amri kutoka kwa Rais ndo aliyeagiza wachunguzwe!

Huyu RA bila kumrudisha kwao alikozaliwa nchi hii haitakuja kupata amani.
Ameendeshana na Mengi huko huko TAKUKURU, sasa anapitia mgongo wa nyuma kuwaburuza wabunge wanaopokea viposho sababu ni kuisema richmond. Kwanini wasipokee posho hizi kamati zimefanya mambo makubwa kwani serikali ilishakufa kama siyo hizi kamati.

Chukulia kamati inayoongozwa na Slaa, Zitto, Sherukindo, n.k wamefanya magauzi makubwa, sasa hivi wanataka kuwapaka matope!
 
Either watu huwa hamsomi au mna kumbukumbu ndogo, huu uchunguzi ulishaanza siku nyingi na hata hapa kuna thread nyingine inaongelea.

Hawa waheshimiwa hasa wa hiyo kamati ya madini, walikuwa wanachukua pesa huku na kule kinyume cha sheria.

Tuache kuangalia sura za wahusika tunapochambua wakosaji.

Ukiongoza mapambano ya vita vya ufisadi inatakiwa yawe kwa matendo na sio kwasababu tu wewe huna nafasi ya kufisadi. Kama wamepewa mwanya wa kufisadi na wamechukua pesa, wakipewa nafasi kubwa itakuwaje?
 
27th October 2009

The Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) has said that it would not like to enter into debate with politicians on the going exercise of interrogating members of parliament alleged to have received double allowance payments.

PCCB's Public Relations Officer Doreen Kapwani said there was nothing to argue about because the anti-corruption watch-dog "is doing its job professionally" according to the laws of the land.

She said PCCB would continue to investigate the matter without any fear. She said the Bureau has powers to interrogate any alleged form of corruption scandal in the country.

"We will make sure that all corrupt people are effectively punished according to the law without any discrimination," said Kapwani.

Kapwani said that people should not mix the issue of interrogating some MPs with Richmond scandal. She refused to name legislators to be interrogated saying doing so would affect investigations.

A total of 3,780 allegations have been received from January to August this year whereby 584 cases have been investigated. PCCB has finalized investigation of 834 cases. A total of 137 new cases have been filed in different courts in the country.

Meanwhile PCCB has launched a book titled ‘Makosa ya Rushwa katika Chaguzi Tanzania,' (Election flaws in Tanzania elections) with the aim of helping the public to identify corrupt candidates in the coming general election.
Currently there is serious dialogue concerning MPs who have been receiving double allowances during parliamentary committee meetings and when visiting public institutions.

SOURCE: THE GUARDIAN
 
Hadi hii leo TAKUKURU haijathubutu hata mara moja kumhoji papa fisadi Rostam Aziz katika ufisadi wake chungu nzima alioufanyia nchi yetu pamoja mafisadi wengine akina Idrissa Rashid, Chenge, Mzindakaya na Mkono kwa kuhusika kwao na kuchota mabilioni ya shilingi pale BoT, lakini wamekuwa na speed ya ajabu kuwahoji Wabunge waliodaiwa kuchukua masurufu mara mbili. Hii inaonyesha wazi jinsi TAKUKURU walivyo na priorities zao kinyumenyume.

Hapa Babu unachanganya mambo:-

1. Ninavyo fahamu mimi Rostam, Idris Rashid, Chenge, Mkono wote wamekwisha hojiwa na Takukuru. I am not sure about Mzindakaya na pia sijui ufisadi wake ni upi?

2. Ninavyoelewa mimi, wabunge wana kinga kwa yale tu wanayoyasema Bungeni kuwa hawawezi kushitakiwa. Hawana kinga nyingine yeyote. Sitta anajaribu ku potray umuhimu usio kuwepo eti kama Mbunge akikosa ahojiwe na ofisa wa ngazi ya juu na ofisi ya Bunge ijulishwe kwanza. Sasa Mbunge kama ni mwizi atasubiriwa IGP ndiye aje kumkamata na yeye Sitta ajulishwe kwanza? Hamna sheria ya namna hiyo nchi. Hapa anataka kutuletea kanuni na kujenga matabaka katika utekelezaji wa haki.

3. Hili sakata la double, triple au quadruplicate allowance payments wala wasilaumiwe Takukuru. Utakumbuka kuwa ni Dk. Mwakyembe huyuhuyu, katika majibishano ya sakata la Dowans, ndiye aliye m-challenge Zitto kuwa kama kweli yeye anauchungu na nchi yake ni vipi anachukua posho Tanesco wakati anapata posho ya Bunge. Hapa ndio kuna ule msemo kuwa mchimba kisima huingia mwenyewe. Mimi sikuamini macho yangu kusoma kuwa Dk. Mwakyembe anaomba kwa maandishi kinga ya Spika asihojiwe. Yeye ni nani? Mbona wabunge wengine walikubali?

4. Suala hili limedhihirisha wazi kuwa hawa wabunge wetu wanaojiita wapiganaji hawana kabisa moral authority. Nilitegemea kutoka kwao kuwa wangelipima jambo hili kama ni haki na sahihi au ni makosa badala ya kujitafutia kinga. Utakumbuka hivi karibuni tu huko Uingereza, wabunge walikuwa wakichukua, KISHERIA, marupurupu ambayo baadaye yalionekana kuwa yalikuwa si haki kuyafanya. Baada ya kubainika hivyo, walilazimika kwa hiari kurudisha malipo hayo japo walikuwa na haki ya kuyadai. Sasa hawa ndugu zetu kwanza wamechukua posho hizi kwa udanganyifu kwa kuwaghilibu walipaji kuwa hawajapata posho hizo, na baadaye wanaleta excuses za hovyo hovyo.

5. Kwa kweli matamshi ya Sitta yanasikitisha sana eti posho hizo ni sawa kama wangepewa chakula na mashirika hayo. Kwanza ni kwanini wapewe chakula na mashirika hayo wakati tayari wamekwisha pewa pesa za chakula na Bunge. Shelukindo naye anasema eti pesa hizo ni takrima. Takrima ya nini, na watawalipa vipi watu walio wakirimu? Kwa kuwa wapole katika kuyachunguza mashirika hayo? Hii si ndi maana ya rushwa?

6. Kwangu mimi huu ni wizi wa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na ni criminal offense. Takukuru iendelee na kazi zake. Kama wao watambana Hosea hilo ni jambo jingine. Lakini nao wabanwe tu.

7. Jee mzee Mapesa amefikia wapi na uchunguzi wa ulaji wa Ofisi ya Bunge? i.e Shs. 70.0m. Sitta lazima awajibishwe kama alivyowajibishwa mweziwe Mongella kwenye Bunge la Afrika.
 
Soma habari hii ya mwezi nwa nane:

Confirmed: PCCB Chief investigates lawmakers​

By Rodgers Luhwago

9th August 2009

Hoseah.jpg

Dr Edward Hosea

Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) is at an advanced stage of investigating dozens of Members of Parliament accused of receiving double payments in allowances amounting to billions of shillings from various ministries and state owned corporations.
The allowance scandal comes just four months after the UK's parliament was rocked by the expense cheating saga that claimed scalps from political parties, including the ruling party. Following the expense scandal, dozens of MPs resigned after being implicated in the cheating saga.

It also comes at a time when lawmakers are asking to raise their salaries at par with the MPs of countries with exponentially higher budgets. The MPs, who currently make Sh7million ($5,292) per month - only Sh1.8m/- of which is their taxable basic salary - want to increase their basic salary to Sh3million and additional allowances to Sh9 million.

The proposed Sh12 million ($9,07 package would put the Parliamentarians in the range of Kenya's MPs, who earn a minimum of Ksh851,000 ($11,335) every month, of which only the basic salary of Ksh200, 000 ($2,664) is taxed. Some of the allowances making up additional Ksh651,000 ($8,560) include funds for gym memberships and unspecified ‘entertainment' costs.

The PCCB move also comes just after last week's tough stance over the anti-corruption Czar Dr Edward Hosea. The MPs called for his resignation accusing him of failing to detect corruption during his Richmond investigation in 2006.
Alarmed by demands of hefty allowances from lawmakers, some permanent secretaries and the chief executive officers of state owned corporations have complained about the MPs' behaviour to demand sitting allowances, The Guardian on Sunday has learnt.

The government directed PCCB to investigate whether in demanding double payments of sitting allowances despite being paid by the Parliament, the lawmakers broke the law or not and a senior PCCB official confirmed to this paper that very soon the public would be informed on this matter.

Declining to be named citing the sensitivity of the matter, the official said: "We started our investigation about a month ago after receiving instructions from the government…we are at the advance stage."

Contacted for comments on Friday, the anti graft Dr Hosea said: "I am barred by the law from discussing or giving details of those being investigated by my bureau. "The only thing I can tell is that investigation is there and we are still going on." The anti-corruption Czar told The Guardian on Sunday.

This paper has also established that nearly all members of key parliamentary committees will be investigated after their names were recorded as recipients of hefty allowances from various ministries and state corporations.
Contacted this week, the Clerk of the National Assembly Dr Thomas Kashilila said: "It's true but I have no mandate to speak about investigations being done by PCCB or any other law enforcement organs."

A senior executive officer of the Parliament who preferred anonymity admitted having knowledge of the investigation, admitting he was among officials interrogated last month.
According to him, the anti-corruption body's decision to venture into the investigation emanated from the complaints lodged by the ministries, departments, authorities and institutions to the government over double payments to committees' members.

The investigations are meant to find out the circumstances under which institutions paid money in the form of allowances to MPs whenever they visited them.
"The alleged extra money paid to MPs whenever members of the Parliamentary Standing Committees visit institutions is illegal because the Parliament pays for everything, including transport, accommodation and meals when the committees are at work," said the executive officer, adding:
"This problem did not start recently, it's a longstanding menace. It also created headache to the previous Parliaments," he added. Dr Thomas Kashilila has said, "It's true but I have no mandate to speak about investigations being done by PCCB or any other law enforcement organs." Contacted yesterday, the Chairman of the Parliamentary Standing Committee for Constitutional, Legal and Public Administration George Lubeleje said : "I am not aware of what you are talking about… After all I don't receive double payments because it is a criminal offence," he said.
Mohammed Missanga, Parliamentary Standing Committee for Infrastructure committee chairman also denied having any knowledge on the subject: "I don't' have such information…I think the Speaker or the Clerk of the National Assembly are the right people to talk about it because it is a Parliamentary affair." he said.
Public Accounts Committee (PAC) Chairman John Cheyo, on his part, too said he was not informed about the case. "To be frank I don't have any information about the matter but surely there is no MP who can demand money from any person or institution," he said. Other chairpersons of the Parliamentary Committees could not be reached yesterday to give their views on PCCB's move.

SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY
 
Hapa nikuangalia sheria ya allowance hizi hapa nchini inasemaji (Utumishi) kwani siyo wabunge tu wanaopokea allowance mara mbili, mawaziri, viongozi serikalini, ukichunguza kwa umakini waandishi wa habari kwenye hili nawenyewe wanahusika.

Itangazwe kuwa ni makosa kupokea mara mbili kwa siku allowance kwenye vikao viwili siyo kuwashushia heshima wabunge.
 
kwani wabunge wana kinga yoyote kisheria??, au wao wako juu ya sheria??, huyu 6 vipi!.
Elewa hoja hajasema hawawezi kushitakiwa.Amesema lazima ofisi yake itaarifiwe na anayehoji lazima awe ofisa wa ngazi za juu. full stop.Mbona unakuja kishabik
 
Elewa hoja hajasema hawawezi kushitakiwa.Amesema lazima ofisi yake itaarifiwe na anayehoji lazima awe ofisa wa ngazi za juu. full stop.Mbona unakuja kishabik

Hizo taratibu ziko chini ya sheria gani na kifungu kipi na kwa kosa lipi?
 
Hapa Babu unachanganya mambo:-

1. Ninavyo fahamu mimi Rostam, Idris Rashid, Chenge, Mkono wote wamekwisha hojiwa na Takukuru. I am not sure about Mzindakaya na pia sijui ufisadi wake ni upi?

2. Ninavyoelewa mimi, wabunge wana kinga kwa yale tu wanayoyasema Bungeni kuwa hawawezi kushitakiwa. Hawana kinga nyingine yeyote. Sitta anajaribu ku potray umuhimu usio kuwepo eti kama Mbunge akikosa ahojiwe na ofisa wa ngazi ya juu na ofisi ya Bunge ijulishwe kwanza. Sasa Mbunge kama ni mwizi atasubiriwa IGP ndiye aje kumkamata na yeye Sitta ajulishwe kwanza? Hamna sheria ya namna hiyo nchi. Hapa anataka kutuletea kanuni na kujenga matabaka katika utekelezaji wa haki.

3. Hili sakata la double, triple au quadruplicate allowance payments wala wasilaumiwe Takukuru. Utakumbuka kuwa ni Dk. Mwakyembe huyuhuyu, katika majibishano ya sakata la Dowans, ndiye aliye m-challenge Zitto kuwa kama kweli yeye anauchungu na nchi yake ni vipi anachukua posho Tanesco wakati anapata posho ya Bunge. Hapa ndio kuna ule msemo kuwa mchimba kisima huingia mwenyewe. Mimi sikuamini macho yangu kusoma kuwa Dk. Mwakyembe anaomba kwa maandishi kinga ya Spika asihojiwe. Yeye ni nani? Mbona wabunge wengine walikubali?

4. Suala hili limedhihirisha wazi kuwa hawa wabunge wetu wanaojiita wapiganaji hawana kabisa moral authority. Nilitegemea kutoka kwao kuwa wangelipima jambo hili kama ni haki na sahihi au ni makosa badala ya kujitafutia kinga. Utakumbuka hivi karibuni tu huko Uingereza, wabunge walikuwa wakichukua, KISHERIA, marupurupu ambayo baadaye yalionekana kuwa yalikuwa si haki kuyafanya. Baada ya kubainika hivyo, walilazimika kwa hiari kurudisha malipo hayo japo walikuwa na haki ya kuyadai. Sasa hawa ndugu zetu kwanza wamechukua posho hizi kwa udanganyifu kwa kuwaghilibu walipaji kuwa hawajapata posho hizo, na baadaye wanaleta excuses za hovyo hovyo.

5. Kwa kweli matamshi ya Sitta yanasikitisha sana eti posho hizo ni sawa kama wangepewa chakula na mashirika hayo. Kwanza ni kwanini wapewe chakula na mashirika hayo wakati tayari wamekwisha pewa pesa za chakula na Bunge. Shelukindo naye anasema eti pesa hizo ni takrima. Takrima ya nini, na watawalipa vipi watu walio wakirimu? Kwa kuwa wapole katika kuyachunguza mashirika hayo? Hii si ndi maana ya rushwa?

6. Kwangu mimi huu ni wizi wa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na ni criminal offense. Takukuru iendelee na kazi zake. Kama wao watambana Hosea hilo ni jambo jingine. Lakini nao wabanwe tu.

7. Jee mzee Mapesa amefikia wapi na uchunguzi wa ulaji wa Ofisi ya Bunge? i.e Shs. 70.0m. Sitta lazima awajibishwe kama alivyowajibishwa mweziwe Mongella kwenye Bunge la Afrika.
Usipindishe hoja.Au hujui maana ya priorities? Mchangiaji ( babu) amesema mbona kipaumbele cha PCCB ni kushughulikia pesa za vitumbua na siyo wahujumu uchumi waliyotusababishia umaskini. Hujui tuna hasira na hawa mapapa!!.Hajakataa kwamba walichofanya wabunge si kosa.Tunataka mapapa washughulikiwe kwanza ndo iwe first priorities.
 
Hoja iko palepale. Katika ufisadi hakuna upapa au upanya. Wote ni ufisadi. Ufisadi mkubwa huanza mdogo. Kama vile vile wanavyobanwa mapapa ndivyo vivyo hivyo wabanwe mapanya.

Upooo!!!
 
Back
Top Bottom