Sitta vs, Lowassa

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
Sitta ‘atafuta njia ya kumkimbia’ Lowassa Send to a friend
Sunday, 05 August 2012 01:12


ATAKA WIZARA YAKE IONDOLEWE KAMATI YA LOWASSA
Habel Chidawali, Dodoma
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amependekeza kuwa wizara yake iondolewe chini ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na iundiwe kamati yake.

Sitta alitoa kauli hiyo bungeni, mjini Dodoma juzi usiku wakati akihitimisha hoja za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/13.

Mkongwe huyo wa siasa alieleza kuwa moja ya sababu za kupendekeza hivyo ni Kamati hiyo ya Mambo ya Nje kukabiliwa na majukumu mengi hata wakati mwingine kushindwa kuitendea haki wizara yake.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Lowassa, ambaye mara kadhaa ametajwa kuwa ni mwiba kwa Wizara za Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na ile ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inayoongozwa na Sitta.

Iliripotiwa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni kuwa Lowassa akiwa kwenye vikao vya kamati yake alitaka kukwamisha bajeti za wizara hizo mbili akidai maelezo ya ufafanuzi kuhusu matumizi ya mwaka uliopita pamoja na masuala kadhaa ya kiutawala.

Kufuatia hali hiyo, kamati ililazimika kumwita Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe mbele ya kamati ili kutoa maelezo ambapo alifanya hivyo na kukubaliana na kamati hiyo.

Kauli ya Sitta inatafsiriwa kuwa ni dalili za kumkimbia Lowassa kutokana na misuguano ya kisiasa ya muda mrefu ndani ya chama chao CCM na Serikali, ambayo imekuwa ikielekezwa katika kuwania nafasi ya juu ya uongozi ndani ya Taifa.

Lowassa alijiuzulu uwaziri Mkuu, Mwaka 2008, kutokana na kuibuka kwa kashfa ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond baada ya Bunge lililokuwa chini ya uongozi wa Spika Sitta kuunda kamati teule kuchunguza kashfa hiyo.

Ingawa Sitta hakutaja moja kwa moja nini hasa atakachofanya, lakini inaonyesha kuwa hakubaliani na Kamati ya Lowassa kuisimamia wizara yake, huku akiwapoza wabunge kuwa anafanya hivyo ili kuipunguzia mzigo kamati hiyo.

Akijenga hoja ya kuundiwa kamati yake, Sitta alitoa sababu kuwa Kamati ya Mambo ya Nje inashughulikia masuala mengi ya msingi hivyo inashindwa kuwa karibu na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

“Napendekeza kuwa iundwe Kamati ya Kudumu ya Bunge itakayoshughulika na masuala ya Afrika Mashariki tu, kwani hii iliyopo sasa imekuwa na mambo mengi sana,’’ alisema Sitta na kuongeza:

“Unaweza kuona kuwa hawa wanaangalia Mambo ya Nje, wanaangalia Ulinzi na Usalama, sasa kuwapa na Afrika Mashariki ni mzigo mzito sana.’’

Hata hivyo, haijulikani kama kamati aliyopendekeza Sitta itaundwa kwa Kanuni ipi kwa kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Bunge hakuna kamati hiyo na karibu kamati zote zimekuwa zikihudumia zaidi ya wizara moja.

Maelezo ya Lowassa
Lowassa alipoulizwa na gazeti hili jana juu ya pendekezo la Sitta, alisema kuwa, haoni kama kuna tatizo endapo kamati hiyo ikiundwa kwa ajili ya kuisaidia wizara hiyo.

“Kimsingi mimi sikuwepo, lakini kama alisema yawezekana alilenga kutoa nafasi kwa Wizara hiyo kupata chombo cha kuisemea kwa karibu.”

Alisema kuwa kamati yake ni kweli imekuwa na majukumu mengi, lakini akakana kuitelekeza Afrika Mashariki.

“Ingawa si kwa mapana sana. Ilikuwapo minong’ono hiyo ya kudai Kamati, lakini hatujafikia hapo ingawa si vibaya kama itakubaliwa maana bado naamini kuwa Watanzania wengi hawaifahamu vema East Africa (Afrika Mashariki).’’


Kwa upande mwingine waziri huyo aliwataka mawaziri kuwapa manaibu nafasi za kujenga uzoefu na kujiamini katika kujibu maswali bungeni.

“Mimi siwezi kujibu swali kama naibu wangu yupo, ni lazima tuwape nafasi hawa nao wapate uzoefu kuliko kuingilia kila kitu sisi haiwezekani,’’ alipendekeza Sitta.

Alisema kuwa kama mawaziri watapendelea kujibu maswali wao, ni wazi kuwa manaibu wao watabaki kutojua mambo mengi pamoja na kutojiamini.

 
wote si wa Chama Cha Magamba!! hapo ngoma droo mi napita tu!!!
 
JK inaelekea alipokuwa mdogo alipenda kuchonganisha majogoo.
 
Kweli lowasa hatari tulijua nape anamuogopa umri kumbe hadi hawa jamaa...duh lowasa inabidi nifatlie background yake ya siasa na alikosomea politcs
 
Sitta alitumia kiti cha spika kuwaadabisha wapinzani wake kisiasa na alijua atakalia kiti milele.Na kama kweli yeye ni safi na anania njema kwa nini amkimbie Lowasa?
 
Kweli lowasa hatari tulijua nape anamuogopa umri kumbe hadi hawa jamaa...duh lowasa inabidi nifatlie background yake ya siasa na alikosomea politcs

usisumbuke sana ngoja nikusaidie siyo lazima ujue amesoma wapi siasa..ila siasa yake ya kutumia nguvu ya hela na vibaraka njaa ndiyo iko kwenye fasheni sasa CCM na hiyo inampa nguvu..bora ungetafuta kwa nini Malecela au Kawawa enzi zao nguvu yao waliijenga na nini na siasa gani? enzi zile za kolimba na wenzake siasa zilikua itikadi zaidi na ufuasi unakuja kwa utashi wa hoja na siasa za kweli siyo hela...
 
Sitta alitumia kiti cha spika kuwaadabisha wapinzani wake kisiasa na alijua atakalia kiti milele.Na kama kweli yeye ni safi na anania njema kwa nini amkimbie Lowasa?

Sitta sio mnafiki tu kama alivyojionesha jinsi alivyoibaka kashfa ya RICHMOND bali ni mwoga pia kama anavyoonesha kutaka kukimbia wigo wa kamati ya Lowassa kwa kisingizio eti ina kazi nyingi!! Ni kamati ya mambo ya nje , ulinzi na usalama inayotakiwa kulalamika kuwa ina kazi nyingi na sio Sitta kulalamika kwa niaba yao!!!
 
Sitta sio mnafiki tu kama alivyojionesha jinsi alivyoibaka kashfa ya RICHMOND bali ni mwoga pia kama anavyoonesha kutaka kukimbia wigo wa kamati ya Lowassa kwa kisingizio eti ina kazi nyingi!! Ni kamati ya mambo ya nje , ulinzi na usalama inayotakiwa kulalamika kuwa ina kazi nyingi na sio Sitta kulalamika kwa niaba yao!!!

Mkuu,asante kwa kuliona hilo.
 
Nina mashaka na uadilifu wa Mh Sitta

Sitta ni mchumia tumbo kama alivyo Lowassa na Membe pia!! Wote ni ni wezi wanaoshindana kuwa karibu ya hazina yetu ili wapate kutuibia zaidi; none of them has the interests of the wananchi at heart!! Sitta angekuwa na interests za wananchi na sio selfishness asingetumia mamillioni ya fedha za wavuja jasho kujenga ofisi ya SPIKA/MBUNGE kule urambo akifikiria angekuwa SPIKA wa maisha!
 
Kama Sitta ni msafi kwanini anaiogopa kamati ya Lowasa? Anaogopa wakigundua madudu wanayofanya kwenye Wizara yake kama walivyoiba CDA na akina Aden Rage kutakuwa hakuna mswaliemtume mbele ya mzee mamvi!
 
Mkuu Amiliki mpango wa kuunda kamati itakayojishughulisha na masuala ya Afrika Mashariki pekee yake aliuanzisha Bi Kiroboto[Spika] mwenyewe wakati wa semina elekezi kwa wabunge wa Afrika Mashariki baada uchaguzi kumalizika.Kauli ya Mheshimiwa Sitta kuhusu uundwaji wa kamati ya Afrika Mashariki ilikuwa ni kumkumbusha Spika juu ya ahadi yake nashangaa magazeti yanajaribu kuzua mambo bila kuangalia asili ya jambo lenyewe ilianzia wapi !.

Kama Sitta ni msafi kwanini anaiogopa kamati ya Lowasa? Anaogopa wakigundua madudu wanayofanya kwenye Wizara yake kama walivyoiba CDA na akina Aden Rage kutakuwa hakuna mswaliemtume mbele ya mzee mamvi!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom