Hapo penye red, huyu bwana huwa analala tu bungeni.
ingesomeka Sitta KUKAIMU USPIKA ingeleta raha kwelikweli
. mh sitta ana deserve ku-act nafasi ya waziri mkuu,huyo ni senior minister,kwani kabla ya hapo mh mohamed seif ndiye aliyekuwa akikaimuHii ndiyo nafasi iliyomgombanisha Sitta na EL. Nadhani Mh Pinda hakufurahishwa na comments za EL siku chache zilizopita alipokuwa akichangia kwenye hotuba ya bajeti ya ofisi ya WM. Siasa za Nchi hii tamu kwelikweli.
What is so special about kukaimu kwake.WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta atakahimu nafasi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuongoza shughuli za Serikali bungeni kwa kuwa anatarajiwa kuondoka nchini wakati wowote kwenda Brazil kikazi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge mjini Dodoma, ziara ya Pinda ina lengo la kuvutia uwekezaji wa nishati ya gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme.
Taarifa hiyo iliongeza kwamba tayari Brazil imeonyesha dhamira ya kutafiti nishati ya gesi katika Ukanda wa Kusini na katika mpango huo nchi hiyo imekusudia kuweka mtambo mkubwa wa kutafiti gesi ukanda wa Mtwara ili kumaliza tatizo la nishati ya umeme.
Kufuatia ziara hiyo ya kiserikali, Waziri Sitta atakaimu nafasi yake bungeni kwa wiki nzima mpaka Julai 11, mwaka huu.Mkutano wa Bunge unatarajiwa kuendelea baada ya mapumziko ya mwisho mwa wiki na wabunge leo watapokea makadirio ya bajeti katika wizara mbili zilizopo chini ya Ofisi ya Rais.
Wizara zinazotarajia kuwasilisha hotuba zao ni pamoja na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu ambazo mjadala wake utakwenda pamoja.
Wiki iliyopita wabunge walipitisha makadirio ya matumizi katika wizara na idara zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Sh 197 bilioni zilipitishwa.
Leo wabunge wataanza kupokea makadirio ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira kuwasilisha na zote zitajadiliwa kwa siku mbili.
Jumatano mpaka Ijumaa Bunge litakuwa likijadili makadirio ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ambazo zitajadiliwa kwa muda wa siku tatu mfululizo.
Asile goodtime kama bosi wake. Ajabu mkulu mwenyewe hajaamua kwenda kuwasaka hao waezuaji uchumi wetu. Wanatoa moja wanachukua mia moja na moja.
Ahsante kaka, mkono uliteleza kidogo!!nisahihishe ,wassira ni waziri katika ofisi ya rais nasio ofisi ya waziri mkuu