Sitta kuongoza shughuli za Serikali Bungeni wiki hii

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,988
4,507
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta atakahimu nafasi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuongoza shughuli za Serikali bungeni kwa kuwa anatarajiwa kuondoka nchini wakati wowote kwenda Brazil kikazi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge mjini Dodoma, ziara ya Pinda ina lengo la kuvutia uwekezaji wa nishati ya gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba tayari Brazil imeonyesha dhamira ya kutafiti nishati ya gesi katika Ukanda wa Kusini na katika mpango huo nchi hiyo imekusudia kuweka mtambo mkubwa wa kutafiti gesi ukanda wa Mtwara ili kumaliza tatizo la nishati ya umeme.

Kufuatia ziara hiyo ya kiserikali, Waziri Sitta atakaimu nafasi yake bungeni kwa wiki nzima mpaka Julai 11, mwaka huu.Mkutano wa Bunge unatarajiwa kuendelea baada ya mapumziko ya mwisho mwa wiki na wabunge leo watapokea makadirio ya bajeti katika wizara mbili zilizopo chini ya Ofisi ya Rais.

Wizara zinazotarajia kuwasilisha hotuba zao ni pamoja na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu ambazo mjadala wake utakwenda pamoja.

Wiki iliyopita wabunge walipitisha makadirio ya matumizi katika wizara na idara zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Sh 197 bilioni zilipitishwa.

Leo wabunge wataanza kupokea makadirio ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira kuwasilisha na zote zitajadiliwa kwa siku mbili.

Jumatano mpaka Ijumaa Bunge litakuwa likijadili makadirio ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ambazo zitajadiliwa kwa muda wa siku tatu mfululizo.
 
Watapata masamaha wa kulipa kodi?
 
Watapata masamaha wa kulipa kodi?
Definetly 10 years free baada ya hiyo kwisha watadai tuwaongezee mingine mitano na baada ya hapo watasema wameshindwa ikawa asubuhi ikawa jioni na siku zinakwenda wakati huo aliyeingia mkataba atakuwa ame retire na kuondoka na mafaili utamhoji nani.
 
Yeah, ur very right. Senkyu.
 
Ofisi ya Waziri Mkuu ingawa haina Naibu Waziri Mkuu lakini ina mawaziri walioko chini yake kama Bw. Lukuvi, Wasira na Bw. Mwanri,
Kwanin asishike mmoja wao?
 
Ofisi ya Waziri Mkuu ingawa haina Naibu Waziri Mkuu lakini ina mawaziri walioko chini yake kama Bw. Lukuvi, Wasira na Bw. Mwanri,Kwanin asishike mmoja wao?
Wassira hayuko WM, hao wengine ni wachanga mno kukaimu dhamana hiyo.
 
Imagine hiyo ofisi ingeachiwa kambi ya upinzani kwa wiki moja mambo yangekuwaje lets say Zitto nafikiri siku Pinda anarudi suala la posho lingekuwa historia.
 
huu ukweli kila Mtz anaujua lakini ukishakuwa serilkarini, utasikia ...."tunachunguza", "mchakato" na ujinga wote utadhani bado tuko miaka 200 nyuma!
Definetly 10 years free baada ya hiyo kwisha watadai tuwaongezee mingine mitano na baada ya hapo watasema wameshindwa ikawa asubuhi ikawa jioni na siku zinakwenda wakati huo aliyeingia mkataba atakuwa ame retire na kuondoka na mafaili utamhoji nani.
 
Hii ndiyo nafasi iliyomgombanisha Sitta na EL. Nadhani Mh Pinda hakufurahishwa na comments za EL siku chache zilizopita alipokuwa akichangia kwenye hotuba ya bajeti ya ofisi ya WM. Siasa za Nchi hii tamu kwelikweli.
 
Definetly 10 years free baada ya hiyo kwisha watadai tuwaongezee mingine mitano na baada ya hapo watasema wameshindwa ikawa asubuhi ikawa jioni na siku zinakwenda wakati huo aliyeingia mkataba atakuwa ame retire na kuondoka na mafaili utamhoji nani.

Najivumilia kuwa Mtanzania
 
nadhani sio vibaya,kwa pinda kusafiri kikazi. chamsingi hyo safari yake iwe na tija kwa taifa.
 
nitajie hata safari moja iliyokuwa natija,just one please,za kikwete usinitajie maana hakuna hata moja iliyowahi kuwa natija
 
nadhani sio vibaya,kwa pinda kusafiri kikazi. chamsingi hyo safari yake iwe na tija kwa taifa.
Tija gani unategemea ya safari hii mkuu. Anakwenda kubembeleza wawekezaji kuja Tanzania hivyo usishangae kusikia amewahamasisha kwa kuahidi msamaha wa kodi na serikali itawanunulia mafuta yakuendeshea mitambo yao wakati watoto wetu hawana hata madawati ya kuandikia. Kwa mini wawekezaji wasitufuate sisi wenye Mali? Btw-how much sitting allowance he will be getting for this meeting in Rio '? My simple guess is a hefty of money.
 
Back
Top Bottom