Sitta Bungeni alazimika kutoa maelezo ya ziara yake

Lunyungu,

Tupe summary ya ripoti hususan walio husika, tutajie majina yao na uhusika wao. Mengine tuta yajua baadae tafadhali mkuu maana hata kazi sasa hazifanyiki tunachungulia chungulia huku nachelea nisije nikamwaga ugali wa watoto hapa....


Msabaha
Rostam

Karamagi
 
Nilisha sema JK is never sincere na sisi,matamshi ya kutenganisha biashara na utumishi kaja nayo baada ya tume ya Richimond na baada ya wao kupitia ripoti kwenye kamati kuu akaja kutuzuga kwamba wameamua kumbe sasa inafichuka .
 
lunyungu hii katabia ya kutubania uiache, maana umeombwa mida utupe brief sasa unaturambisha rambisha maana yake nn?

mwaga vitu tujuwe wametajwa kivipi?
 
lunyungu hii katabia ya kutubania uiache, maana umeombwa mida utupe brief sasa unaturambisha rambisha maana yake nn?

mwaga vitu tujuwe wametajwa kivipi?

Kwa kweli mh Lunyungu, tupe briefing wahusika wakuu, mapendekezo ya kamati na way forward...simple
 
Watu walio matatizoni ni hawa:
Msabaha
Mwakapugi
Karamagi
Hosea - PCCB
Mwanyika (Mwanasheria Mkuu wa Serikali)
EL japo kamati imetoa option ya yeye mwenyewe kuangalia uzito wa ngoma then aamue kusuka ama kunyoa.

Nimefurahishwa na ushangiliaji wa Mama Anne Kilango na jinsi alivyo mpongeza Mwakyembe kwa kazi nzito.

Sikufurahishwa na Mwakyembe alivyokuwa anauma na kupuliza kwa EL kwamba inawezekana anaandamwa na wabaya wake, japo yeye EL 'inawezekana' alikuwa na NIA NJEMA au ndiyo style yake ya ufanyaji kazi.

Nje ya Kiapo kwamba RDC ilikuwa ni mradi wa Big Brother EL na mshiriki wake wa kibiashara RA. E-mail address za caspian zilitumika kwenye some documents! Yaani hapo ni madudu kwa kwenda mbele.
 
Mtu wa Pwani,

Ngoma leo ilikuwa nzito sana. Mawaziri wote walikuwa kama wamenyewa mvua kwa jinsi mawe yalivyokuwa yanaishukia serikali. Kwa kifupi ni kwamba serikali imeanikwa hadharani. Point za maana nilizoziona kwenye report ni hizi:

Moja, Kamati Teule inasema kwamba Wizara ya Nishati na Madini ilipata kiburi kutoka juu na ndiyo maana ilifika mahali ilikiuka maamuzi ya Baraza la Mawaziri. Hapo ni MSABAHA ndo alikuwa anakomwa za usoni bila ya woga.

Kutokana na ushahidi wa kimazingira pamoja na mawasiliano kati ya Wizara ya Nishati na Madini na Waziri Mkuu, it seems kwamba Waziri Mkuu aliingilia huo mchakato na Wizara ilikuwa inafanya kazi kwa maelekezo ya Waziri Mkuu. Msabaha na Kazaura walijitetea kwamba huo mradi ulikuwa wa EL na RA (lakini maelezo hayo yako nje ya kiapo na hivyo kamati inayachukulia kama minong'ono).

Mwanasheria Mkuu wa Serikali hakujua lolote linaloendelea kwenye hiyo mikataba mibovu yenye 'UJASIRI WA KIFISADI", kwa hiyo nae ametakiwa awajibishwe.

PCCB wanatakiwa kubadilishiwa uongozi kwa kuwa report yao ilisema mambo yalikuwa poa wakati wao (Kamati) wamekuta kuna uozo, na hivyo PCCB imepoteza imani kwa wananchi.

Timu iliyoundwa na EL kwa ajili ya majadiliano ikiwakilisha serikali imetakiwa iwajibike (hiyo ni kamati ya makatibu wakuu wa Wizara ya Fedha, Nishati na Madini na pia Mwanassheria Mkuu wa Serikali).

Karamagi ametakiwa awajibike kwa kuendelea kutetea RDC pamoja na kujua kwamba lilikuwa ni bomu (Karamagi aliwatetea RDC mara baada ya kuingia Wizarani, nae ameangikwa msalabani).

Mamvi kapewa option ya kuchagua kusuka ama kunyoa. Kamati haijapendekeza lolote, bali wamesema kwamba kulingana na nafasi yake na ushiriki wake kwenye mchakato na jinsi ofisi yake ilivyoingilia swala hilo Kamati imesema ataangalia afanye nini kutokana na maudhui ya report.

Kamati imependekeza mikataba yote iwe wazi ili kuepuka madudu ya RDC. Na ishughulikiwe kikamilifu.

Hayo ndiyo niliyoyadaka kwa kifupi kutoka kwenye mapendekezo.
 
Watu walio matatizoni ni hawa:
Msabaha
Mwakapugi
Karamagi
Hosea - PCCB
Mwanyika (Mwanasheria Mkuu wa Serikali)
EL japo kamati imetoa option ya yeye mwenyewe kuangalia uzito wa ngoma then aamue kusuka ama kunyoa.

Nimefurahishwa na ushangiliaji wa Mama Anne Kilango na jinsi alivyo mpongeza Mwakyembe kwa kazi nzito.

Sikufurahishwa na Mwakyembe alivyokuwa anauma na kupuliza kwa EL kwamba inawezekana anaandamwa na wabaya wake, japo yeye EL 'inawezekana' alikuwa na NIA NJEMA au ndiyo style yake ya ufanyaji kazi.

Nje ya Kiapo kwamba RDC ilikuwa ni mradi wa Big Brother EL na mshiriki wake wa kibiashara RA. E-mail address za caspian zilitumika kwenye some documents! Yaani hapo ni madudu kwa kwenda mbele.

Keil

Shukran mkuu hicho ndicho nilichokuwa nakitaka, kwa hiyo in short hapo Lowasa, Msabaha, Karamagi, Mwakapugi, Hosea na Mwanyika wanatakiwa wawajibishwe period!

Ninacho shindwa kuelewa hapo will be the next step as far as Bunge is concerned? watu kama Mwakapugi na Hosea ambao si wabunge watahukumiwa vipi kwa maazimio ya Bunge?

JK kikombe kipo mezani kwako sasa ama ukiepuke au ulale nacho mbele..
 
Nimemsikiliza Mwakyembe.LOWASA hana budi kuachia ngazi.Asipoachia inabidi apelekwe Mental illlness clinic.
 
Nimemsikiliza Mwakyembe.LOWASA hana budi kuachia ngazi.Asipoachia inabidi apelekwe Mental illlness clinic.

Akigoma kutoka kama kuna wabunge wa CCM ambao wana guts na ushawishi mkubwa waweke hoja ya kura ya kutokuwa na imani na EL. Kwa jinsi wana siasa wa Bongo walivyo, anaweza kupuuza na hakuna kitu kitafanyika. Lakini kwa jinsi alivyochambuliwa pamoja na Kamati kuuma na kupuliza, bado ninamuona kachafuka sana.

Mtu mwingine wa kumshughulikia ni Marmo. Maana aliombwa report ya PCCB akagoma akaishia kudai kwamba jamaa walichunguza na kukuta mchakato ulikuwa safi!
 
rroo na iri naro rinawaigi kweri na miapari ya kudakiaga. siwaiongerea hiyo miapari kwenye ripunge. ri tvt sirinaaparishaga hiyo miapari raifu.

Can something be done about this? Seriously we dont understand this language, ni uharibifu wa kiswahili na its not funny at all. I think i am not the only one who hate this. Tuwe serius, kama mtu unataka utani kwenye nenda kandike kule kwenye jokes aina hii ya lugha si kila sehemu.
 
Nimefurahishwa na wote waliochukua muda wao na kutuhabarisha sisi ambao tumeshindwa kuwa karibu na Runinga zetu.Ni jambo zuri kila mmoja kuona analo jukumu la kuwahabarisha waTanzania wenzake masuala yanayogusa musatkabali wa nchi yetu.hiki ni kitendo cha uzalendo.Hongera JF
 
Naanza kuhisi yaleyale ya 2005 ambapo yule jamaa dr. nani yule wa znz alipojaribu kusimama na karume kugombea uteuzi wa CCM Zanzibar, aliitwa na baadaye tukasikia kuwa "ameamua" kujiondoa kwenye mchakato ili kutoleta mgawanyiko ndani ya CCM, pia kama ilivyokuwa kwa malecela aliyedai kujiondoa kwa vile "busara" zake zilikuwa zikihitajika katika uchaguzi wa presidential hopefuls, what i can see here ni kuwa tusishangae kusikia kuwa waziri mkuu Lowassa kajiuzulu ili "kurudisha" imani kwa wananchi na pia kipimo cha utawala bora etc...the bottom line is ataondoka tu, huwezi kumpa option eti kwa uzito wa nafasi yake na status yake na kuonekana kwake kwenye richmond afikirie!!!
 
Nimerudia kuangalia kile kitimtim cha leo asubuhi na Richmond nimegundua Spika ali tahayari sana na akawa anawaka na vijikanuni .Wewe unaonaje maana Sitta kweli he was almost going ballistic.
 
Back
Top Bottom